Companero,

Ahsante kwa kuleta maana ya majina ya sehemu za huko Katesh. Tumefahamu kianzia (prefix) "Basod" ni ziwa. Tuambie na maana ya Katesh (sahihi Qatesh) na Hanang (Anang') pengine Dr. Mary Nagu, Mbunge wa Katesh ambaye ni multilinguist atakusaidia.
 
Mwanazuoni tafsiri hii ina tofauti gani na ya ule mji wa Brunei Darusalaam?

Hicho cheo ni kikubwa kuliko nilivyo, Mkuu!

Kwa kweli sijatoa tafsiri, bali nimejaribu kuelezea tu matumizi ya kiambata "al".

Km nimekuelewa vema, DaruSsalaam ndio matamshi halisi ya Kiarabu; Dar Es Salaam ni mnyumbulisho tu wa DaruSsalaam.
 
Asanteni sana ndugu zang kwa ufafanuzi murua wa majina ya maeneo.
Je mshawahi kudodosa kuhusu 'KAWE' ?
Jina Kawe linatokana na jina la kiingereza "Cow way". hii ilikuwa ni njia ya ng'ombe waliokuwa wanapelekwa pale kiwanda cha nyama cha Tanganyika Packers ambacho kipo eneo hilo. Hivyo Waswahili wakaita KAWE badala ya "COW WAY" mpo hapo?
 
Na jina Tanzania limetokana na Nini? Kuna siku nilipata kusikia kuwa ni muunganisho wa maneno ya mwanzo ya nchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar. Lakini nalo Zanzibar limetokana na nini, kwani kule ni kuna visiwa vikuu viwili vya Unguja na Pemba?
 
Ilikuwa kama mtumwa hajatoroka njia zima mpaka kufika panapoitwa sasa bagamoyo ilikuwa ngoma anaambiwa "bwaga moyo" kama vile usijepe moyo tena wa kutoroka.

Kuhusu kariakoo alikogwa jogoo pale alipata nafasi ya kutoa sauti/ukelele mara moja tu "koo".Kwa hiyo watu wakawa wanasema karia koo karia koo karia koo wakimaanisha jogoo.Hivyo wana refer pale alipo gongwa jogoo karia koo.(toka vikao vya kahawa isikupe taabu kuibishia )
 
Babati = Baba huyu hapa. Tunaambiwa kwamba ilitokana na mzungu alifika nyumbani kwa mwenyeji. Akamkuta baba amelala na mtoto akiwa hapo karibu na alipomwuliza hapo palikuwa ni wapi, mtoto akajibu huku akimwashiria baba yake "Baba huyu hapa" ili ikiwa katika jinsia ya kike/kike (neuter/feminine gender) kwa vile watoto wanapojifunza lugha huwa hawatofautishi jinsia hizo, kwani baba angekuwa katika masculine gender.
 
Na jina Tanzania limetokana na Nini? Kuna siku nilipata kusikia kuwa ni muunganisho wa maneno ya mwanzo ya nchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar. Lakini nalo Zanzibar limetokana na nini, kwani kule ni kuna visiwa vikuu viwili vya Unguja na Pemba?

Ni kweli kwamba TanZania ni muungano wa majina ya Tanganyika na Zanzibar.
Binafsi nina hamu sana ya kujua maana ya jina lanchi yangu....

Tanganyika?
Labda lina uhusiano na ziwa Tanganyika (ambalo laweza kuwa ni jina lilitokana na samaki fulani wapatikao ziwani humo)...
Zanzibar
Niko kizani.......Labda Kibunango atusaidie
 
Yah man, kama ulivyosema, nadhani Kibunango ana historia nzuri zaidi ya jina hili. Ila nilivyosoma katika historia, jina Zanzibar linatokana na "ZENJ BAR" ama dola ya Zenj. Sasa sijajua kuwa nani alitohoa kuwa ZANZIBAR.
 
Ni kweli kwamba TanZania ni muungano wa majina ya Tanganyika na Zanzibar.
Binafsi nina hamu sana ya kujua maana ya jina lanchi yangu....

Tanganyika?
Labda lina uhusiano na ziwa Tanganyika (ambalo laweza kuwa ni jina lilitokana na samaki fulani wapatikao ziwani humo)...
Zanzibar
Niko kizani.......Labda Kibunango atusaidie
Zanzibar limetokana na lugha ya kiarabu "Zayn Z'al Barr" ikiwa na maana ya "Fair is this land"
 
Zanzibar limetokana na lugha ya kiarabu "Zayn Z'al Barr" ikiwa na maana ya "Fair is this land"

Mkuu Kibunango thanx,
Now where is the Zenj coming from? As it is in the link in your signature.
 
Kuna mwenyeji mmoja wa Kigoma aliwahi kuniambia kuwa ktkt ziwa Tanganyika kuna samaki wawili mashuhuri sana ambao kwa kiha wanaitwa "Itanga" na "Nyika". Mmoja wao inasemekana ana umeme mkali.

K/hiyo, huenda neno "Tanganyika" limetokana na majina ya samaki hao.

Zanzibar limetokana na lugha ya kiarabu "Zayn Z'al Barr" ikiwa na maana ya "Fair is this land"

Huu muungano umeekaaje wakuu (kama maana za Tanganyika na Zanzibar ni hizi)....'Lake Tanganyika fishes' combined with 'fair land' and we got Tanzania.
 
Kariakoo ilitokana na sentensi ya kizungu enzi hizo. Pale ilikuwa nisehemu ya kufanyia manunuzi ya bidhaa toka kwa wakulima.Kumbuka wakulima wa pwani hawakuruhusiwa kuvuka Anatoglo. Hivyo vijakazi wa wazungu na wahindi walitumwa pale ilipo kariakoo kuchukua/kununua bidhaa za shambani Ikawa CARRY AND GO, waswahili wakashindwa kutamka maneno hayo vizuri basi wakaishia kusema kariakoo badala ya carry and go. Sehemu kabla ya kubadilishwa wenyewe waliita tua tugawane. Kama kuna historia sahihi basi iletwe hapa.
Mkuu Malila sidhani kama Kariakoo ilitokana na CARRY AND GO!
KARIAKOO ilitokana na neno CARRIER CORPS ambayo ilikuwa ni kombania ya wapagazi wa kiafrika wakati wa vita kuu ya pili.Makao yao yalikuwa hapo ilipo Kariakoo.
Na ndio maana ukuenda Nairobi vilevile kuna sehemu hiyo waliyokaa hao CARRIER CORPS.
 
Mkuu Kibunango thanx,
Now where is the Zenj coming from? As it is in the link in your signature.
Zenj ni mambo ya vijana wa miaka ile ya themanini walipoamua kufupisha jina zima la Zanzibar na kuibuka na Zenj...
 
Tukuyu
Nilivyosikia historia, ni kwamba eneo hilo ilikuwa ni eneo la watu kukutana (kama mnada vile) na palikuwa na miti ya mikuyu (sycamore) ambayo ilikuwa haikui. Sasa wenyeji wakwa wanaita hiyo miti ya mikuyu isiyokua, "Tukuyu" kwa sababu "Hatukui".

Mkuu Idmi Tukuyu ninayo ifahamu mimi inatokana kweli na miti ya mikuyu, kama ulivyoelezea vizuri.Hata hivyo jina la mji wa Tukuyu ina tokana na hiyo hiyo miti ya Mikuyu ambayo Kinyakyusa inaitwa Mikuju, Tukuyu hadi leo kwa mwenyeji wa pale inaitwa TUKUJU kutokana na asili ya miti hiyo.
 
DSC_5689.JPGtt.JPG

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA SHADYA KARUME AKISALIMIANA NA WANAFUNZI WA SKULI YA MSINGI YA UZINI WAKATI KALIPOWEKA JIWE LA MSINGI LA SKULI YA MAANDALIZI YA TUNDUNI WILAYA YA KATI KUSINI UNGUJA LEO

DSC_5638.JPG

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI NA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA ZAYEDESA MAMA SHADYA KARUME AKIONDOSHA KIPAZIA KUASHIRIA KUIZINDUWA RASMNI SKULI YA MAANDALIZI YA CHEKECHEA TUNDUNI UZINI JANA

DSC_5649%5B1%5D.JPG

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MAMA SHADYA KARUME AKLIPANDA MNAZI BAADA YA KUIFUNGUWA SKULI YA MAANDALIZI WA WATOTO KATIKA KIJIJI CHA TUNDUNI UZINI WILAYA YA KATI JANA. PICHA NA OTHMAN MAULID WA ZANZIBAR LEO

Chanzo: Michuzi Blog
 
Last edited:
I doubt if this history is correct. Is 'Daru salaam' also arabic? Dar es Salaam is arabic for a safe habour Bandari (dar) ya(es) Salama (Salaam). By then most of the hobours along the indian coast were not safe for arab merchants.
Duh, mkuu SMU. Hivi na Kariakoo maanake nini?
 
I doubt if this history is correct. Is 'Daru salaam' also arabic? Dar es Salaam is arabic for a safe habour Bandari (dar) ya(es) Salama (Salaam). By then most of the hobours along the indian coast were not safe for arab merchants.

Yupi ni sahihi, angalieni msitumie hii thread kutupotosha maana naona mnaanza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom