Shetani kashindwa kwa mara nyingine kesi ya Sabaya

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,396
3,901
NA HAYA NDIO MAAMUZI YA MAHAKAMA YA RUFAA KATIKA KESI YA LENGAI OLE SABAYA.

Well,Kwanza Nitangulize Kusema kwamba Mahakama hii ya Rufaa ndio Mahakama ya Mwisho Kabisa katika Ngazi ya Maamuzi ya Kimahakama Nchini Tanzania, Shauri hili baada ya hapa limefungwa Rasmi....tuendelee..👇

Hili Ni Shauri la Rufaa namba 231 ya mwaka 2022 iliyokatwa na mwendesha mashtaka wa serikali (DPP) kupinga uamuzi wa awali wa hukumu ya rufaa namba 129 ya mwaka 2021 iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mbele ya Jaji Sedekia Kisanya iliyompa ushindi Ole Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kufuatia kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021 iliyohusisha wizi na makundi ya unyang’ayi wa kutumia silaha.

MAAMUZI YA MAHAKAMA YA RUFAA:

1. Mahakama imejiridhisha kuwa Watu hawa Walikuwa katika Majukumu Yao Halali kwa mujibu wa Sheria kufuatilia Wakwepa Kodi na Wahujumu wa Uchumi, na Hakuna Ubishi Mtu huyo Sabaya ana Historia hiyo ya Ufuatiliaji na utekelezaji katika Majukumu yake, Hivyo walienda kutekeleza Majukumu ya Kawaida

2. Mahakama ilielezwa na Mashahidi wa Upande wa Mashtaka kuwa Watu hao Washtakiwa Walipofika Dukani Walindoka na EFD Mashine 2 na Nyaraka za Kikodi Kama Risiti, huu Ni Uthibitisho Mwingine kuwa Watu hao walikuwa katika Kutekeleza Majukumu Yao ya Kikodi na sio Unyan'ganyi au Ujambazi.

3. Kwa Uzoefu wa Mahakama ya Rufaa hapa Tanzania hili Ni Tukio la Kwanza katika Historia ya Nchi hii ambalo wanaoitwa "Majambazi" wanawachukua Watu Waliowaibia na kuwapora na kuwapeleka Polisi"

4 .Shahidi nambari 4 wa upande wa Mashtaka kwa jina la Saad Ajirini alikuwa kwenye Mfungo na anasema alikuwa Ametoka Nje ya Duka kwa kuwa Muda wa kufuturu ulikuwa umefika na anasema Mshtakiwa Sabaya alimnunulia Ndizi pale nje kwa ajili ya kufuturu...Sasa katika Hili Mahakama hii ya Rufaa kwa Uzoefu wake imeshangazwa Sana Kuona aitwaye Jambazi anamfuturisha Mtu aliyempora.

5.Shahidi nambari 6 kwa jina la Bakari Msangi aliieleza Mwenyewe Mahakama kwamba Huko nyuma aligombea Uenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM(UVCCM) akishindana na Sabaya na Sabaya akamshinda, Hivyo Mahakama ya Rufaa imeona kuwa Ushahidi wa Bakari Msangi Ni Fitina za Kisiasa kwa Mshindani wake aliyemshinda Katika Uchaguzi na isitoshe Shahidi Huyo alienda katika eneo la Tukio ambalo duka sio la kwake na Sabaya ndipo alipomwambia " Una kiherehere katika kufuatilia Mambo yangu"

6. Pia Mahakama hii imeshangazwa kwamba Shauri la Msingi ambalo lilipelekwa Polisi lilikuwa Kesi ya Uhujumu Uchumi ambayo ndio walishtakiwa nayo lakini Ghafla ikabadilishwa kuwa Kesi ya Ujambazi na Unyang'anyi wa kutumia Silaha.

7. Hivyo Mahakama ya Rufaa imegundua kuwa kulikuwa na Uongo Mwingi katika Maelezo ya Mashahidi na Hivyo Mahakama hii ya Rufaa
Inakubaliana na maamuzi ya Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na rasmi inamuachia huru Lengai ole Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura .

#Mytake :Ikumbukwe Mh Rais alimsimamisha Sabaya kupisha Uchunguzi wa Tuhuma zake, lakini ajabu badala ya Kufanya Uchunguzi watu wakaenda nje ya Maamuzi ya Msingi ya Mh Rais yaani "Kupisha Uchunguzi" Wao wakaenda kumfungulia Kesi Sabaya na akiwa bado ni Mkuu wa Wilaya ya Hai aliyesimamishwa Kupisha "Uchunguzi" na sio "Aliyetenguliwa"

Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan,hii ndio Hali halisi ilivyo katika Siasa zetu na hasa ndani na nje ya Chama, ipo Vita kubwa Sana Kati ya "Watu wababaishaji" Dhidi ya "watu Makini" wenye Nia ya Dhati ya kukusaidia Mh Rais na Taifa hili, na kadiri vile ambavyo Mh Rais unaendelea Kung'amua Uwepo wa Watu Makini na kuwatumia na kuwaamini katika Kutekeleza majukumu unayowapa na ndivyo Asilimia ya Uwepo Wa Wababaishaji inavyozidi kupungua.

Kwani Watu walio Wababaishaji na wasio na Nia njema kwako na Taifa letu wamekuwa siku zote wakijaribu kuwa Vizingiti Kati yako na Watu Makini. Sabaya, Makonda na Wengine wengi ni Wahanga katika hili, kwa sababu Hawa Moja ya Hazina ya Vijana Makini na Wazalendo,ni Moja ya Viongozi imara wanaoweza kukusaidia Mh Rais katika Kutekeleza Malengo na Vision Njema katika Nchi hii, nimalizie kwa Kusema kwamba Mh Rais endelea kuwatumia kwa Maslahi Mapana ya Taifa na zaidi ya yote Uwalinde kwa Gharama yoyote.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

🇹🇿✊
 
Back
Top Bottom