Idimi
Platinum Member
- Mar 18, 2007
- 15,506
- 11,439
Sana mkuu tupo pamoja. Sema tu kuna baadhi yetu hubadili mwelekeo wa mada wakishaona wanazidiwa hoja, ndio maana raia mwema anashangaa. Tatizo sasa kijiwe kinabadilika nakuwa cha mipasho na udaku. Mtupori kawa Idimi, kabadili jina. Sababu ni kuwa kuna mtu anajiita 'Mtu pori'. Nikamwachia jina, sitaki makuu...raia,sijui kama we ni mwema kweli,ila,karibu!
..hili baraza ni pana sana na lina kila aina ya watu,wenye kila aina ya msimamo na wengine hawana kabisaa!
..nadhani kitu cha muhimu si kuwa katika upande gani wa kisiasa,bali,ni uwezo wa kutoa mawazo ya nini kifanyike ili nchi yetu iweze songa mbele vizuri na kwa manufaa ya wengi!
..kuna kipindi issues zilikuwa zinakatwa hapa mpaka ilitia msisimko!hali si hivyo kwasasa!kwani majungu yamezidi!focus imepotea...unajikuta unaongea au kuchangia pumba!
..kama nilivyosema awali,hili ni baraza na baraza ni watu!sasa,kwenye wengi kuna mengi na ndio haya!ila,naamini ipo siku tutarudi kwenye kukata issues baada ya huu upepo mbaya wenye pepo baya utakapopita!
..wapo watu kama fd,dua,mjj,mkandala,philemon mikael,kithuku,jokakuu,masatu,invicible,kada,mwafrika wa kike,samvulachole,mtupori,fmes,drwho,mtumwitu,na wengine ambao nadhani wamebadilisha majina. hawa walikuwa wanakata ishu si mchezo...ila siku hizi....aagh!tuache huu upepo upite!
..kuwa na subra,hii ndio tanzania!
Mi naendelea kusubiri nyeti toka ndani ya Kizota Dodoma.