Uchaguzi 2020 Kamati ya Maadili yatolea ufafanuzi adhabu dhidi ya Lissu kumfungia kampeni. Yasema ameadhibiwa na Kamati ya Vyama 15 vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,235
2,000
KAMATI YA MAADILI: Baadhi ya watu kutaka kuwaaminisha umma wa Watanzania kwamba mgombea huyo ameadhibiwa na tume ya Taifa ya uchaguzi, ukweli ni kwamba bwana Lissu ameadhibiwa na kamati ambayo inajumuisha wawakilishi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi wa kiti cha Rais.

Wajumbe 15 kutoka vyama vya Ada-Tadea, CUF, SAU, UPDP, CHADEMA, CHAUMMA, CCM, NCCR-Mageuzi, DP, UMD, ACT-Wazalendo, NRA, Demokrasia Makini, ADC na AAFP ndio waliotoa adhabu kwa bwana Tundu Lissu.

Kamati pia ina mjumbe kutoka serikalini na mjumbe kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi ambaye ni mwenyekiti wa kamati.

Ifahamike kwamba katika kikao hicho, kulikuwa na mawakili wawili nguli kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) waliosimama kutetea hoja ya bwana Tundu Lissu.

Walisimama mbele ya kamati kujibu hoja zilizokuwepo na kudai kwamba Tundu Lissu na CHADEMA ni vitu viwili tofauti.

Kwa kuzingatia adhabu zilizoainishwa katika kanuni ya 5.11 ya maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 mgombea huyo amepewa adhabu ya kutofanya kampeni kwa muda wa siku 7 kuanzia leo tarehe tatu Octoba mpaka tarehe tisa Octoba. Hii ina maana kwamba haruhusiwi kufanya kampeni zake yeye mwenyewe wala kwa ajili ya mgombea mwingine awaye yeyote.

Endapo mgombea huyo atadharau uamuzi wa kamati na kufanya kampeni atambue kuwa kamati imepewa mamlaka ya kuelekeza makosa mengine kwenye vyombo vingine kadri itakavyoona inafaa kama ilivyoainishwa kwenye kanuni ya 5.7L ya maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2020. Ikimbukwe kuwa katika kipindi cha uchaguzi, sheria nyingine za nchi hazijaacha kufanya kazi.

==============


Hivi punde kamati imetoa sababu na imejibu baadhi ya hoja za Lissu kuhusu adhabu hiyo

Kamati inasema
(1) Kwamba kwa mujibu wa kanuni barua za wito hupelekwa kwa katibu mkuu wa chama maana huyo ndiyo wana anuani zake, na kamati haitunzi anuani za mtu binafsi

(2) Kamati inasema tarehe 24 September Lissu ashapelekewa malalamiko na chama cha SAU yaliyokuja kwa mtindo huu huu yalivyokuja safari hii na Lissu akayajibu, Kamati inashangaa iweje leo Lissu akosoe utaratibu huu, Kamati imumuita Lissu ni Muongo.

(3) Akijibu maswali ya waandishi Ofisa kamati amesema kwa adhabu hii aliyopewa Lissu haruhusiwi kupanda majukwaani na kuwanadi Madiwani au Wabunge maana kitendo cha yeye kupanda majukwaani tu inahesabika kuwa kafanya kampeni.

(4) Msomaji wa Taarifa ya kamati asema kuwa adhabu inamhusu Lissu tu, haihusu mawakala wake, kwa hiyo watu wengine wenye dhamana ya kumpigia kampeni wanaruhusiwa kuendelea kumpigia kampeni

Kwa taarifa zaidi tazama video hii hapa:

tumeyauchaguzi_tanzania_20201003_2.jpg
tumeyauchaguzi_tanzania_20201003_3.jpg
tumeyauchaguzi_tanzania_20201003_4.jpg

 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,899
2,000
Tume hii iliyojaa doublestand nani mwenye akili ataiamini?

Ina maana kwenye hizo form za kugombea wahusika hawajazi ananuani zao?

Na kama hawajazi anuani tofauti na za vyama vyao bali wanajaza za chama, nani alipaswa kuwa addressed kwenye hiyo barua kupitia ananuani ya chama?

Je, si walipaswa kumu-address Lissu kama mgombea kupitia anuani ya chama chake?
 

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,961
2,000
Wanachojaribu kufanya ni kuwatisha watu wanaomzunguka. Hii itafanyika kwa njia ya kuwakamata na kuwafungulia makesi na njia zingine. Nia ni kumfanya Lissu ajione hana watu madhubuti na wenye misimamo kama yeye au tu kumkatisha tamaa aone anachojaribu kufanya hakiwezekani.

Mliona Salum Mwalimu alivyoshindwa kujitetea kama Lissu pale alipotaka kusimama kusalimia watu. Huko Lema amekamatwa. Huko Iringa kuna viongozi wamepewa kesi za mauaji, nk.

Watu wote mlioamua kusupport kampeni inabidi mpige moyo konde. Majaribu na vizingiti vitakuwa vingi na vikubwa sana kwa jinsi siku zinavyokwenda.
 

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
1,308
2,000
Hv tuvyama vya mfukon vya SAU ni maccm tupu
Hii ni tume 2020 na imevunja historia, nakumbuka 2010 Dr slaa alikua anarusha mawe ya kufa mtu kwa JK na serikali yake ila hatukuyaona haya, 2015 Lowassa alirushiwa mawe kutoka chama dola hatukuyaona haya.

Mpaka mda huu wananchi wamepoteza Sana Imani juu yao Sana Jambo ambalo naliona sio zuri tunapoelekea, bora kusitisha uchaguzi , kuepuka yanayoweza jitokeza mbele.
 

Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
8,555
2,000
Cha kujiuliza hapa ni: hivi ni nani mgombea wa Urais kwa tiketi ya SUA, ukisha libaini hilo ndio utajuwa nini kinaendelea nyuma ya pazia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom