Miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar sherehe zipo. Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyia sherehe hakuna. Huu siyo upofushaji?

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Nchi mbalimbali duniani huona fahari sana kukumbuka siku za kuzaliwa mataifa yao. Neno kuzaliwa nimemaanisha siku ya kupata uhuru.

Nimeangalia majuzi hapa kwa jirani zetu Kenya, walisherehekea siku yao ya Uhuru kwa kishindo wakiwa pamoja na Rais wao Dr. Ruto. Nchi nyingi hasa zilizojikomboa kutoka kwa tawala dhalimu za kikoloni hukumbuka siku hiyo muhimu kwa njia mbalimbali. Kama vile magwaride rasmi ya vikosi vya majeshi yao, ngoma za aslili. Nyimbo za kusifu na hufanyika kwa mtindo maalumu uitwao "Public Rally".

Nini lengo hasa la nchi kufanya vile;'
1. Ni kumbukizi kwa wananchi hasa waliokuwepo kipindi cha uhuru wasisahau walikotoka.
2. Ni kurithisha vijana au watoto waliozaliwa baada ya uhuru historia ya nchi yao. Wajue kuwa hawa baba, babu, bibi zao walionao leo wamefanya makubwa huko nyuma.
3. Ni kujenga uzalendo kwa wananchi kuwa kumbe ukiwa na dhamira unaweza kujiletea maendeleo.
4. Kuwapa fursa wananchi kuweza kutathmini mwenendo wa maendeleo ya nchi yao kila mwaka, kuona wapi parekebishwe ili kuongeza kasi ya maendeleo.
Kwa miaka ya karibuni Tanzania Bara(Tanganyika) imekuwa ikiahirisha sherehe hizo zinazopaswa kufanyika kila Disemba 9 kwa kutolewa sababu mbalimbali. Mwaka jana 2023 hazikufanyika japo kulikuwa na mapumziko ya kimyakimya ya Kitaifa. Pamoja na mapumziko, lilifanyika zoezi la Kikazi la kusoma Mpango wa Maendeleo 2025- 2050.

Wakati huohuo sherehe kama hizo ambazo zimepewa jina la [ Sherehe za Mapinduzi] kule Zanzibar zimekuwa zikifanyika. Leo zinafanyika uwanja wa Amaan kuanzia saa 8 mchana. Na nafikiri Viongozi kutoka Bara kama ambavyo imekuwa huko nyuma,watajisomba kwenda kuhudhuria.

Kuna mtanziko mkubwa unaojijenga ndani ya Watanganyika kuwa nini kinafichwa?
Huko nyuma Sherehe hizi za Uhuru, kwa Tanganyika zilifanyika kwenye vijiji kata,wilaya na hata Kimkoa kwa wananchi kujumuika pamoja kwa hamasa kubwa. Hakukuwepo na ulazima wa kutumia gharama kubwa ambayo imewahi kuelezwa kuwa ndiyo sababu ya Nchi kutofanya sherehe hizo.

Labda kama ni suala la gharama kubwa, hivi inakuwaje kuchangia Taifa Stars Bilioni 3 kwa siku moja kuona ni fahari na kipaumbele zaidi?

Kama kuahirisha sherehe ni suala la kukosa fedha, ni nini kiliwanyima viongozi wa vijiji,kata,wilaya, mikoa, na hata Taifa kuchangisha kama ilivyofanyika kwa Taifa Stars? Mbona sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru wananchi wamekuwa wakichangia? Ni nani anataka kupofushwa hapa? Kwamba siku hizi Zanzibar iko more organized kuliko Tanganyika(Bara).

Mimi kama Mwananchi ninayo haki Kikatiba kutoa maoni,kushauri au kuhoji pale viongozi wetu wanapokwenda sivyo.

Haipendezi machoni pa Watanganyika kuwa wenzao Waunguja wanasherehekea, kwao wamezimwa. Ingefaa pote wafanye au pote wasifanye.

Niombe walioguswa kwa njia moja au nyingine na mtanziko huu tuishauri Serikali ni nini kifanyike ili tusherehekee sherehe hizi kama wafanyavyo Mataifa mengine. Ilikuwa ni utamaduni wetu kusherehekea kwa hamasa. Na Mwl. Nyerere aliwahi kusema,nanukuu " Taifa lisilokuwa na utamaduni wake na sawa ni Taifa mfu" . Mwisho wa kunukuu.
 
Zanzibar wakifanya ni sawa maana Zanzibar Bado ipo, Tanganyika Iko wapi hadi ifanye hiyo sherehe?
Kwani imenda wapi?.Hizi siasa uchwara tusizipe muda wakuzijadili kwasababu tunapoteza utaifa wetu kwasababu zakisiasa zinazokana na ujinga wakutojitambua.
 
kwani sherehe si alizifuta rais magufuli, akasema hela znazotumika kwenye sherehe karbu ma billion bora zkatumike kwenye shughuri za maendeleo au nmekosea
 
Sherehe hazijafutwa ila kwa mwaka husika rais anaweza kuamua zisifanyike hela iende kwenye shughuli nyingi kwangu naona ni jambo jema tumeshazifanya sanaa.
 
Nchi mbalimbali duniani huona fahari sana kukumbuka siku za kuzaliwa mataifa yao. Neno kuzaliwa nimemaanisha siku ya kupata uhuru.

Nimeangalia majuzi hapa kwa jirani zetu Kenya, walisherehekea siku yao ya Uhuru kwa kishindo wakiwa pamoja na Rais wao Dr. Ruto. Nchi nyingi hasa zilizojikomboa kutoka kwa tawala dhalimu za kikoloni hukumbuka siku hiyo muhimu kwa njia mbalimbali. Kama vile magwaride rasmi ya vikosi vya majeshi yao, ngoma za aslili. Nyimbo za kusifu na hufanyika kwa mtindo maalumu uitwao "Public Rally".

Nini lengo hasa la nchi kufanya vile;'
1. Ni kumbukizi kwa wananchi hasa waliokuwepo kipindi cha uhuru wasisahau walikotoka.
2. Ni kurithisha vijana au watoto waliozaliwa baada ya uhuru historia ya nchi yao. Wajue kuwa hawa baba, babu, bibi zao walionao leo wamefanya makubwa huko nyuma.
3. Ni kujenga uzalendo kwa wananchi kuwa kumbe ukiwa na dhamira unaweza kujiletea maendeleo.
4. Kuwapa fursa wananchi kuweza kutathmini mwenendo wa maendeleo ya nchi yao kila mwaka, kuona wapi parekebishwe ili kuongeza kasi ya maendeleo.
Kwa miaka ya karibuni Tanzania Bara(Tanganyika) imekuwa ikiahirisha sherehe hizo zinazopaswa kufanyika kila Disemba 9 kwa kutolewa sababu mbalimbali. Mwaka jana 2023 hazikufanyika japo kulikuwa na mapumziko ya kimyakimya ya Kitaifa. Pamoja na mapumziko, lilifanyika zoezi la Kikazi la kusoma Mpango wa Maendeleo 2025- 2050.

Wakati huohuo sherehe kama hizo ambazo zimepewa jina la [ Sherehe za Mapinduzi] kule Zanzibar zimekuwa zikifanyika. Leo zinafanyika uwanja wa Amaan kuanzia saa 8 mchana. Na nafikiri Viongozi kutoka Bara kama ambavyo imekuwa huko nyuma,watajisomba kwenda kuhudhuria.

Kuna mtanziko mkubwa unaojijenga ndani ya Watanganyika kuwa nini kinafichwa?
Huko nyuma Sherehe hizi za Uhuru, kwa Tanganyika zilifanyika kwenye vijiji kata,wilaya na hata Kimkoa kwa wananchi kujumuika pamoja kwa hamasa kubwa. Hakukuwepo na ulazima wa kutumia gharama kubwa ambayo imewahi kuelezwa kuwa ndiyo sababu ya Nchi kutofanya sherehe hizo.

Labda kama ni suala la gharama kubwa, hivi inakuwaje kuchangia Taifa Stars Bilioni 3 kwa siku moja kuona ni fahari na kipaumbele zaidi?

Kama kuahirisha sherehe ni suala la kukosa fedha, ni nini kiliwanyima viongozi wa vijiji,kata,wilaya, mikoa, na hata Taifa kuchangisha kama ilivyofanyika kwa Taifa Stars? Mbona sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru wananchi wamekuwa wakichangia? Ni nani anataka kupofushwa hapa? Kwamba siku hizi Zanzibar iko more organized kuliko Tanganyika(Bara).

Mimi kama Mwananchi ninayo haki Kikatiba kutoa maoni,kushauri au kuhoji pale viongozi wetu wanapokwenda sivyo.

Haipendezi machoni pa Watanganyika kuwa wenzao Waunguja wanasherehekea, kwao wamezimwa. Ingefaa pote wafanye au pote wasifanye.

Niombe walioguswa kwa njia moja au nyingine na mtanziko huu tuishauri Serikali ni nini kifanyike ili tusherehekee sherehe hizi kama wafanyavyo Mataifa mengine. Ilikuwa ni utamaduni wetu kusherehekea kwa hamasa. Na Mwl. Nyerere aliwahi kusema,nanukuu " Taifa lisilokuwa na utamaduni wake na sawa ni Taifa mfu" . Mwisho wa kunukuu.
Naona unataka kurejesha rasimu ya katiba ya Jaji Warioba kiujanja.
 
Sherehe hazijafutwa ila kwa mwaka husika rais anaweza kuamua zisifanyike hela iende kwenye shughuli nyingi kwangu naona ni jambo jema tumeshazifanya sanaa.
Hizo shughuli nyingine ni za dharura? Na kama ni hivyo , tuna mapungufu ya kifikra.
 
Ni sawa kabisa kwa kuwa Zanzibar ipo na ni nchi ikiwa na vigezo vyote vya kuitambulisha kama nchi akiwepo rais, baraza la mawaziri, bunge, mahakama, jaji mkuu, jeshi, wimbo wa taifa, bendera ya taifa nk.

Tanganyika ilishakufa haina hivyo vyote nilivyoeleza kuitambulisha kama nchi hivyo haina uhuru tena wa kuamua mambo yake ndiyo maana anaweza kuja mzanzibari Tanganyika akawa kuongozi hadi kuwa rais, kumiliki ardhi na majengo lakini hakuna mtanganyika anayeweza kuwa hata sheha au nyumba kumi kule na hawezi kumiliki ardhi kule kama mtanzania ila atahesabika kama mgeni mwekezaji.

Hivyo hakuna ya kuwa na sherehe za nchi ambayo haipo ni kupoteza muda na pesa. Zanzibar wakati wa sherehe rais wao anakagua gwaride. Tanganyika inakaguliwa na mtu ambaye siye rais wa Tanganyika bali wa Tanzania nchi ambayo haijawahi kupata uhuru. Sherehe za uhuru Tanganyika zifutwe mpaka Tanganyika itakaporudi
 
Muungano wetu bado una dosari kubwa.
 
Back
Top Bottom