Dkt. Stergomena Tax ashiriki sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 60 ya muungano Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
866
547
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA ASHIRIKI SHEREHE ZA UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO ZANZIBAR

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Aprili 14, 2024 ameshiriki katika sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika viwanja vya Dimani, Nyamanzi Zanzibar, ambapo Mgeni rasmi katika Uzinduzi huo alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Uzinduzi wa Sherehe hizo za Muungano zilizoongozwa na Rais Hussein Ali Mwinyi zilihudhuriwa na Viongozi na Mawaziri toka pande zote mbili za Muungano na zilitanguliwa na Rais Mwinyi kutembelea maonesho ya Taasisi za Serikali za Muungano na burudani ya vikundi vya utamaduni na ngoma za Asili toka Zanzibar na Tanzania bara.

IMG-20240415-WA0006.jpg
IMG-20240415-WA0005.jpg

IMG-20240415-WA0007.jpg
IMG-20240415-WA0004.jpg
 
Back
Top Bottom