BBC wako sahihi kuita jengo la Freemason kanisa?

BBC wako sahihi kuita jengo la Freemason kanisa?

umeambiwa bbc walitoa habari kwa kiswahili na si kwa kiarabu. Mjomba elewa freemason majumba yao hayaitwi kanisa, kanisa ni mwili wa kristo na wakristo huabudu kanisani
Kanisa ni neno la kiarabu wewe mbwiga,kama hayo majengo yenu ni mwili wa kristo tafuteni neno jingine muyaite
 
Nikiwa simba basi siijui yanga?.. vichwani huwa mmejaza nini!?..nahitaji kuwa mkristo Ili niujue ukristo?
kwa taarifa yako: uKristo sio dini. mtu mKristo ni mtu mwenye huyo Kristo ndani ya moyo wake. huna Huyo Kristo huwezi kuujua uKristo! wewe unafananisha uKristo na Yanga? what a tragedy!

haya ni mambo ya kiroho, sio ya kifalsafa.
 
sasa kama unajibu kihuni ni vema pia hayo majengo ya freemason yakatwa pia msikiti wa freemason kwa mtazamo wako
Nimekuambia msikiti ni masjid,sharti watu wawe wanasujudu(sijda,sujuud,masjid-msikiti), freemason hawasujudu
 
kwa taarifa yako: uKristo sio dini. mtu mKristo ni mtu mwenye huyo Kristo ndani ya moyo wake. huna Huyo Kristo huwezi kuujua uKristo! wewe unafananisha uKristo na Yanga? what a tragedy!

haya ni mambo ya kiroho, sio kifalsafa.
Ukristo ni dini, waarabu wanaita masihiya(wafuasi wa masihi), suala la luna na kristo ndani,sijui roho mtakatifu akuongoze ni porojo, uwongo tu
 
Kanisa ni watu walioitwa na Mungu kwa ajili ya kusudi la Mungu. Ni watu waliookolewa, na Imani yao Iko katika Kristo Yesu Bwana. MDO 2:47.

neno kanisa limetokana na neno la kigiriki "ekklesia" ikimaanisha kusanyiko la watu wa Mungu.
Mkuu una uhakika hilo neno lina maana ya kusanyiko la watu wa Mungu na si kusanyiko tu?

Kwahiyo hapo BBC wapo sawa tu kutumia neno kanisa kuita hilo jengo au hawako sawa?
 
Mkuu una uhakika hilo neno lina maana ya kusanyiko la watu wa Mungu na si kusanyiko tu?

Kwahiyo hapo BBC wapo sawa tu kutumia neno kanisa kuita hilo jengo au hawako sawa?
Nina uhakika.

kanisa sio jengo, kanisa ni watu wa Mungu. Watakatifu kwa maana ya kutengwa kwa ajili ya kazi ya Bwana.

hakuna kanisa la freemason, halipo!
 
Yesu alitumwa kwa ajili ya a Wana wa israel waliopotea,mimi mtu wa mataifa alinifananisha na mbwa nisiyefaa kupewa chakula cha watoto(Wana wa israel)
Matendo ya Mitume 28 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁶ akisema, Enenda kwa watu hawa, ukawaambie, Kusikia, mtasikia wala hamtafahamu; Na kuona, mtaona wala hamtatambua;
²⁷ Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni mazito ya kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kubadili nia zao, nikawaponya.
²⁸ Basi ijulikane kwenu ya kwamba wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwa Mataifa, nao watasikia!
²⁹ Alipokwisha kusema hayo, Wayahudi wakaenda zao, wakiulizana mengi wao kwa wao.]
 
Nina uhakika.

kanisa sio jengo, kanisa ni watu wa Mungu. Watakatifu kwa maana ya kutengwa kwa ajili ya kazi ya Bwana.

hakuna kanisa la freemason, halipo!
Mkuu naona unatumia tafsiri ya kidini au kiimani katika neno kanisa.
 
Back
Top Bottom