Uchaguzi 2020 Kamati ya Maadili yatolea ufafanuzi adhabu dhidi ya Lissu kumfungia kampeni. Yasema ameadhibiwa na Kamati ya Vyama 15 vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu

Mara nyingi huwa napenda kumwangalia mtoa tamko machoni kipindi anapotoa tamko...huwa ukweli hujifichi machoni pa mtu
 
Usipende reply ukiwa chooni
Huyu bwana mkubwa umemstukia maana watanzania wanajua nani anayevuruga uchaguzi, ukiwanyima mawakala kufanya kazi zao kwenye kituo cha kura unavuruga uchaguzi kama ilivyotokea kwenye uchaguzi wa marudio kinondoni mpaka Akwiline R.I.P wakamuua, Binafsi watu wa kwanza kuvuruga amani ya nchi hii ni wakurugenzi na watendaji wa kata.Anachokifanya Lissu ni kuwaprovoke kama alivyofanya kwa mapolisi, Lisu na wagombea ubunge na udiwani chadema wanajua kabisa hawatatangazwa hata kama wakishinda, Sasa Lissu anajitengenezea mazingira ya kutoka na wananchi barabarani na alitoa msimamo wake since day one kwamba atawaingiza watu barabarani , kuepusha haya watende haki tu waacha janja janja.
 
KAMATI YA MAADILI: Baadhi ya watu kutaka kuwaaminisha umma wa Watanzania kwamba mgombea huyo ameadhibiwa na tume ya Taifa ya uchaguzi, ukweli ni kwamba bwana Lissu ameadhibiwa na kamati ambayo inajumuisha wawakilishi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi wa kiti cha Rais.

Wajumbe 15 kutoka vyama vya Ada-Tadea, CUF, SAU, UPDP, CHADEMA, CHAUMMA, CCM, NCCR-Mageuzi, DP, UMD, ACT-Wazalendo, NRA, Demokrasia Makini, ADC na AAFP ndio waliotoa adhabu kwa bwana Tundu Lissu.

Kamati pia ina mjumbe kutoka serikalini na mjumbe kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi ambaye ni mwenyekiti wa kamati.

Ifahamike kwamba katika kikao hicho, kulikuwa na mawakili wawili nguli kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) waliosimama kutetea hoja ya bwana Tundu Lissu.

Walisimama mbele ya kamati kujibu hoja zilizokuwepo na kudai kwamba Tundu Lissu na CHADEMA ni vitu viwili tofauti.

Kwa kuzingatia adhabu zilizoainishwa katika kanuni ya 5.11 ya maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 mgombea huyo amepewa adhabu ya kutofanya kampeni kwa muda wa siku 7 kuanzia leo tarehe tatu Octoba mpaka tarehe tisa Octoba. Hii ina maana kwamba haruhusiwi kufanya kampeni zake yeye mwenyewe wala kwa ajili ya mgombea mwingine awaye yeyote.

Endapo mgombea huyo atadharau uamuzi wa kamati na kufanya kampeni atambue kuwa kamati imepewa mamlaka ya kuelekeza makosa mengine kwenye vyombo vingine kadri itakavyoona inafaa kama ilivyoainishwa kwenye kanuni ya 5.7L ya maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2020. Ikimbukwe kuwa katika kipindi cha uchaguzi, sheria nyingine za nchi hazijaacha kufanya kazi.

==============


Hivi punde kamati imetoa sababu na imejibu baadhi ya hoja za Lissu kuhusu adhabu hiyo

Kamati inasema
(1) Kwamba kwa mujibu wa kanuni barua za wito hupelekwa kwa katibu mkuu wa chama maana huyo ndiyo wana anuani zake, na kamati haitunzi anuani za mtu binafsi

(2) Kamati inasema tarehe 24 September Lissu ashapelekewa malalamiko na chama cha SAU yaliyokuja kwa mtindo huu huu yalivyokuja safari hii na Lissu akayajibu, Kamati inashangaa iweje leo Lissu akosoe utaratibu huu, Kamati imumuita Lissu ni Muongo.

(3) Akijibu maswali ya waandishi Ofisa kamati amesema kwa adhabu hii aliyopewa Lissu haruhusiwi kupanda majukwaani na kuwanadi Madiwani au Wabunge maana kitendo cha yeye kupanda majukwaani tu inahesabika kuwa kafanya kampeni.

(4) Msomaji wa Taarifa ya kamati asema kuwa adhabu inamhusu Lissu tu, haihusu mawakala wake, kwa hiyo watu wengine wenye dhamana ya kumpigia kampeni wanaruhusiwa kuendelea kumpigia kampeni

Kwa taarifa zaidi tazama video hii hapa:

View attachment 1588923View attachment 1588924View attachment 1588925

Mh vyama 15 vitoke wapi Tz kuna vyama vya siasa vitatu tu. CCM Chadema na ACT . Vilivyobaki vyote ni CCM B. hata wkt wa mobutu Zaire vyama vilikuwa kama 100 ila ni vya mobutu vyote magirini tu
 
Dr Kawishe ambaye ni mkurugenzi wa sheria pale Tume ya uchaguzi amesema Tundu Lisu hajahukumiwa na NEC bali amehukumiwa na kamati ya maadili yenye yenye wajumbe 15 kutoka vyama vya siasa vyenye wagombea kwenye nafasi ya Rais.

Dr Kawishe ni Katibu wa kamati ya maadili ambayo ni huru!

Maendeleo hayana vyama!
 
Huyu nae kila mda anaongea tu,

Tatzo anajistukia sana, maamuzi ya CHADEMA yamewachanganya.
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Back
Top Bottom