Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,486
7,928
Mhandisi Ezra Chiwelesa amewasilisha azimio la Bunge kumpongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu kwa kuimarisha demokrasia nchini na kuimarisha diplomasia ya Uchumi.

Mhandisi Ezra pia amemshukuru Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson kwa kuruhusu na kumpa fursa ya kuwasilisha hoja ya azimio.

Mhandisi amesema mambo muhimu yaliyochangia kuimarisha demokrasia ni
  1. Uamuzi wa kuruhusu shughuli za siasa hasa mikutano ya hadhara
  2. Kuanzisha vikao vya maridhiano ya kisiasa miongoni mwa vyama vya kisiasa nchini
  3. Marekebisho ya kimfumona kisheria yanayoongoza shughuli za kisiasa
  4. Kuundwa kikosi kazi masuala yanayohusu demokrasia
Hoja imeungwa mkono kwa kishindo na kinachoendelea kwa sasa ni wabunge wanaendelea kutoa hoja zao kumsifu Rais Samia.
 
Mhandisi Ezra Chiwelesa amewasilisha azimio la Bunge kumpongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu kwa kuimarisha demokrasia nchini na kuimarisha diplomasia ya Uchumi...
Namuona mbunge EZRA CHIWELESA wa Biharamulo kufika mbali sana kisiasa hapa nchni

USSR
 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa Kumi na Moja, Kikao cha Kwanza, tarehe 04 Aprili, 2023, limeazimia kwa dhati na kauli moja:

(a) Kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuimarisha Demokrasia nchini;

(b) Kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukuza Diplomasia ya Uchumi; na

(c) Kumuunga mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika majukumu yake ya kazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumuombea afya njema, baraka na ulinzi wa Mwenyezi Mungu katika kutekeleza majukumu yake.
8DA512BE-425E-4A36-877F-40E6E8D6B5B0.jpeg
87AC4BA7-3E80-4C02-973F-37BDAB64251B.jpeg
2A501272-9913-46B1-90D8-EC7AD598E44E.jpeg
CC55A660-3532-4129-A6D1-E8B8AD920D6C.jpeg
6F1B0A66-05BE-414F-B838-0AFE21CCCFEF.jpeg
 
Mhandisi Ezra Chiwelesa amewasilisha azimio la Bunge kumpongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu kwa kuimarisha demokrasia nchini na kuimarisha diplomasia ya Uchumi...
Kuna haja ya kutoa maana rasmi tena/ definition rasmi ya demokrasia na haki za binadamu ili kujitenga na demokrasia/haki za binadamu za kimagharibi zinazolazimisha kuingiza masuala ya ushoga kama sehemu ya demokrasia na haki za binadamu!

Demokrasia si uhuru wa kufanya unavyotaka bila kujali athari ya kile unachotaka kwa jamii unayoishi, na haki za binadamu hazipaswi kuingilia haki za binadamu wengine kwenye jamii!

Vinginevyo Marekani watakenua meno na kudhani kuwa malengo ya makamu wa marekani kutembelea Tanzania yamefanikiwa kwa maana ya kushinikiza demokrasia yao!!
 
Mnampongeza kwa mambo aliyofanya ambayo yapo kikatiba? Aliapa kufanya hivyo sasa ccm wanashangaa nini?
Kwa hiyo pia mtu akisimama hadharani ni kutoa Azimio la kutaka ashutumiwe kwa kusimamia vyema ;
*Watumishi kuiba fedha za umma
*Mfumuko wa bei wa kutisha
*kushindwa kutoa maslahi bora ya watumishi na wastaafu nk.
Jee itakubalika?
Hii tabia ya nchi kuendeshwa kiupambe upambe inatia aibu sana! Tuiache.
 
Ukipita airport kuna matangazo ya kiswahili ya kumpingeza mama, sijui yanamlenga nani
Ujinga mwingi sana kabla tutangaze bidhaa zetu hata wageni wakija wazione kwenye mabango watu wamejaaa uchawa na Mama nae alikemee hili . mabango sehem kubwa yamejaaa yy kwani hii nchi hatuna hata mbuga za wanyama.
 
... na watuambie ni lini na nani alizorotesha demokrasia nchini. Tatizo tunapenda kuzunguka badala ya ku-hit kiini cha tatizo ili lisijirudie tena.
 
Bunge la Tanzania limepitisha azimio la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuimarisha demokrasia, utawala bora na kukuza diplomasia ya kiuchumi.

Hoja hiyo ya azimio hilo iliwasilishwa na Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Ezra Chiwelesa leo Januari 4, 2023

Baadhi ya Wabunge ambao wamezungumzia mafanikio hayo kwenye maeneo hayo wamesema
"Katika kipindi cha miaka miwili rais ameonyesha wazi dhamira yake kusimamia misingi ya haki za binadamu na utawala bora, demokrasia pamoja na diplomasia ya uchumi. Nampongeza kwa kuruhusu mikutano ya hadhara na kufungulia vyombo vya habari-Mbunge Viti Maalum, Neema Lugangira.

Pia Mbunge wa Simanjiro, Christopher Olesendeka, amepitisha azimio la Bunge la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan “ameimarisha demokrasia, utawala bora na diplomasia ya kiuchumi, haya anayafanya kwa kuzingatia mahitaji ya pande zote za muungano sababu yeye ni mtu wa haki. Haki na usawa viokishamiri katika jamii undugu hujengeka, maovu hujitenga.”

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (Chadema), Aida Khenani, amewataka wabunge wa CCM kuacha unafiki ili wamsaidie Rais Samia Suluhu Hassan, kutekeleza majukumu yake “Naunga mkono azimio la kumpongeza Rais endapo Bunge tutamsaidia, tukikaa kwenye unafiki hatumsaidii Rais"

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kujadili wizi na ripoti za maelfu ya pesa wao wanajikita kwenye vitu vyepesi. Hilo Azimio ndio litashusha bei ya Maharage?
 
Kwenye hilo azimio wachangiaji wa hoja baadhi yao wakaanza kuwasulubu wabadhirifu wa fedha za umma kabla ya ripoti ya CAG haijawa wazi kwa wananchi.

Wachangiaji tayari wameanza kuwaonesha mlango wa kutokea wabadhirifu na kuwaweka matumbo joto
 
Back
Top Bottom