Magufuli kaondoka phase one na two ziko asilimia ngapi? Wewe unajua utaratibu wa malipo Serikalini ni wa awamu (as per certificate), unadhani hizo percentage pesa zilitoka wapi? Alafu vipi kuhusu phase 3,4,5 na leo 6……hizo hela zinatoka wapi?
Magufuli aliacha Bwawa liko below 20% leo linakimbia over 70%, hizo zote ni hela.
Magufuli aliacha BRT phase 2 ikiwa inasuasua, leo tumepata pesa hadi ya phase 5.
Magufuli aliacha ndege 6 nadhani, Samia kaongeza tano zinakuja.
Mji wa Serikali Dodoma, Magufuli aliacha wizara zinatumia majengo madogo, Samia kaongeza hela wizara zote zinamalizia majengo yao makubwa kuwezesha watumishi wote kuamia kule.
Barabara, Samia kaweka hela za kujenga ring road Dodoma over 105km, hapo sijaweka za TARURA.
Daraja la Busisi JPM aliacha liko chini ya 20% leo limefika 60%,
Miradi iko mingi na hizo zote ni hela ambazo bajeti yetu haiwezi kussuport. Huu ndio ukweli. Tuendelee kukopa au tulipe kodi, tuchague tunataka nini…..!!