Naomba niseme kidogo. Nimekuwa mfuatiliaji wa karibu wa JF kwa karibia mwaka. Nimegundua kwamba jamboforums kuna rangi nyingi sana when it comes to politics in Tanzania. Muhimu zaidi, wengi wa Jamboforums wanaonyesha bado wana imani na chama chao cha mapinduzi kwani wakati wa chaguzi hizi huwa wanakuwa wana base hoja zao zaidi on nini kitaimarisha au kuvunja chama. Ukweli huu huwa unazidi kujiidhirsha nyakati hizi za chaguzi ambapo wengi huwa wanakuwa na preferences za on nani awe au asiwe kiongozi ndani cha chama cha mapinduzi na kusahau kabisa how hizi development can or should shape upinzani. Mbali zaidi, kama kawaida, siasa za kusengenyana na kuanikana na vilevile kutafutiana kashfa humu jamboforums huwa hazikawii kujitokeza baada ya chaguzi. Hakika nyakazi za chaguzi za ccm ni muda mzuri sana wa kuchambua msimamo wa wana jamboforums wengi sana. wengi hawapo consisent na misimamo yao ya kisiasa. Hili ni bayana kama ukitumia muda wako kidogo kuangalia historia ya postings za watu kadhaa humu over time. In other words, wengi humu hawana dira. tusubiri matokeo ya NEC yapite na tutaona haya kwa mara nyingine tena.
..raia,sijui kama we ni mwema kweli,ila,karibu!
..hili baraza ni pana sana na lina kila aina ya watu,wenye kila aina ya msimamo na wengine hawana kabisaa!
..nadhani kitu cha muhimu si kuwa katika upande gani wa kisiasa,bali,ni uwezo wa kutoa mawazo ya nini kifanyike ili nchi yetu iweze songa mbele vizuri na kwa manufaa ya wengi!
..kuna kipindi issues zilikuwa zinakatwa hapa mpaka ilitia msisimko!hali si hivyo kwasasa!kwani majungu yamezidi!focus imepotea...unajikuta unaongea au kuchangia pumba!
..kama nilivyosema awali,hili ni baraza na baraza ni watu!sasa,kwenye wengi kuna mengi na ndio haya!ila,naamini ipo siku tutarudi kwenye kukata issues baada ya huu upepo mbaya wenye pepo baya utakapopita!
..wapo watu kama fd,dua,mjj,mkandala,philemon mikael,kithuku,jokakuu,masatu,invicible,kada,mwafrika wa kike,samvulachole,mtupori,fmes,drwho,mtumwitu,na wengine ambao nadhani wamebadilisha majina. hawa walikuwa wanakata ishu si mchezo...ila siku hizi....aagh!tuache huu upepo upite!
..kuwa na subra,hii ndio tanzania!