Waliotorosha madini ya Bilioni 300 wahukumiwa kulipa fidia ya milioni 923.8

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imewaamuru wafanyabiashara wanane waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, kuilipa Serikali fidia ya Sh923.8 milioni huku ikiamuru kutaifishwa pia kwa mali zao na Sh103.9 milioni.

Hii ni baada ya mahakama kuwatia hatiani kwa makosa matatu ya kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara, baada ya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kukiri makosa yao.

Hukumu hiyo imetolewa jana Novemba 15, 2023 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Johari Kijuwile baada ya kuwatia hatiani kwa makosa hayo ambapo mbali na kuwaamuru kuilipa serikali fidia, pia wametakiwa kutotenda kosa lolote la jinai ndani ya miezi 12.

Makosa hayo walidaiwa kuyatenda katika siku tofauti kati ya Februari Mosi, 2018 na Juni Mosi 2023 kwa kufanya biashara ya kuuza dhahabu kilo 2,348 zenye thamani ya Sh345.9 bilioni bila kuwa na leseni.
 
Kuna mjane kala mvua 22 kwa kukutwa na kilo 12 za nyama ya swala huko iringa.
 
Halafu unakuta mama wa watu ana hukumiwa maisha kwa vipande kadhaa vya nyama.

Nyie watu wa sheria Kuna hukumu baada ya hapa.
 
Back
Top Bottom