Sabaya na wenzake washinda Rufaa dhidi ya Serikali kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali Rufaa iliyokatwa na Upande wa Jamhuri, ikipinga uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, kumuachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela.

Hukumu hiyo iliyosomwa na Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Abesiza Kalegeya, leo Ijumaa Novemba 17, 2023, imesema hakukuwepo na tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha, badala yake Mjibu rufani wa kwanza Lengai Ole Sabaya, alikuwa katika majukumu yake halali ya kufuatilia Makosa ya uhujumu uchumi kama ilivyoelezwa na Mashahidi wenyewe wa upande wa mashtaka.

Mahakama hiyo ya rufaa iliyokaa chini ya Mwenyekiti wake Jaji Jacob Mwambegele imeeleza zaidi kwamba, Mahakama ya Hakimu Mkazi iliyomtia hatiani Sabaya na wenzake, ilikosea kutochambua ushahidi unaoonyesha wazi kwamba, haiijawahi kutokea Jambazi akamate Mtuhumiwa, amnunulie Ndizi na baadae kumpeleka Polisi kama Mashahidi wenyewe walivyoelezwa kutendewa na Sabaya.

Majaji wameeleza hiyo ni aina ya kwanza ya unyang’anganyi wa Majambazi kuepeleka waliowaibia Mahakamani, na kuhitimisha kwamba Wajibu rufaa waliachiwa kihalali na Mahakama Kuu.

Mkurugenzi wa Mashtaka alikata Rufaa kupinga uamuzi wa Jaji E. Kisanya, kuwaachilia huru Lengai Ole Sabaya, Sylivester Nyegu na Daniel Mbura, waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha.
 
Ukiona wanaopandishwa kuwa Justices of Appeal unaona kabisa kuwa kuna shida sana huko CoA! Ni hao judges kutoka High court ambako ni incompetent judges in thinking capacity, hao yanapanda kwenda kwenye apex court! Soma hata kiingereza chao, shida tupu! Linganisha hukumu za bold judges kama Mwalusanya na za hawa UPE, utaona clear intellect difference, a very big one
 
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai na kipenzi cha rais wa awamu ya tano Hayati Magufuli ameshinda rufaa yake ya pili iliyokuwa imefunguliwa na DPP akipinga Sabaya kuachiwa huru kutoka kwenye kifungo cha miaka 30 jela alichotuhumiwa kuvamia na kuibia watu.

Sasa Sabaya yuko huru kugombea na kufanya siasa popote kama akitaka kufanya hivyo kwani mahakama imemsafisha na kumfanya kuwa raia mwema asiye na doa lolote.
Hivyo manabii feki akina Lema na Chadema kwa ujumla watajinyonga kwa wivu kwani walikuwa msitari wa mbele kumsingizia na kumchafua kijana huyu mchapakazi.

 
Back
Top Bottom