Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797

Wakili wa upande wa utetezi Moses Mahuna akieleza kuhusu Sabaya na wenzake
kushinda rufaa yao na kuachiliwa huru katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.




Sabaya na wenzake watatu wamebakiza ngwe moja ya hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mahakama Kuu ya kumwachia huru muda huu. Warufani wengine katika kesi hiyo ni Silvester Nyegu na Daniel Mbura, waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Oktoba 15, mwaka 2021, Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo, alimtia hatiani Ole Sabaya na wenzake kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.




Ole Sabaya wakati akifikishwa Mahakamani kusikiliza rufaa yake Mei, 2022


Pia, soma=> Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha
 
Serikali kwa mara nyingine ijitathmiini katika uwezo wa Idara na Taasisi zake kutayarisha kesi na mashahidi kwani zimefeli hivyo kushindwa ku-i-move Mahakama Kuu kuwa kulikuwa na kesi ya kusikilizwa kwa kutumia mizania ya kisheria.


Je tatizo ni kukosekana wanasheria wa serikali walioiva ? Je mfumo haki jinai (criminal justice system) yaani Polisi, TAKUKURU, DPP na Mahakama za chini zinakosa rasilimali watu wabobevu wa kuchunguza, kuandaa na kusikiliza tuhuma / kesi toka mwanzo wa mchakato mzima wa kutoa haki Au kesi hii ilikuwa kuna shindikizo?



06 May 2022
Arusha, Tanzania
Hukumu ya Jaji Ezedekia Kisanya wa Mahakama Kuu ya Tanzania :

Rufaa hiyo ya jinai namba 129/2021
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemuachia huru aliyekuwa DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamekata rufaa ya kupinga kuhukumiwa miaka 30 kwenda jela kila mmoja kwa sababu mbalimbali kwakuwa Mrufani namba mbili Silvester Nyegu na namba tatu Daniel Mbura hawakupewa haki ya kumhoji Shahidi namba mbili wa Jamhuri na kutokufanya hivyo kunawanyima haki yao msingi.

Jaji Ezedekia Kisanya amesema kulikuwa na mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa kesi hiyo ikiwemo kutofautiana kwa mashahidi na kuufanya ushahidi kuwa batili.

Jaji amesema Lengai Ole Sabaya na wenziwe, watakuwa huru endapo watakuwa hawana kesi nyingine kwenye Mahakama yoyote.
"Kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji ...

Kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha namba 27 /2021 inayomkabili Lengai Ole Sabaya na wenzake watano nayo imeahirishwa hadi July 16,2021 kutokana na

Kesi nyingine ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha namba 27 /2021 kutolewa hukumu tarehe 31 May 2022

Kumbukumbu zinaonesha Lengai Ole Sabaya na wenzie watano bado wanakabiliwa na kesi ya tuhuma ya uhujumu uchumi. Hivyo ataendelea kuwa mahabusu na siyo mfungwa baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutengua hukumu ya kesi ya unyanganyi kwa kutumia silaha ambapo mahakama ya Hakimu Mkazi ilimuhukumu miaka 30 lakini imetenguliwa leo na kumbatilisha kuwa mahabusu anayesubiri hukumu ya kesi iliyobaki mahakamani ya Uhujumu Uchumi.
 
Back
Top Bottom