Baba kizimbani kwa mashtaka ya kumnajisi mwanawe wa kumzaa mwenye miaka 14

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
MKAZI wa Mtaa wa Nyabubele Kata ya Kasamwa Kukailwa (40), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita kwa mashtaka ya kunajisi mwanawe - msichana mwenye miaka 14.

Alipandishwa kizimbani jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Johari Ki uwile na aliposomewa mashtaka, alikana kuhusika na kosa hilo na yuko mahabusu katika Gereza la Wilaya ya Geita bada ya kukosa wadhamini.

Upande wa Mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Venance Mkonongo, ulidai mahakamani huko upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mashtakiwa maelezo ya awali.

Hakimu Mkazi Mwandamizi Kijuwile alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hivo hadi Agosti 30 mwaka huu kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa huyo maelezo ya awali. Hakimu huyo pia alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa huyo awe na wadhamini wawili wenye barua ya utambulisho kutoka kwa Ofisa Mtendaii wa Kata na mali isiyohamishika venye thamani ya Shilingi milioni tano.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Venance Mkonongo, alidai mahakamani huko kuwa katika tarehe tofauti Februari na Machi mwaka huu, katika mtaa wa Nyakubele, Kata ya Kasamwa, mkoani Geita, mshtakiwa alimnajisi mwanawe wa kuzaa (kulala na maharimu) msichana mwenye umri wa
miaka 14.​
 
Back
Top Bottom