Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,810
- 11,981
Matukio Katika Picha: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwaongoza Viongozi wa Kitaifa na Kimataifa pamoja na Wananchi katika Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam
#Miaka60YaUhuru
#AMANIYETUFURAHA YETU
====
UPDATES:
1150hrs: Vijana wanaendelea na maonesho.
======
Rais Samia awashukuru watanzania kwa kufika uwanja wa Jamhuri kuadhimisha maadhimisho ya siku ya Uhuru, Na pia ametoa utambulisho wa Viongozi mbalimbali wa Nchi tofauti wakiwemo wawakilishi waliowawakilisha viongozi wakuu wa nchi.
Lakini pia amemtaja Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kuwa ndiye mgeni rasmi katika shughuli hii ya leo na kuwa yupo nchini kwa ziara maalum.
Dar es Salaam. Marais wa nchi nne pamoja na marais wastaafu watatu wamehudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru zinazoendelea sasa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Desemba 9,2021.
Marais hao ni wa Kenya, Rwanda, Msumbiji pamoja na visiwa vya Comoro na wengine ambao hawakuweza kufika wametuma wawakilishi.
Kati yao, alianza kuwasili rais mstaafu wa Malawi Joyce Banda ndiye na kufuatiwa na rais mstaafu wa Msumbiji aliyeambatana na Waziri wake wa Afya.
Baadaye aliwasili rais mstaafu wa Botswana aliyeambatana na waziri wa mambo ya nje na baadaye aliwasili waziri mkuu wa nchini DRC Congo.
Aliyefuata alikuwa rais wa visiwa vya Comoro, Azali Assouman, rais wa Msumbiji, Philipe Nyusi, rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na wa mwisho alikuwa rais wa Rwanda Paul Kagame.
Viongozi wengine waliowasili ni rais wa mahakama ya Afrika, mabalozi wa nchi mbalimbali na wakurugenzi wa wizara.