Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,742
- 10,728
Hii Story nimeipata mahali Baada ya kusoma mpaka Mwisho Kuna kitu nimejifunza Kwa Hawa Mapaster au wachungaji....soma tudiscuss Kwa Kina
PART 1
TABIA ZA MUME WANGU ZILINICHOSHA
ANAANZA KUSIMULIA....
Kabla ya kufunga ndoa na Mume wangu tumekuwa na mahusiano ya uchumba yakupelekeshana sana, uchumba wetu umeshavunjika kama mara tatu kutokana na tabia zake za uhuni, pombe na kupenda starehe. Sio siri Mimi nampenda sana Mume wangu sijui kwanini hata tugombane vipi baada ya muda namkumbuka tunarudiana. Kuna muda tunaachana na najaribu kutafuta mahusiano mengine lakini akirudi anavyoomba msamaha yani najikuta tu namsamehe tunaendelea. Kifupi nimekuwa na mahusiano ya kimkanda mkanda.
Nakumbuka walikuja kwetu kwaajili ya kujitambulisha wakaleta barua ya uchumba tukafurahi sana, siku mbili baada ya kunitolea barua nikakutana nae mahali ile naingia kwenye gari kwenye kiti cha nyuma kwa chini nakuta mfuko umefungwa nikafungua nakuta vitu vya mwanamke, chupi, makeup, wanja inaonyesha huyu Dada alivisahau akawa anampelekea. Aisee nilikasirika nikashuka kwenye gari nikaondoka. Nikamblock kabisa tukawa hatuna mawasiliano kama miezi miwili hivi. Alinitafuta sana hakunipata, na niliamua kwenda mkoani kwa Dada yangu kipumzika. Sikumwambia mtu tatizo langu nilinyamaza. Nikiwa mkoani Baba akanipigia simu wiki hii urudi jumamosi tunapokea wageni wanaleta ile Mahari naomba uje tumalize hili jambo. Nilishangaa imekuwaje huyu mtu tumegombaba, Hapo nastuka ndugu zangu washafika nyumbani mashangazi, wajomba Bibi babu wote walikuwa wako standby. Nikaamua nimu unblock huyu jamaa nikampigia nikamwambia naomba uache kuleta Mahari waambie ndugu zako tumeachana, weeeh wacha alie usifanye hivyo wazazi wangu wanakupenda na Mimi nakupenda nilipitiwa tu mpenzi naomba Mahari ipokelewe na nipe adhabu yoyote nitafanya, wewe ndio mke wangu siwezi ishi bila wewe
Jamani nilijikuta nimelainika nikajiandaa kurudi Dar akanipokea mwenyewe ubungo, yani mapenzi yakaanza upyaaaa.
Mahari ikatolewa, ila wakaomba harusi iwe ndani ya miezi miwili kwani ndugu zake walitoka nje ya nchi wamekuja wanataka wahudhurie harusi ndio waondoke.
Sio siri wakwe zangu wananipenda sana sana tatizo mtoto wao habebeki.
Basi tukaandaa harusi siku moja kabla ya harusi alipotea, nikimtafuta sana hapatikani usiku kucha, mpaka asubuhi yake siku ya ndoa yenyewe alikuwa hapatikani, baadae niko salon pressure imepanda akapokea simu "Hallow mke wangu, nishajiandaa naelekea kanisani" yani sijui alikuwa wapi nilikasirika sana. Basi tukaenda kanisani yani nina kinyongo tumefunga ndoa nasema nasubiri tumalize shughuli aniambie alikuwa wapi. Sasa Tumetoka kanisani tumefunga ndoa tunaelekea kupiga picha nikasema nichukue simu yake niangalie ana nini huyu mtu, yani ile napiga jicho nakutana na message anachat na mdada anamwambia
"usijali hata nikioa wewe bado wangu tulia Mama, mara sijui jana nilienjoy ukimaliza Honeymoon tutoke tena."
Ndio nikajua kumbe jana alilala na mwanamke, Yani nilipomaliza kusoma zile message nikajiuliza nimefanya nini, nimejiingiza kwenye nini, kwanini nimejifunga hivi mimi, nimefunga ndoa ya kanisani na mtu aseye jitambua. Nikajikuta naanza kulia, yani hata picha hazikutoka vizuri.
Nilipanga ukumbini nivae nguo nyingine, nikaenda hotelini kuvaa nikampigia simu Dada yangu aje nikamuhadithia kila kitu, akasema mbona sasa hukusema umekaa mpaka kimya mpaka unafunga ndoa umeshajifunga. Dada yangu akasema lakini ndoa ndivyo zilivyo vumilia tu nyumaza futa machozi twende kwenye harusi.
Basi nikavaa nikatoka nikasema ndio basi tena nimeshaingia nikapambane.
Kwenye harusi nipo tu sielewi elewi, wakaja marafiki zake kutoa zawadi watu aliosoma nao chuo vidada vinajishaua vinavishepu, nikawa nasema kimoyomoyo sijui aliyekuwa nae jana yupo hapa yani sikuwachangamkia hataaa.
ITAENDELEA PART 2
PART 2
TABIA ZA MUME WANGU ZILINICHOSHA
Baada ya harusi tukaenda Honeymoon nikamuwashia moto nikamwambia nimesoma message zako nimegundua ulikuwa kwa mwanamke, tujagombana sana baadae akaomba msamaha mke wangu nisamehe wewe ndio mke wangu Kwasasa hao wengine hawana nguvu. Daaah nilijikuta nalia baadae nikanyamaza. Tukatoka tukarudi nyumbani maisha yakaanza. Na alitulia kama miezi miwili hivi hana issue hakuna hekaheka.
Mimi na Mume wangu tulipanga nyumba maeneo ya sinza. Hiyo nyumba ilikuwa na nyumba kama tatu ikiwemo ya mwenye nyumba. Mama mwenye nyumba alikuwa na mabinti zake wawili waswahili sana, so nilipohamia hawakunipenda, wakaanza kunisema vibaya, nikifanya kitu kidogo maneno kama wananisuta. Kuna muda nawasikia wanasema " hehehe ndoa kitu gani bwana, ndoa makaratasi tu kila mtu ajilie kivyake"
Na wakikutana na Mimi hawanisalimii, lakini Mr wanamsalimia na wanaongea. Nikikaa kidogo hizo taarabu daaah mpaka nikahisi kunakitu. Ila nikanyamaza.
Baada ya muda niliumwa sana kwenda hospital nikapima nikakuta na ujauzito ikabidi nisiende kwenye kazi zangu nitulie nyumbani nipumzuke, weeeh wakaanza kusema hakuna mtu kuzaa hapa hazai mtu hapa, nikashangaa mimba ina miezi miwili wamejuaje nina mimba. Na sikumwambia mtu ni mume wangu tu ndio anajua nikahisi kuna kitu.
Basi nikakaa mimba ikawa inakuwa ikaanza kuonekana ila kila siku naumwa hata sielewi naumwa nini, nakumbuka kuna siku nikiwa na mimba ya miezi nane usiku nimelala nastuka mume wangu hayupo ndani na tulilala wote, nikazunguka ndani kila mahali hayupo, simu kaizima, nikajiambia sio kawaida ngoja nitoke nje, nafungua mlango uko wazi haujabanwa, kuna kitu kikaniambia nenda dirishani kwa hawa mabinti usikilize, nikanyata usiku huo mpaka kwenye dirisha la chumba cha hao mabinti nikasikia sauti ya mume wangu anaongea nikama walikuwa wanafanya mapenzi nilipiga kelele Mume wangu kwanini jamani uwiii nikasikia huko ndani wanahangaika nikarudi ndani naliaa, nililia sana mpaka nikaanza kujisikia vibaya, nilikuwa na rafiki yangu jirani nikampigia simu akaja na mumewe wakanichukua mpaka hospital. Niko hospital mume wangu hakuja, wakaja ndugu zake kuniona. Jioni walikuja ndugu zangu na yeye akaja ile namuona tu nikazimia ilabidi waondolewe nikapelekwa ICU nikakaa huko, baadae nikatoka hali yangu ilikuwa mbaya, pressure ilikuwa juu sana Doctor akashauri nibaki hospital nilikaa hospital mpaka wiki ya 36 nikafanyiwa operation, japo nilikaa tena hospital kama wiki nikatoka. Ikabidi nirudi nyumbani kwa wazazi niuguzwe, niliumwa sana pressure ilisumbua nilivimba, na kila nikikumbuka lile tukio nazidi kuumwa.
Nikakaa nyumbani kama miezi mitatu mtoto wangu alichangamka, Mume wangu akaja akaomba turudi nyumbani, akasema anaomba nimsamehe sasahv amepata nyumba maeneo mengine nyumba kubwa na inajitegemea hakuna watu wengine. Basi nikarudi kwangu ila vituko vinaendelea taratibu.
Tukakaa vituko vinaendelea Mara apotee, asirudi nyumbani mpaka kesho, yani hekaheka. Nikaanza kuzoea nikawa busy na mtoto wangu na kazi zangu. Baada ya mwaka nikagundua nina ujauzito tena nilistuka sana nikasema uwiiii, niliponea chupuchupu kufa Mungu nisaidie. Nikaanza kwenda kanisani kwenye maombi maana mtoto bado mdogo huku nina mimba mume hajielewi. Ilikuwa kazi kwakweli.
Nilipata binti wa kazi yule binti siku hiyo ghafla anasema Dada naomba kuondoka nikamuuliza kwanini akasema kila siku usiku shemeji ananifwata chumbani anataka tufanye mapenzi namkatalia, Mimi nakuheshimu sana naomba nirudishe nyumbani. Aisee nilijisikia vibaya basi nikamrudiaha kwao binti. Siku hiyo anarudi anauliza Dada yuko wapi nikasema kaondoka kakukimbia. Alikuwa mpole hatari. Na kama kawaida yake akiomba msamaha mpaka analia. .
ITAENDELEA PART 3
PART 3
TABIA ZA MUME WANGU ZILINICHOSHA
Mume wangu alikuwa na marafiki zake hao walisoma wote wengine wanafanya kazi pamoja jamani ni vichomi vichomi, ni kama mapopo hawatulii majumbani mwao kila mtu mkewe analalamika. Kutwa kushinda kwenye mabar na wanawake. Usiwe na shida ukasema unashemeji wa kukusaidia wote lao moja.
Kuna siku Mr aliniaga akasema anaenda Dodoma kikazi akasema atakaa kama mwezi ila atajitahidi baada ya wiki mbili aje kutuona. Alinifanyia shopping yote akanipa na hela za kutosha tu nikamshukuru tu. Akasema anaenda na gari lake na anawenzie anawapitia waondoke pamoja. Basi asubuhi akaondoka zake na Mimi nikaendelea na kazi zangu. Nikawa dukani kwangu maana wateja walikuwa wengi kukawa busy kidogo. Baada ya kusafiri kama siku mbili akawa hapatikani nikamtumia message vipi akasema Dodoma kuna bonge la mvua inanyesha, yani ni balaa network inasumbua na umeme unakatika sana sababu ya upepo nikasema sawa pole, nikamuacha. Baada ya siku kama mbili alinipigia simu Dada yangu anaishi Dodoma nikamwambia poleni na mvua naskia Dodoma inanyesha balaa akashangaa akasema "Mvua? Mvua gani?, Huku ni jua kali vumbi mpaka kwenye kope". Nikashangaa ila sikumwambia kitu tukaongea akakata simu.
Asubuhi nikampigia Mama Dorry ambae mumewe anafanya kazi na Mr na alisema wanasafiri wote, nikamuuliza kama mumewe yupo akasema yupo ila anarudi usiku sana na kalewa kama kawaida yake, nikamwambia Mimi Mr kasema yuko Dodoma na kasafiri na Baba Dorry na hapatikani kwenye simu anasema network inasumbua, Mama Dorry akasema hapana ngoja ajiandae aje dukani kwangu tuongee. Alipofika akasema Baba Alvin mume wangu yupo hapahapa Dar na jana alikuwa na Baba Dorry akamrudisha usiku pale kwake. Akaniambia tulia na hali yako ngoja nifwatilie kitu nitakustua. Akapiga simu ofisini akaambiwa mume wangu hayupo kazini ana likizo ya mwezi, nikajua hapa kuna jambo.
Baba Dorry ana driver wake anamuendesha na wanaelewana sana na Mama Dorry, akasema ngoja niongee nae wakiwa pamoja anistue twende. Jioni nilifunga duka nikarudi nyumbani nimepumzika Mama Dorry akanipigia akasema njoo Tabata kuna bar moja kubwa sana akasema vaa ushungi na barakoa uje. Basi nikajiandaa kufika kwenye parking nakuta gari ya Mr r imepaki. Mama Dorry akaja tukaingia ndani ile tumekaa tunaagiza vinywaji nikapiga jicho kule ukutani namuona Mr ,Baba Dorry, na mwenzao mwingine wako na wanawake zao. Tena Mr mwanamke wake kamuwekea miguu kabisa. Tukanyanyuka tukaenda Mama Dorry akamkunja mumewe huyu nani, mara Mr kuniona akaanguka chini akazimia, nilijua hajazimia nikajaribu kumburuta ili aamke hajaamka, wale wanawake walitimua mbio hatukuwaona. Wakaja watu ni marafiki zao wakajifanya wanamchukua Mr wakampeleka hospital.
Nilikasirika sana nikasema hata siendi kokote nikarudi nyumbani, nikampigia simu Mama mkwe na wifi wakaja nikawahadithia kila kitu, usiku sana tano Mr akarudi kaletwa na wenzie, anafika ndani anakutana na Mama yake weeeeh Mama akawawashia moto woteee wakaomba msamaha pale basi.
Mimi nikaona tena nishachoka nikatulia sikumfwatilia tena. Mpaka nikajifungua mtoto wangu wa pili wakiume, sikwenda nyumbani kwani Mama Mkwe na wifi walikuja kunisaidia.
Maisha yaliendelea, mapichapicha yaliendelea...
ITAENDELEA PART 4
PART 4
TABIA ZA MUME WANGU ZILINICHOSHA
Kwakweli baada ya kujifungua mtoto wangu wa pili, nilichoka sana. Nilijikatia tamaa na hii ndoa nikaanza kujilaumu mwenyewe kwanini niliingia kwenye ndoa ya namna hii, mwanaume hatulii kila siku majanga, nilijuta sana nikaanza kuwaza natokaje maana nimeshachoka.
Mr alipataga mwanamke huyu yani ilikuwa balaa, Mr hakai ndani kutwa yuko na huyo mwanamke. Alikuwa haogopi chochote huyo dada hata usiku Mr yuko nyumbani atanipigia na akimwambia aje popote pale Mr anaenda.
Mr akaanza kuwa mkali, akija nyumbani anahasira mara aseme nyumba chafu sisafishi vizuri, atanitukanaa weeeeh, mara nikipika chakula anasema kimeungua au nyama imechacha ananifokea na kunipiga vibao. Wakati nyama ni nzima na haijaharibika nimenunua buchani asubuhi, mara ukipika chakula kinachumvi mara chumvi hamna, mara akiangalia watoto anasema wachafu yani alianza kunichukia Mimi na watoto.
Hii hali ilinistua kidogo sababu haikuwa ya kawaida, Mr alikuwa anafanya mambo yake mabaya lakini akija nyumbani ni mtulivu tu ila sasahv kawa mbogo, mkali kufoka kila wakati, nyumbani halali yani tafrani. Kuna siku alisema anaenda Dubai kuna mtu airport akamuona Mr na huyo mwanamke wamesafiri wote. Yani wakawa na mahusiano ya wazi kabisa hawaogopi chochote. Alivyorudi nikamuuliza ulienda Dubai na nani akasema Girlfriend wangu mwanamke msafi nimpendae. Nikaanza kuchanganyikiwa sielewi cha kufanya.
Kiukweli Pastor Anni Kaleb namfahamu muda mrefu tu tangu wanasali kanisa la ilala, kuna siku nilimuona humu Facebook akiingia live anafundisha nikamtumia message Dada yangu nakufa huku naomba nikuone.
Nikapanga kuonana na Pastor, nikamuhadithia kila kitu nikamwambia nataka niondoke niachane na Mume wangu maana hali imekuwa mbaya kifupi hakuna ndoa.
Akaniomba sana akasema umefanya sana kwa akili zako hembu mpe Mungu nafasi nae afanye, akaniambia muachie Mungu na tuingie kwenye maombi tuombe msaada wa Mungu. Nikacheka nikasema huyu Pastor anasema nini naombaje Mimi, namuombeaje jitu kama lile?
Pastor akasema unaweza niamini na nisikilize, tuombe. Nikamkubalia.
Akaniambia sasa tutaanza maombi ya kimkakati akasema tunayaita emergency prayers, haya maombi ya kumuomba Mungu afanye kwa haraka. Basi tukaanza kufunga, tulipanga tufunge mwezi mzima na wiki ya kwanza aliniomba niombe rehema kwa Mungu, nimuombee Mume wangu rehema kwa Mungu, nitangaze msamaha kwaajili yake. Akasema huwezi muombea mtu uliye na kinyongo nae, akasema omba msamaha toa uchungu wote, hakikisha umesamehe kila kitu ndio tuanze maombi yetu.
Kweli ile wiki niliomba Mungu msamaha nilitubu juu yangu na mume wangu, nikawa naamka usiku namuombe mume wangu. Nilimaliza wiki nikaanza kuona nguvu na amani. Tukaingia wiki ya pili Pastor aliniongoza maombi, wiki ya tatu, lakini hali kwa Mr haikubadilika kabisa kabisa ikazidi kuwa mbaya. Nikamwambia Pastor mbona tunaomba na hakuna mabadiliko tuache tu maombi.
Nakumbuka ilikuwa jumanne wiki ya mwisho ya maombi sikufunga na Pastor Anni akinipigia sipokei. Nikaamka asubuhi nakuta Mr kamtumia message huyo mwanamke kuwa jumamosi waende vacation warudi jumapili jioni ajiandae. Niliumia sana. Nikampigia Pastor Anni nikamwambia mbona nadharilika hivi Pastor, Pastor akasema vita vyetu si vya mwili ni vya roho, usimuulize Mr chochote tuendelee kuomba.
Sikumwambia Pastor kama nimeacha kufungua, nilikuwa nishakata tamaa. Pastor atanipigia jioni anaomba naitikia tu ila nakula kama kawaida.
Ilifika ijumaa Mr akasema niandalie nguo zangu hizi zinyooshe kesho nasafiri kidogo naenda kupumzika mahali nitarudi jumapili. Alivyoondoka nikampigia Pastor nikamwambia akasema sawa muache aende akasema usiku wakati unapanga nguo nipigie tuombe.
Nia yangu nilitaka kitokee chochote Mr ahairishe safari lakini ilishindikana.
Nilikuwa naumia sana maana safari iliiva.
ITAENDELEA PART 5 MWISHOOO
PART 5 MWISHOOO
TABIA ZA MUME WANGU ZILINICHOSHA
Ikafika usiku Mr alirudi akaingia ndani akalala alikuwa amekunywa, sikumsemeha. Nikampigia Pastor Anni wakati wote wamelala Pastor akaniambia chukua shati lake analovaa kesho, suriali, vest, boxer mpaka sock zibebe weka mabegani, basi nikaweka akawa anaomba na Mimi naomba huku nguo ziko mabegani nazunguka nazo. Tuliomba kama saa nzima, alikuwa anasema tu Mungu jitikuze, Mungu jitwalie utukufu, Mungu jidhihirishe. Basi tukaomba tukamaliza akasema akiondoka asubuhi nipigie tuombe tena.
Sio siri sikulala moyo unauma, asubuhi Mr kaamka nashindwa kumzuia maana ni mkali kama mbogo. Nikaandaa zile nguo akavaa akaondoka.
Ile anatoka nikampigia Pastor Anni nikamwambia huku nalia Pastor ameenda Pastor, akaniambia sawa haina neno. Akaniambia piga magoti kitandani kwako nikaweka simu loud speaker akaanza kuomba, Mimi huku ninalia, nililia sana huku Pastor anaomba. Pastor aliomba muda akaniambia muamini Mungu usiache kuomba Mungu atafanya ila hatujui atafanyafanyaje lakini najua atafanya.
Basi tukamaliza maombi na Pastor akakata simu, kama kawaida yangu sijafunga nikaenda zangu nikaanga mayai na chai nikalaaa, na soda nikashushia. Nikawa naangalia TV kuna tamthilia za vichekesho nikawa nacheka na wanangu. Ikapita kama masaa manne tangu Mr aondoke ghafla nasikia honi ya gari inapigwa kwa nguvu sana, nikashangaa ni honi ya Mr imekuwaje au kasahau kitu, nikasema au sijanyoosha vizuri nguo zake anakuja kunipiga maana kazoea kitu kidogo ananipiga. Nikawa na hofu kweli.
Basi nikatoka naenda kufungua geti Mr kaingiza gari ndani anatapika kashuka pale kwenye gari kakaa chini anatapika, yani katapika kama robo saa nikawa sielewi nikamuita wifi yangu alikuwa ndani akasema ni nini alitapika mpaka akawa anaishiwa nguvu. Ikabidi niite watu wengine watusaidie nikakodi Bajaj mpaka hospital. Kufika hospital hali ni mbaya anatapika mpaka anakakamaa.
Dr akauliza nini shida nikasema sijui na yeye hasemi kabisa. Wakamuingiza wodini wakamuwekea drip na dawa za kuzuia kutapika. Baadae nikachukua simu yake nikasema niendenayo nyumbani nikaicharge ile natoka nafungua nakutana na message za matusi yule mwanamke anamtukana Mr na anamlalamikia kumshutumu kuwa ananuka kaoza. Nikagundua Mr alienda kule akakutana na harufu kali kwa huyo mwanamke ya kuoza ndio akaanza kutapika.
Basi nikarudi nyumbani nikampigia Pastor Anni kumuhadithia Pastor akasema tumshukuru Mungu ametenda. Tukawa tunacheka imekuwaje hatuelewi.
Nikarudi hospital Mr bado hali mbaya anatapika, nikamletea nguo akabadilisha lakini wapi bado, alikaa hospital siku tatu. Kila anachokula anatapika. Baadae hali ikakaa sawa akasema aisee kuna watu wananuka mke wangu, kuna wanawake wameoza daaah ni balaa, akiongea hivyo anatapika.
Basi tukarudi nyumbani, kutapika kulipungua ila alikuwa anatapika kidogo kidogo, siku moja akajaribu kunywa pombe weeeh alitapika tukarudi tena hospital. Doctor akashauri aache pombe. Jamani mambo yalitokea kama ndoto.
Ugonjwa hauonekani na haieleweki ila ndio hivyo mtu anaumwa.
Ninanyoongea sasa Mume wangu hanywi pombe tenaa, haendi bar akitoka kazini yuko nyumbani maana akikaa kwenye mikusanyiko anatapika. Yani sijui nini kimempata ila ndio hivyo, siku moja akasema mke wangu unanukia kama malaika nakupenda, yani sitaki mtu anisogelee natapika.
Basi mpaka leo mume wangu yupo, anarudi nyumbani saa kumi na moja, anaogesha watoto atawalisha Mimi nikifunga duka namkuta nyumbani. Yani akisikia harufu mbaya ya pombe au mtu anatapika.
Mwisho.