Kisutu: Mahakama yamhukumu Mfanyabiashara Herbinder Seth Kulipa fidia ya Tsh. 26.9 bilioni

Miaka 6 waliyokaa ndani wangezalisha zaidi ya hizo,huku wakichangia uchumi,kutoa ajira na kodi.
 
DPP Sylvester Mwakitalu leo amemuachia huru mfanyabiashara Herbinder Seth baada ya kukiri makosa na kulipa faini.

Mzee Ruge bado amekomaa, tusubiri tuone nini kinaendelea.

Source: Darmpya Blog
Jela si Kuzuri Mkuu hata Yeye 'atakaza' ila 'ataachia' Siku si nyingi. Anajaribu tu Kujitutumua na Kujidhira ila najua Familia pamoja na Mwandamizi Mmoja ( sasa ni Mstaafu ) Serikali ' watampoza ' kwa Ushauri na Kuridhia hatimaye nae Kuachiwa Huru hivi kwa Dhamana kama ' Swahiba ' wake huyu.
 
Ina maana huyu DPP mpya nae anaendelea na tabia ya kujigeuza ndie mahakama?

Kama hawa watu wanakiri wana hatia ni kitu gani kinachoishinda jamhuri kupeleka kesi mahakamani ushahidi utolewe ili adhabu kama itakuwepo wapewe iwe kifungo au kulipa faini?

Hii tabia ya kumalizana kwa DPP lilikuwa kosa la Magufuli, nashangaa na awamu hii nayo wanaendelea nalo, mahakama ziachwe ziamue kesi kisheria, DPP abaki na kazi yake ya awali asiingilie majukumu ya mahakama.
Mkuu umeisoma vizuri hiyo Habari kweli? Mahakama imemhukumu kulipa fidia bilioni 26 na kifungo cha nje cha mwaka mmoja bila kufanya jinai yoyote
 

Leo 16/06/2021 12:45

Dar es Salaam.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth kulipa fidia ya Sh26.9 bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Sh309 bilioni kwa njia ya udanganyifu.

Pia, mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja akitakiwa kutokujihusisha makosa yoyote ya jinai.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amefanikiwa kulipa Sh200 milioni benki na kiasi kinachobakia anatakiwa kukilipa ndani ya mwaka mmoja kuanzia siku ilipotolewa hukumu.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano Juni 16, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa makubaliano ya kuimaliza kesi hiyo.

"Ni wazi kama wakili Marandu alivyotueleza mahakama kuwa Seth ni mkosaji wa mara ya kwanza na ni wazi umekubali mwenyewe kuingia katika makubaliano na DPP (mkurugenzi wa mashtaka nchini), ni wazi umekubali mwenyewe kulipa Sh26.9 bilioni, hivyo mahakama inakuhukumu kifungo cha nje cha mwaka moja, kutokujihusisha na makosa yoyote ya jinai" amesema Shaidi.

Awali, mawakili wawili wakuu wa Serikali, Marterus Marandu, Renartus Mkude na wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon na Faraja Ngukah, walidai kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa mashtaka yake baada ya kuingia makubaliano na DPP.

=====

15/06/2021
Serikali yaafiki maombi majadiliano na Seth

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mtendaji wa PAP, Harbinder Seth, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamepitia barua iliyoandikwa na mshtakiwa huyo na kufikia makubaliano kwa kile alichokiomba. Seth aliandika barua hiyo Juni 10, kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), akiomba kukiri mashtaka yake na kupunguziwa adhabu.

Barua hiyo ilijadiliwa kwa siku mbili na upande wa mashtaka na ule wa utetezi na kisha kutolewa mrejesho.

Wakili wa Serikali Mkuu, Marterus Marandu akisaidiana na Ladslaus Komanya jana alitoa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili Marandu alitoa maelezo hayo wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya upande wa mashtaka kuwasilisha mrejesho wa kile walichozungumza kati yao na Seth kwa ajili ya kuimaliza kesi hiyo.

“Kesi imekuja kwa ajili ya kutoa mrejesho wa barua iliyoandikwa na mshtakiwa huyu (Seth), niseme barua tumeshazipitia kwa pamoja na tumefikia mahali pa kukubaliana kuhusu kile ambacho mshtakiwa alikuwa anakiomba na baada ya hapo, tumekubaliana kuendelea na shauri hili,” alidai wakili Marandu na kuongeza:

“Kwa muktadha huo, upande wa utetezi kama hawatakuwa na pingamizi, naomba shauri hili lije mahakamani hapa kesho ( Juni 16) kwa ajili ya usikilizwaji,” alidai Marandu.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Seth, Melchisedeck Lutema alikubaliana na maelezo ya upande wa mashtaka na kueleza kuwa huo ndio ukweli na ndio msimamo wa pande zote mbili za majadiliano waliyofanya.

Hakimu Shaidi baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Juni 16 itakapoitwa kwa ajili ya usikilizwaji au majadiliano ya kuimaliza kesi.

Hata hivyo, jana Seth alikuwepo mahakamani peke yake, wakati upande wa mashtaka walipowasilisha mrejesho huo.

Itakumbukwa Juni 10, Mahakama hiyo ilikubali upande wa mashtaka kufanya mazungumzo na mshtakiwa huyo ya kuimaliza kesi hiyo. Mahakama hiyo ilirihusu majadiliano hayo baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi mahakamani hapo la kutaka kufanya majadiliano na Seth na kisha kutoa mrejesho wa kile walichozungumza kwa ajili ya kuimaliza kesi.

Mbali na Seth, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ambao hawajaandika barua ya kukiri mashtaka yao kwa DPP ni aliyekuwa Mwanasheria wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege na Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya IPTL, James Rugemalira.

Katika kesi ya msingi, Seth na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 12 likiwemo la kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Niulize tu kwa ukihiyo wangu sijui hukumu/kesi za makosa ya uhujumu uchumi zinaendeshwa kwenye mahakama hizi za kawaida na sio mahakama kuu? halafu hii faini mbona kama Ze comedy vile, yaani ni sawa na huku Uswazi nifanye kosa la faini ya shilingi 300,000 na ushee halafu ukipelekwa kwenye mahakama za kata unaambiwa bwashee tunakuachia kwa sasa lipa kwanza faini ya shilingi 2,000/= hizo zingine utamalizia baadae. Kama sio maigizo ni nini basi ....
 
Singa singa intown....sasa ile mitambo pale pameota nyasi....yale ma HOF engines yatahitaji mpunga ww kutosha kuyaamsha na kuyawasha au kuyauza ... Kuna hatari ya kesi inakuja kati ya GOVT na SETH + RUGE na hichi ndicho yule jamaa alikikwepa akaamua kuwahifadhi akiamini kwa mateso na kukosa uhuru natural death itasema nao...
Japo si mtaalam wa sheria huyo baniani kishakiri kosa,anaanzaje sasa kushtaki kwa kitu ambacho alikubali aliiba!
 
Am sure alijaribu kipindi cha Magufuli pia kujinunulia uhuru.

Ila hii approach itumaanishie nini maskini? Kwamba inawezekana tukafungwa kisa hatuna pesa? Mtu akikiri makosa anatakiwa atumikie adhabu iliyopo kisheria au alipe pesa atoke?
Ndugu yangu miaka 4yrs Jela tena jela ya Tanzania ni sawa sawa na miaka 40yrs especially kwa MTU kama yule Seth. Hata rudia tena ujanja ujanja itakuwa kapata darasa la kutosha.
 
Na kalipa 200m baadae utasikia katorokea Canada, tunarudi enzi za awamu ya Kilimo kwanza.
Bila kusahau Big Results Now (BRN) na Tanzania Beyond Tomorrow (TBT),
Tulipoambiwa flat screen zipo Chamwino na Magogoni ila remote control ipo Chalinze hatukuamini
 
Samia = Magufuli

Mtaelewa tu nyie vivutio vya utalii
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth kulipa fidia ya Sh26.9 bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Sh309 bilioni kwa njia ya udanganyifu.
YAANI KAPIGA BIL 309 FAINI SH BIL29, HIVI HAWA WANASHERIA WAKIITWA MAJINA YA OVYO WATABISHA,
 
Naunga mkono hoja. Mtu akiiba kwa kutumia udhaifu wa sheria ni ngumu kumshinda, labda nguvu itumike.

Sidhani kama lilikuwa dili la watu wawili tu la kina Seth na Ruge. Hilo dili lilienda kisheria kabisa ndo mana mwendazake aliamua kutumia nguvu ili watoe mpunga. Jamhuri ilishindwa kukamilisha ushahidi.

Sasa itategemea uungwana wa hao mabwana, kwani wanaweza kuja kuibua kesi huko mbeleni, ukizingatia kwa sasa tunaenda kidemokrasia angalau.
Ushahidi wote wa kinyaraka unaipa haki serikali na ni wazi pesa zimeibiwa na Serikali imepoteza.
Ila maelekezo ya kisheria ya mwanasheria mkuu wa Serikali na hukumu ya Jaji wa mahakama kuu inawabeba kina Harbinger Singh na Ruge mwenzake.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom