Uchaguzi 2020 Kamati ya Maadili yatolea ufafanuzi adhabu dhidi ya Lissu kumfungia kampeni. Yasema ameadhibiwa na Kamati ya Vyama 15 vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu

Naona Katibu wa kamati ya maadili ya tume ya uchaguzi Dr Kavishe bado amemkalia kooni mgombea urais wa Chadema Tundu Lisu.

Dr Kavishe amesema kinachogombea ni chama cha Chadema ambacho kimemdhamini Tundu Lisu kwa nafasi hiyo hivyo Tundu Lisu atapaswa kutumikia adhabu ambayo kimsingi Chadema wameikubali.
Dr Kavishe amenukuliwa na ITV akisema adhabu ya Chadema kupitia kwa Tundu Lisu ni halali kabisa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ni kweli kabisa kama alivyosema, Adhabu hii ni halali kabisa.

Kikubwa aitumikie tu kama alivyoadhibiwa.
 
Watanzania wanataka uhuru na haki ndani ya nchi yao. Watanzania hawataki kuonewa na kunyanyaswa na kutukanwa ndani ya nchi yao. Ndiyo maana kipindi cha miaka 5 ya Meko amejisifu kuwa kafanya maendeleo sana, lakini why this REJECTION ? Sasa hivi haongelei tena madaraja na madege
 
Ukijifanya unajua sana ndio hivi sasa,

Yeye alifikiri pekeake ndio anajua sheria pekeake
 
Inavyoonekana hata ndani ya chadema lisu anajiona yupo juu ya kila mtu anafanya atakavyo, mbowe kajiweka mbali na huu msala, maana baada ya uchaguzi watz watarudi hapa kuanza kuattack strategies za lisu anazozitumia sasa
 
Watanzania wanataka uhuru na haki ndani ya nchi yao. Watanzania hawataki kuonewa na kunyanyaswa na kutukanwa ndani ya nchi yao. Ndiyo maana kipindi cha miaka 5 ya Meko amejisifu kuwa kafanya maendeleo sana, lakini why this REJECTION ? Sasa hivi haongelei tena madaraja na madege
Limetepeta kama nini?
 
Kwanza kabisa, kwa nini kamati itoe ufafanuzi? Simply means ni kweli uamuzi wake haueleweki na kweli kwamba hoja za Lissu zina mashiko. Kama kamati ina uhakika kuwa ilifuata utaratibu na imempa Lissu haki ya rufaa ilitakiwa ikae kimya isubiri reaction ya Lissu ione kama anapeleka rufaa, au anatekeleza adhabu au anaendelea na kampeni then utaratibu ufuatwe kwa mujibu wa sheria.
Lakini kitendo cha kutoa ufafanuzi tayari ni weakness. Na ufafanuzi sio sehemu ya uamuzi hivyo huwezi kutekeleleza ufafanuzi.
Mfano ni kama jaji amesikiliza kesi akatoa hukumu, anakuwa ameshamaliza haruhusiwi kutoa maelezo eti ufafanuzi wa hukumu zaidi na nje ya kilichoandikwa kwenye hukumu hiyo. Hivyo ambaye hajaridhika huchukua hatua ya kukatarufaa.
 
Lissu anafanya makusudi kuvuruga uchaguzi, kwani anajua hawezi kushinda. Tamanio lake ni kuleta vurugu ili kuchafua nchi kwa wahisani ionekane Tanzania hakuna haki wala demokrasia. Hila zake hazitafanikiwa.

Usipende reply ukiwa chooni
 
KAMATI YA MAADILI: Baadhi ya watu kutaka kuwaaminisha umma wa Watanzania kwamba mgombea huyo ameadhibiwa na tume ya Taifa ya uchaguzi, ukweli ni kwamba bwana Lissu ameadhibiwa na kamati ambayo inajumuisha wawakilishi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi wa kiti cha Rais.

Wajumbe 15 kutoka vyama vya Ada-Tadea, CUF, SAU, UPDP, CHADEMA, CHAUMMA, CCM, NCCR-Mageuzi, DP, UMD, ACT-Wazalendo, NRA, Demokrasia Makini, ADC na AAFP ndio waliotoa adhabu kwa bwana Tundu Lissu.

Kamati pia ina mjumbe kutoka serikalini na mjumbe kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi ambaye ni mwenyekiti wa kamati.

Ifahamike kwamba katika kikao hicho, kulikuwa na mawakili wawili nguli kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) waliosimama kutetea hoja ya bwana Tundu Lissu.

Walisimama mbele ya kamati kujibu hoja zilizokuwepo na kudai kwamba Tundu Lissu na CHADEMA ni vitu viwili tofauti.

Kwa kuzingatia adhabu zilizoainishwa katika kanuni ya 5.11 ya maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 mgombea huyo amepewa adhabu ya kutofanya kampeni kwa muda wa siku 7 kuanzia leo tarehe tatu Octoba mpaka tarehe tisa Octoba. Hii ina maana kwamba haruhusiwi kufanya kampeni zake yeye mwenyewe wala kwa ajili ya mgombea mwingine awaye yeyote.

Endapo mgombea huyo atadharau uamuzi wa kamati na kufanya kampeni atambue kuwa kamati imepewa mamlaka ya kuelekeza makosa mengine kwenye vyombo vingine kadri itakavyoona inafaa kama ilivyoainishwa kwenye kanuni ya 5.7L ya maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2020. Ikimbukwe kuwa katika kipindi cha uchaguzi, sheria nyingine za nchi hazijaacha kufanya kazi.

==============


Hivi punde kamati imetoa sababu na imejibu baadhi ya hoja za Lissu kuhusu adhabu hiyo

Kamati inasema
(1) Kwamba kwa mujibu wa kanuni barua za wito hupelekwa kwa katibu mkuu wa chama maana huyo ndiyo wana anuani zake, na kamati haitunzi anuani za mtu binafsi

(2) Kamati inasema tarehe 24 September Lissu ashapelekewa malalamiko na chama cha SAU yaliyokuja kwa mtindo huu huu yalivyokuja safari hii na Lissu akayajibu, Kamati inashangaa iweje leo Lissu akosoe utaratibu huu, Kamati imumuita Lissu ni Muongo.

(3) Akijibu maswali ya waandishi Ofisa kamati amesema kwa adhabu hii aliyopewa Lissu haruhusiwi kupanda majukwaani na kuwanadi Madiwani au Wabunge maana kitendo cha yeye kupanda majukwaani tu inahesabika kuwa kafanya kampeni.

(4) Msomaji wa Taarifa ya kamati asema kuwa adhabu inamhusu Lissu tu, haihusu mawakala wake, kwa hiyo watu wengine wenye dhamana ya kumpigia kampeni wanaruhusiwa kuendelea kumpigia kampeni

Kwa taarifa zaidi tazama video hii hapa:

View attachment 1588923View attachment 1588924View attachment 1588925
Watanzania wanataka uhuru na haki ndani ya nchi yao. Watanzania hawataki kuonewa na kunyanyaswa na kutukanwa ndani ya nchi yao. Ndiyo maana kipindi cha miaka 5 ya Meko amejisifu kuwa kafanya maendeleo sana, lakini why this REJECTION ? Sasa hivi haongelei tena madaraja na madege
 
Lissu anafanya makusudi kuvuruga uchaguzi, kwani anajua hawezi kushinda. Tamanio lake ni kuleta vurugu ili kuchafua nchi kwa wahisani ionekane Tanzania hakuna haki wala demokrasia. Hila zake hazitafanikiwa.
Aliyeweza kuiba 1.5T na kisha kufukuza CAG mchana kweupe anashindwaje kuiba kura ambazo ni siri? Subiria uone mawakala wa vyama vingine watakavyonimwa nakala za matokeo ndo utajua nani mwenye nia ya kuvuruga utulivu aka amani ya nchi
 
Watanzania wanataka uhuru na haki ndani ya nchi yao. Watanzania hawataki kuonewa na kunyanyaswa na kutukanwa ndani ya nchi yao. Ndiyo maana kipindi cha miaka 5 ya Meko amejisifu kuwa kafanya maendeleo sana, lakini why this REJECTION ? Sasa hivi haongelei tena madaraja na madege
 
Hoja za Lissu kuhusu adhabu hazina mashiko kisheria hata yeye nwenyewe anajua .
Mtu yeyote yule ana physical address yake ambayo ndiyo hutumika pale anapotakiwa kupewa documents. Lissu kama mgombea wa urais kupitia CHADEMA na pia makamu m/ kiti wa chama hicho hawezi dai eti ofisi ya KM wa CHADEMA sio care of (c/f) ya mgombea urais wa CHADEM au Lissu as lon9g as bado ana wadhifa hapo. Vinginevyo aseme physical addresss yake ni ipi maana hakuna mtu mwenye mobile physical address.

Katika nchi yeyote ile kuna mifumo ya kimaamuzi ambayo inawabana wahusika once maamuzi yakitolewa hata kama kuna mtu hakubaliani nayo labda akate rufaa chombo cha juu na uamuzi wa chini utenguliwe.

Lissu alikuwa na nafasi ya kujitetea pengine angeweza kushinda lakini kwa kuburi na kujiona yeye tu ndiye yuko sahihi siku zote na ndiye anayejua akadharau wito; hivyo kesi ikasikilizwa upande mmoja bila maelezo yake ya utetezi.

Hakuna mtu anayeweza kushindana na DOLA katika nchi yeyote hata kama mtu huyo awali alikuwa rais. Lissu hataweza kushindana na dola na hao wanaomdanganya kupitia key board hawatamsaidia lolote.

Dunia kwa sasa ni bipolar haiendeshwi na nchi za magharibi pekee, kuna nchi kama China na Urusi ambazo zimekuwa zukiikabili vilivyo Marekani, hivyo ni kujidanganys eti Tanzania itazipigia magoti nchi za magharibi. Amkumbuke Morgan wa Zimbabwe hadi amekufa alifanikiwa kuing' oa ZANU PF au Mugabe? Syria Venezuela au Iran hali kadhalika?

Uchaguzi utafanyika kihalali na Lissu atashindwa kihalali japo hatakubali matokeo na atawadanganya wafuasi wake aneshinda na ameporwa ushindi lakini haitabadilisha chochote na maisha yatasonga mbele.

Hatuwezi kuwa na nchi kila mmoja ni muamuzi wa kila jambo linalomuhusu, ukifikia hapo unaruhusu anarchy. Lazima pawepo na vyombo vilivyoundwa kwa mujibu wa sheria ili kufanya maamuzi mbalimbali yanayohusu watu. Si lazima wote tukubaliane na maamuzi ya vyombo vilivyowekwa kisheria lakini tuna wajibu wa kutii maamuzi halali yaliyotolewa na vyombo hivyo.

Kuna watu wanamdanganya eti asitii adhabu aendelee na kampeni haya mtumbukizeni shimoni lakini wakati anaangamia atakuwa peke yake.
Nadhani Robert anachangia Sana kumpa huyu jamaa kiburi. Ametamba twiter kuwa yeye ndie aliemshauri asitii.
Screenshot_20201003-161731_1.jpg
 
Lissu anafanya makusudi kuvuruga uchaguzi, kwani anajua hawezi kushinda. Tamanio lake ni kuleta vurugu ili kuchafua nchi kwa wahisani ionekane Tanzania hakuna haki wala demokrasia. Hila zake hazitafanikiwa.
Tatizo lake kubwa hivi sasa mbinu zake zimejulikana na ameamua kufanya makusudi. Anasubiriwa tu wahenga walisema ''subira yavuta heri.''
 
Mataahira sijui mkoje!!! yaani Lissu anavunja kanuni, anaadhibiwa hamtaki!! sasa ataongozaje nchi kama hataki kufuata Kanuni??
TL anafahamu kabisa hawezi kushinda, wewe subiri tu, anaweza kuwa disqualified kwa sababu anafanya makusudi, kupigwa kwake risasi na njama zao na Chadema ndio zinawatesa hivi sasa.
 
Back
Top Bottom