Huyu hapa jamaa aliyejaribu kuibia freemasons

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,591
Reaction score
4,471
HUYU HAPA JAMAA ALIYEJARIBU KUIBIA FREEMASONS
Huruma sio malezi. Ukijaribu kucheza na fedha za makundi ya siri ya dunia huku ukiwa na wazo la kuwapiga changa la macho, lazima utambue kuwa unaandika mkataba wako mwenyewe wa kifo.

Huu ni mkasa wa Roberto Calvi, mwanabenki aliyefikiri ana akili nyingi kuliko mtandao wa siri uliomweka mjini.

Roberto Calvi Ni Nani?

Kama jina hili ni geni kwako, Roberto Calvi alikuwa mwanabenki nguli nchini Italia na Mwenyekiti wa benki kubwa ya kibinafsi iliyoitwa Banco Ambrosiano.
Alikuwa mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa zaidi wa kifedha Ulaya. Kwa sababu benki yake ilikuwa na ushirikiano mzito wa kimkakati na wa karibu sana na Benki Kuu ya Vatican, vyombo vya habari vya kimataifa vilimpa jina la utani la "God's Banker" (Mwanabenki wa Mungu). Lakini nyuma ya suti zake za kishua na heshima ya mtaani, Calvi alikuwa mchezaji wa kamari kwenye mtandao mzito wa siri.

Mtandao Haramu: P2, Vatican, na Mwanabenki
Calvi hakuwa anafanya michezo yake peke yake. Ili kutakatisha mabilioni na kufanya uwekezaji wa kificho, alitengeneza ushirikiano wa pembetatu hatari sana:

Lodge ya P2 (Freemasons): Kundi la siri la Freemasons lililojulikana kama Propaganda Due (P2), lililoongozwa na Licio Gelli. Calvi alikuwa mwanachama wa P2 pamoja na mwanabenki hatari Michele Sindona (aliyetumika kama daraja kati ya Freemasons na mtandao wa Mafia).

Kanisa la Katoliki (Vatican): Mfumo wa Benki Kuu ya Vatican (Institute for the Works of Religion - IOR) chini ya Kanisa la Roman Catholic.

Askofu Paul Marcinkus: Askofu Mkuu raia wa Marekani aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Vatican. Askofu Marcinkus ndiye aliyekuwa mshirika mkuu wa Calvi, akimpa barua rasmi za udhamini na makampuni ya kivulini (shell companies) huko Panama na Bahamas ili kupitisha mabilioni ya dola bila kukaguliwa na serikali.

Calvi alitumia mgongo wa Benki ya Vatican na ulinzi wa Freemasons wa P2 kukopa na kuzungusha zaidi ya Dola Bilioni 1.3. Lakini Calvi alianza kufanya makosa makubwa—alianza kutumia sehemu ya fedha hizo za mtandao wa P2 na Mafia kwa matumizi yake binafsi na uwekezaji wa kijinga uliokula hasara.

Wakati benki yake ya Banco Ambrosiano inafilisika mwaka 1982, Calvi alikimbia nchini Italia. Alijua wazi kuwa akileta ujeuri, atafungwa au kuuawa. Basi, alianza kutoa vitisho: alitishia kufichua orodha ya wanachama wa Freemasons wa P2, viongozi wa kisiasa, na siri za Askofu Paul Marcinkus na Benki ya Vatican na kutisha angetoa siri jinsi kanisa linavyotakatisha fedha kama wasingemwokoa!

Calvi alisahau kanuni moja kuu: Freemasons wa P2 hawajawahi kutishiwa na mtu wao wa ndani.

Tarehe 18 Juni 1982, mwili wa Calvi ulipatikana unaning'inia chini ya daraja la Blackfriars jijini London. Wajumbe wa P2 na Mafia walimwekea mawe mazito mifukoni mwake—ishara ya kiutamaduni ya Masonic inayohusu "kujenga" na nidhamu—kabla ya kumnyonga.

Licio Gelli na mtandao wa P2 walihakikisha sauti ya Calvi inazimwa milele kabla hajataja majina ya Askofu Marcinkus na mabwana wakubwa wa kundi hilo la siri.

Mpaka sasa mwaka 2002 kesi ilirudi mahakamani ila ilikosa ushahidi wa nani alihusika kuagiza mauaji ya jamaa huyu, washukiwa wakiwa watatu
Freemasons, Vaticans au Mafia.
Wengi hupinga kua na andika makala za uongo, ila kabla hujapinga basi tumia hata Google kucheki kisa nyuma ya hilo jina Roberto Calvi.
1787927231248.jpg
 
Wengi hupinga kua na andika makala za uongo, ila kabla hujapinga basi tumia hata Google kucheki kisa nyuma ya hilo jina Roberto Calvi.View attachment 3658984
Wakati haya yakitokea wewe ulikua wapi dogoli kinyamkela ?
 
kuna dhambi zingine za asili kama tamaa kwa wanaume unapoona mapaja ya mwanamke unawezaje kuacha?
yani hapa mkuu, nikukimbia hilo eneo kwa nguvu zako zote, maana hata mimi hua inanishinda, yani kuna jirani hapa anajifunga kanga inaishia kwenye mapaja akiwa anaenda kuoga yaninikionaga tu et! mtandao chapu na haraka unasoma! Naanza kujikumbusha zaburi tu nisiwaze zaidi.
 
Back
Top Bottom