CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Nyama vingine sio mali ya mtu binafsi!
NADHANI NI UAMUZI SAHIHI NA MAKINI, KAMA SERIKALI IMEDHAMIRIA KUIPA CCM USHINDI KWA NJIA HISIYO SAHIHI, HAKUNA HAJA, WAACHIWE, MWENYE NGUVU MPISHA, KULIKO KUATARISHA, KUFUNGULIWA KESI KAMA HIZO ZA TARIME, KUJERUIWA NA HATA MUDA MWINGINE KUHATARISHA MAISHA YAO. SIKU NA MWAKA AKIJA FARAO ANAYE HESHIMU DEMOKRASIA NA KUHESHIMU KATIBA NA SHERIA ZA NCHI, WALEJEE KWENYE CHAGUZI. Soma biblia kitabu cha KUTOKA
Kutoka 1:8-22
[8]Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.
[9]Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi.
[10]Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.
[11]Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.
[12]Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli.
[13]Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali;
[14]wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.
[15]Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua;
[16]akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.
[17]Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.
[18]Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai?
[19]Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia.
[20]Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi.
[21]Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.
[22]Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.
 
napongeza kwa maamuzi mazuri ili watanzania tubaki na amani yetu kuliko kushiriki upuuzi huu
 
Haya mambo mnayafurahia ila mwisho wake ni mbaya sana kwa CCM.
Dhambi hii haiwezi kuwaacha salama, kitakachowakuta ni kugawanyika wenyewe kwani hata 2020 mtakuwa na timu ndani ya CCM na uchaguzi ukiisha mtaanza kunyoosheana vidole wenyewe msijue adui yenu ni nani na hapo ndio maandiko yatatimia.
Washindane wenyewe kwa wenyewe.wapasuanee
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Pia soma
CDM pengine na vyama vingine ambavyo vitaufuata mkumbo huo, visiishie tu ktk kuususia uchaguzi tu. Vifanye kitu kingine ili kuweza kuleta mgogoro wa kisiasa.

Suala lililobakia sasa ni kutangaza mgogoro sasa kwa uwazi kabisa, CDM sasa kupitia BAVITA iratibu maandamano nchi nzima siku ya tarehe 24 ili kupinga huo uchaguzi. Waratibu kama walivyofanya kwenye "operation" ya UKUTA ama kwa njia ya hamasa kupitia mitandao ya mithili ya alivyofanya Mange Kimambi.

Hamasa ya namna hii ikifanyika hata kama hawatadhamiria kuifanya kwa dhati. Lkn "impact" yake itawafanya makada wa CCM na polisi wasilale na kupata muda wa ziada wa mapambano.

Jambo la pili ni kuanza kutoa matishio ya uvumi wa uwepo wa vitu vya milipuko ktk maeneo ya kupigia kura. Hawatambui Watanzania wenzetu,, kwa uvumi kama huu utawafanya walale mbele kwa kuogopa kudhurika hata kama watahakikishiwa usalama na vyombo vya dola.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Pia soma
In reality CDM haijajiondoa bali imeondolewa na uhuni wa Jiwe.
 
Naona kuna Faida chache na Hasara nyingi kwa CHADEMA Kujitoa katika hizi Chaguzi. Sauti zao za Malalmiko huenda zingesikika kwa uharaka na kupatiwa Ufumbuzi hata Kimataifa. Maamuzi yao haya ni ya Kimhemko, Kimkakati na Kipropaganda zaidi.
Hakuna tena kungoja kama upuuzi umefanyika kwa muda mrefu sana.nikuulize kama chadema wagombea wao wameenguliwa ulikua unataka washiriki kufanya nini kwenye huu uchafuzi na ubakaji wa demokrasia.
 
Back
Top Bottom