Kisutu: Mahakama yamhukumu Mfanyabiashara Herbinder Seth Kulipa fidia ya Tsh. 26.9 bilioni

Isije ikawa kaishia kulipa tu hizo milioni sijui mia 2,mtatupa mresho 2025 maana huo tu ndo muda muafaka nguvu yetu ilipo.
Huyu jamaa aliachwa tu na JK.mpaka Mwendazake alipojitoa mhanga.
 
Jeshi la polisi lirejeshe mpunga aliowapa haraka

1544778_IPTL_MBWENI_PIX_2.jpg
 
Ina maana huyu DPP mpya nae anaendelea na tabia ya kujigeuza ndie mahakama?

Kama hawa watu wanakiri wana hatia ni kitu gani kinachoishinda jamhuri kupeleka kesi mahakamani ushahidi utolewe ili adhabu kama itakuwepo wapewe iwe kifungo au kulipa faini?

Hii tabia ya kumalizana kwa DPP lilikuwa kosa la Magufuli, nashangaa na awamu hii nayo wanaendelea nalo, mahakama ziachwe ziamue kesi kisheria, DPP abaki na kazi yake ya awali asiingilie majukumu ya mahakama.
kwani kazi ya dpp ni nini?hilo sio miongoni mwa majukumu ya dpp kisheria?
 
Mkuu mbona sioni uzi wako ukijadili bajeti? Sasa hivi naona ukiamzishwa uzi wowote unarukia ili uone utamtakatishaje dhalimu.
Mkuu tuko busy na MONDI kwanza hasa ukizingatia dhalimu wako anakomolewa
 
Ina maana huyu DPP mpya nae anaendelea na tabia ya kujigeuza ndie mahakama?

Kama hawa watu wanakiri wana hatia ni kitu gani kinachoishinda jamhuri kupeleka kesi mahakamani ushahidi utolewe ili adhabu kama itakuwepo wapewe iwe kifungo au kulipa faini?

Hii tabia ya kumalizana kwa DPP lilikuwa kosa la Magufuli, nashangaa na awamu hii nayo wanaendelea nalo, mahakama ziachwe ziamue kesi kisheria, DPP abaki na kazi yake ya awali asiingilie majukumu ya mahakama.
Kabla hujalaumu kwanza jiridhishe vya kutosha kwa kupitia sheria zilizopo. Soma sheria kuhusu plea bargain utaona inaruhusu hicho kilichofanyika.
 
Mzee wa Heineken mbishi bado naona ngoja tusubiri kidogo tuone

Bila shaka atakuwa anajiamini siyo bure.

Kwa muda wote alokaa mahabusu halafu na vipensheni vyake na wajukuu zake vikombwe itakuwa na maana gani?!

Bora angelipa mwanzoni kukwepa jera muda wote angeutumia kwa uzalishaji au biashara zake.

Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi.
 
Leo 16/06/2021 12:45

Dar es Salaam.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth kulipa fidia ya Sh26.9 bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Sh309 bilioni kwa njia ya udanganyifu.

Pia, mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja akitakiwa kutokujihusisha makosa yoyote ya jinai.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amefanikiwa kulipa Sh200 milioni benki na kiasi kinachobakia anatakiwa kukilipa ndani ya mwaka mmoja kuanzia siku ilipotolewa hukumu.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano Juni 16, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa makubaliano ya kuimaliza kesi hiyo.

"Ni wazi kama wakili Marandu alivyotueleza mahakama kuwa Seth ni mkosaji wa mara ya kwanza na ni wazi umekubali mwenyewe kuingia katika makubaliano na DPP (mkurugenzi wa mashtaka nchini), ni wazi umekubali mwenyewe kulipa Sh26.9 bilioni, hivyo mahakama inakuhukumu kifungo cha nje cha mwaka moja, kutokujihusisha na makosa yoyote ya jinai" amesema Shaidi.

Awali, mawakili wawili wakuu wa Serikali, Marterus Marandu, Renartus Mkude na wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon na Faraja Ngukah, walidai kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa mashtaka yake baada ya kuingia makubaliano na DPP.

=====

15/06/2021
Serikali yaafiki maombi majadiliano na Seth

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mtendaji wa PAP, Harbinder Seth, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamepitia barua iliyoandikwa na mshtakiwa huyo na kufikia makubaliano kwa kile alichokiomba. Seth aliandika barua hiyo Juni 10, kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), akiomba kukiri mashtaka yake na kupunguziwa adhabu.

Barua hiyo ilijadiliwa kwa siku mbili na upande wa mashtaka na ule wa utetezi na kisha kutolewa mrejesho.

Wakili wa Serikali Mkuu, Marterus Marandu akisaidiana na Ladslaus Komanya jana alitoa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili Marandu alitoa maelezo hayo wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya upande wa mashtaka kuwasilisha mrejesho wa kile walichozungumza kati yao na Seth kwa ajili ya kuimaliza kesi hiyo.

“Kesi imekuja kwa ajili ya kutoa mrejesho wa barua iliyoandikwa na mshtakiwa huyu (Seth), niseme barua tumeshazipitia kwa pamoja na tumefikia mahali pa kukubaliana kuhusu kile ambacho mshtakiwa alikuwa anakiomba na baada ya hapo, tumekubaliana kuendelea na shauri hili,” alidai wakili Marandu na kuongeza:

“Kwa muktadha huo, upande wa utetezi kama hawatakuwa na pingamizi, naomba shauri hili lije mahakamani hapa kesho ( Juni 16) kwa ajili ya usikilizwaji,” alidai Marandu.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Seth, Melchisedeck Lutema alikubaliana na maelezo ya upande wa mashtaka na kueleza kuwa huo ndio ukweli na ndio msimamo wa pande zote mbili za majadiliano waliyofanya.

Hakimu Shaidi baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Juni 16 itakapoitwa kwa ajili ya usikilizwaji au majadiliano ya kuimaliza kesi.

Hata hivyo, jana Seth alikuwepo mahakamani peke yake, wakati upande wa mashtaka walipowasilisha mrejesho huo.

Itakumbukwa Juni 10, Mahakama hiyo ilikubali upande wa mashtaka kufanya mazungumzo na mshtakiwa huyo ya kuimaliza kesi hiyo. Mahakama hiyo ilirihusu majadiliano hayo baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi mahakamani hapo la kutaka kufanya majadiliano na Seth na kisha kutoa mrejesho wa kile walichozungumza kwa ajili ya kuimaliza kesi.

Mbali na Seth, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ambao hawajaandika barua ya kukiri mashtaka yao kwa DPP ni aliyekuwa Mwanasheria wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege na Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya IPTL, James Rugemalira.

Katika kesi ya msingi, Seth na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 12 likiwemo la kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

E0NhMwdXIAAW0HL (1).jpeg
 
Ebo!!! Kaiba bilioni 300 analipa bilioni 26?????? Na kifungo cha nje tu!?!?!? Kakiri aliiba halafu anarudisha 10% tu ya alichoiba!!??!!??
Hiyo mbona hata mimi naweza. Hilo fundisho negative kabisa!

Ohhh! Yes! I'm dreaming!!!
 
Lakini naona Singasinga kawa 'trim', na anaonekana mwenye nguvu kuliko alivyokuwa kabla ya yote haya!

Mwanzo alikuwa kavimbiana kama anataka kupasuka! Au shauri ya 'puto'?
Mpk ana six park sa hivi,aliomba kwenda kutolewa hilo puto huko S/Africa akakataliwa wakamwambia alitolee hapa hapa.
 
Leo 16/06/2021 12:45

Dar es Salaam.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth kulipa fidia ya Sh26.9 bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Sh309 bilioni kwa njia ya udanganyifu.

Pia, mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja akitakiwa kutokujihusisha makosa yoyote ya jinai.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amefanikiwa kulipa Sh200 milioni benki na kiasi kinachobakia anatakiwa kukilipa ndani ya mwaka mmoja kuanzia siku ilipotolewa hukumu.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano Juni 16, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa makubaliano ya kuimaliza kesi hiyo.

"Ni wazi kama wakili Marandu alivyotueleza mahakama kuwa Seth ni mkosaji wa mara ya kwanza na ni wazi umekubali mwenyewe kuingia katika makubaliano na DPP (mkurugenzi wa mashtaka nchini), ni wazi umekubali mwenyewe kulipa Sh26.9 bilioni, hivyo mahakama inakuhukumu kifungo cha nje cha mwaka moja, kutokujihusisha na makosa yoyote ya jinai" amesema Shaidi.

Awali, mawakili wawili wakuu wa Serikali, Marterus Marandu, Renartus Mkude na wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon na Faraja Ngukah, walidai kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa mashtaka yake baada ya kuingia makubaliano na DPP.

=====

15/06/2021
Serikali yaafiki maombi majadiliano na Seth

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mtendaji wa PAP, Harbinder Seth, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamepitia barua iliyoandikwa na mshtakiwa huyo na kufikia makubaliano kwa kile alichokiomba. Seth aliandika barua hiyo Juni 10, kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), akiomba kukiri mashtaka yake na kupunguziwa adhabu.

Barua hiyo ilijadiliwa kwa siku mbili na upande wa mashtaka na ule wa utetezi na kisha kutolewa mrejesho.

Wakili wa Serikali Mkuu, Marterus Marandu akisaidiana na Ladslaus Komanya jana alitoa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili Marandu alitoa maelezo hayo wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya upande wa mashtaka kuwasilisha mrejesho wa kile walichozungumza kati yao na Seth kwa ajili ya kuimaliza kesi hiyo.

“Kesi imekuja kwa ajili ya kutoa mrejesho wa barua iliyoandikwa na mshtakiwa huyu (Seth), niseme barua tumeshazipitia kwa pamoja na tumefikia mahali pa kukubaliana kuhusu kile ambacho mshtakiwa alikuwa anakiomba na baada ya hapo, tumekubaliana kuendelea na shauri hili,” alidai wakili Marandu na kuongeza:

“Kwa muktadha huo, upande wa utetezi kama hawatakuwa na pingamizi, naomba shauri hili lije mahakamani hapa kesho ( Juni 16) kwa ajili ya usikilizwaji,” alidai Marandu.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Seth, Melchisedeck Lutema alikubaliana na maelezo ya upande wa mashtaka na kueleza kuwa huo ndio ukweli na ndio msimamo wa pande zote mbili za majadiliano waliyofanya.

Hakimu Shaidi baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Juni 16 itakapoitwa kwa ajili ya usikilizwaji au majadiliano ya kuimaliza kesi.

Hata hivyo, jana Seth alikuwepo mahakamani peke yake, wakati upande wa mashtaka walipowasilisha mrejesho huo.

Itakumbukwa Juni 10, Mahakama hiyo ilikubali upande wa mashtaka kufanya mazungumzo na mshtakiwa huyo ya kuimaliza kesi hiyo. Mahakama hiyo ilirihusu majadiliano hayo baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi mahakamani hapo la kutaka kufanya majadiliano na Seth na kisha kutoa mrejesho wa kile walichozungumza kwa ajili ya kuimaliza kesi.

Mbali na Seth, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ambao hawajaandika barua ya kukiri mashtaka yao kwa DPP ni aliyekuwa Mwanasheria wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege na Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya IPTL, James Rugemalira.

Katika kesi ya msingi, Seth na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 12 likiwemo la kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Hizi pesa hebu tuandikie kwa maneno plz. Sitaki kugeuka kama yule mbunge wa kike bungeni
 
Singa singa intown....sasa ile mitambo pale pameota nyasi....yale ma HOF engines yatahitaji mpunga ww kutosha kuyaamsha na kuyawasha au kuyauza ... Kuna hatari ya kesi inakuja kati ya GOVT na SETH + RUGE na hichi ndicho yule jamaa alikikwepa akaamua kuwahifadhi akiamini kwa mateso na kukosa uhuru natural death itasema nao...
Yaani ilimradi tu kumsumbua jpm...
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom