Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Na miradi mikubwa a.k.a mega projects tunazofanya kwa pesa za ndani hela inapitia wapi vileeee
Bwahaha!!hamna uwezo huo kiuchumi nyie raia wa kwaida
We kubali tu km wakenya wana nguvu kiuchumi hapa EA...

Eti miradi ya ndani wakati external debt ni kubwa inacheza 80%
 
Hahahaha, Tony naona kichwa kimepata moto Leo, unadhani nchi kuagiza bidhaa nyingi kutoka nchi zingine(Imports) ni positive or negative

Hawa wako kinyume sana na natural principles. Mfano utakuta Tony254 anajigamba kwamba kuna wengi sana nje ya nchi kuliko nchi nyingine ukana huu. Sasa yeye hajui hiyo ni sign moja wapo ya failure. Most of the failed states have a big number of their citizens abroad. Mfano ni hapo jirani zao wa hapo kaskazini. Nimetembea mabara yote duniani, hamna sehemu ambayo sikuwakuta. Mpaka kuna nchi fulani ulaya, kuna kaeneo wamejazana kanaitwa mogadishu. 😛 🤣 😆
 
Hawa wako kinyume sana na natural principles. Mfano utakuta Tony254 anajigamba kwamba kuna wengi sana nje ya nchi kuliko nchi nyingine ukana huu. Sasa yeye hajui hiyo ni sign moja wapo ya failure. Most of the failed states have a big number of their citizens abroad. Mfano ni hapo jirani zao wa hapo kaskazini. Nimetembea mabara yote duniani, hamna sehemu ambayo sikuwakuta. Mpaka kuna nchi fulani ulaya, kuna kaeneo wamejazana kanaitwa mogadishu.
Nyie endeni sauzi aflika bana, si tumeelewana sauzi aflika ndio kuna maisha mazuri sana kuliko sehemu yyte ile duniani
 
Mpuuzi pekeake ndio atakuja kuandika ujinga kisa hasira..
Wakenya wana nguvu kiuchumi kuliko tz mara kadhaa..
Haiwezekani eti nyie mjiite mna uchumi bora wakati zero, tuonyeshe mobile banking tz inaingiza pesa ngapi na mabenki je kampuni binafsi vipi..

Nyie watu misifa tu lkn zero kabisa kiuchumi

I can see how nerves have been tormented.
Relax, huu mchezo hauhitaji hasira. Jikaze tu hata kama huja pata kiamsha kinywa.
😛 😛 😛
 
Ninakubaliana na wewe kwamba Kenya uchumi wake ni tofauti hapa Sub-sahara Afrika
1) Ni nchi pekee ambayo ni "middle income" lakini inategemea chakula cha msaada
2)Ni nchi pekee ambayo haiwezi kujenga hata 5Km ya railway bila kukopa
3)Ni nchi pekee ambayo inakusanya pesa nyingi lakini bado inategemea mikopo kuendesha nchi kwa 80%
4)Nchi pekee ambayo uchumi wake ni mkubwa lakini raia wake wanategemea nchi jirani kupata huduma Bora za Afya.

Kitendo cha kwamba mnakusanya Kodi mara dufu ya Tanzania, lakini Tanzania inafanya miradi mingi kwa pesa za ndani kuliko Kenya, hiyo ndio inathibitisha kwamba Kenya Kuna rushwa, 50% ya bajeti ya Kenya huushia mifukoni mwa politicians.
Tzn kuna udokozi,kujifuta kwenye maamuzi ila hakunaga rushwa.Rushwa na ufisadi uko Kenya na Nigeria huko
 
Kenya na Tanzania huwa tunareport quarterly Gdp figures miezi mitatu baadaye wakati South Africa, UK, USA na nchi zingine zilizoendelea huripoti mwezi mmoja baadaye. Kwa mfano Gdp data ya October-December 2021, utakuta South Afrika, UK na nchi za ulaya zitairipoti mwishoni mwa Januari 2022 wakati Kenya na Tanzania na nchi za Afrika zitaripoti mwisho wa machi au Aprili 2022. Tunachukua miezi mitatu au minne kuripoti kitu ambacho kinachukua nchi za ulaya mwezi mmoja tu kuripoti.

Unajua kwa nini inakuwa hivyo!!? Apart from the policy, but their system of doing things is in a well defined fashion. That is, almost all businesses are registered, this renders to all transactions to be recorded. Unlike our economies, which have a lot of unregistered businesses/enterprises that triggers to a lot of transactions go unrecorded.
 
sijapenda sana hio greenery on columns, wange iwacha tu hio concrete jinsi ilivyo
download (5) (1) (1).jpeg
 
Bado napenda Tanzania na bado naamini uchumi wenu upo under-valued. Nimesema hivyo kwa muda mrefu sasa kwamba kulingana na miradi mingi inayoendelea Tanzania na kwamba mnaeexport chakula ukanda wote huu na munauza dhahabu ya $3 billion kwa mwaka, uchumi wenu haustahili kuwa mdogo hivyo. Gdp yenu inastahili kuwa mkubwa kushinda hio $70 billion ambayo serikali huwa inataja. Halafu mumekwama hapo kwa $60-70 billion kwa miaka mitano au sita sasa japo uchumi wenu unakuwa kwa asilimia 5 au 6% kila mwaka. Licha ya kurebase uchumi wenu mwaka wa 2014 na 2019 bado uchumi wenu umekwama pale pale. Tatizo liko wapi ikiwa nchi kama Ethiopia ambalo lina a more primitive economy linashinda uchumi wenu kwa ukubwa? Mimi huwa ninashuku Tanzania bureau of statistics haina ujuzi unaofaa na wanahitaji msaada kutoka nje ili waweze kupima ukubwa wa uchumi wenu vizuri.

Kuna uwezekano wameshindwa kuzingatia sector mpya zinazoingia kwenye uchumi wenu kwa mfano boda boda wa pikipiki wamekuwa wengi sana miaka mitano zilizopita hapa Africa mashariki, hii lazima izingatiwe kwenye kucalculate mapato ya nchi kama sub-sector mpya ya transportation and logistics. Na mambo ya internet nayo imechipuza biashara mpya kama ya kuuza na kuchuuza bidhaa kupitia mtandao. Halafu miradi mikubwa kama JNHPP ambayo ni takriban $2.5 billion na SGR yenu ambayo ni zaidi ya $4 billion, unaweza imagine kama ni cement au vyuma vinanunuliwa ndani ya nchi basi ni cement ngapi zinanunuliwa hapo? Miradi za daraja ni cement ngapi zinanunuliwa hapo? Ni watu wangapi wanapokea mishahara wanaofanya kazi kwenye miradi hii? Yaani itakuwaje uchumi wenu umekwama kwenye $60 billion kwa miaka mitano? Haiwezekani, lazima kuna tatizo mahali.

Mimi huwa naona uchumi wenu umekaribia wetu na unastahili kuwa around $90 billion. Lakini hio ni maoni yangu tu kwa sababu sijakaa chini na kupitia ripoti ya gdp yenu kwa undani kama nilivyofanya ya Kenya. By the way, Imf wana kitengo maalum ya kusaidia nchi masikini kuboresha statistical reporting capacity zao. Nchi nyingi za Africa zipo hovyo sana katika kupima ukubwa wa uchumi zao. Kuna nchi za central Afrika ambazo hazijawahi kurebase uchumi zao kwa zaidi ya miaka ishirini. Nchi nyingi za Afrika zipo hovyo sana kwenye suala hili. Inawezekana Kenya tunabahatika kupata training na maarifa kutoka Imf na World Bank kwa maana taasisi hizi zina regional headquarters hapa Nairobi. Halafu Kenya sisi tunapenda kujipendekeza kwa wazungu so unakuta Wafanyikazi wa KNBS wanapata training kila wakati jinsi ya kupima na kuclassify different sectors za uchumi. Wafanyakazi wa KNBS huwa wanakwenda hadi ulaya kupata trainings kila uchao kwenye masuala ya kumeasure, kuclassify na kureport different sectors za uchumi. Tieni bidii kidogo kwenye hili. Nchi kama ya South Afrika ipo mbele sana kwenye suala hili kiasi cha kwamba wao hurebase uchumi wao kila baada ya mwaka mmoja badala ya kila baada ya miaka mitano kama tunavyofanya Kenya na Tanzania. South Afrika wao wanarebase kila mwaka kwa sababu wana pesa na ujuzi na wataalam wa kutosha.
big up ,umenena mzee

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom