3.KOLOMIJE[BUNDA].
Inasemekana mahali hapo alifika Mzungu aliyeitwa James.Yule Mzungu akataka watu wamwiite 'J' badala ya kutamka jina lote. Hivyo akawaambia CALL ME J, wabantu wakatamka KOLOMIJE na kutengeneza jina la lile eneo.
N:B SOURCE yake ni HEARSAY STORIES....unaweza kusahihisha ama kuongeza majina mengine.
Huku kolomije ndipo mkuu wa mkoa wa dar anapotokea?
 
1 Nimesikia baadhi ya watu kusema Mlima Kilimanjaro ni jina la kizungu (wageni). Naomba niwaelimishe kwa sehemu tu. Jina la Mlima Kilimanjaro lilitokana na neno la kichaga lililosema - Kilema Kyarwa ikimaanisha Mlima wa Ajabu/ Mlima wa Mungu, kutokana na Volikano iliyo kuwa inatoka. hayo mapokeo wageni walishindwa kuyatamka vema na kuanza kuita Kilimanjaro.
2 Asili ya jina Mbeya wengine husema wahindi walishindwa kusema neno chunvi kwa kisafwa yaani Iv'eya. Mimi nasema asili ya jina la Mbeya ilitokana na chifu aliyewahi kutawala eneo hilo ambaye aliitwa chifu Mbeye, katika kutamka waka wageni wanaanza kuingia kwenye nchi ya chifu Mbeye ndio wakaanza kusema Mbeya mpaka leo. Lakini binafsi sijajua mpaka leo kaburi la huyo chifu alizikwa wapi au ndiyo huko mbeya mlimani sijui. hebu nipanueni hapo.
3 Kwa kifupi tu Mama John amezalisha majina yafuatayo jiji la Mbeya:- Sinde, Makungulu, Mwanjerwa, na Mama John. = Makungulu ndipo alipokuwa anaishi alitunza miti ambayo kungulu walikuwa wanalala kwa wingi. Sinde - aliweka kilabu cha pombe ya kienyeji na wateja wake walikuwa wanakaa kwenye vitita vya nyasi kama viti kwa kisafwa vitata hivyo vinaitwa INSINDE. mji ulipoanza kupanuka kilabu hicho kilipitiwa na ramani ya barabara ya sokomatola mwanjelwa na kumsababishia kuhamisha kilabu hicho eneo jipya yaani MAMA JOHN - mpakaleo hiyo mama John. na mwanae aliyeitwa jina lake Mwanjelwa ndiye alijenga nyumba yake hapo mwanjelwa na baadaye eneo hilo likabaki kwa jina la Mwanaye MWANJELWA mpaka leo. Karibuni wana historia kudadavua
 
Mji wa Shinyanga ulitokana na jina la mti ujulikanao kama mbono kaburi, kwa kisukuma huitwa "inyanga".
Ka hiyo kulikuwa na mti huo eneo hilo kama kituo cha wachuuzi.
Kituo hicho kikawa kinaitwa "hinyanga" kwa kisukuma. Tafsiri yake ni " kwenye mbono"
Kwa Tabora, eneo la Kazehill ulipoanzia mji wa Tbr kulikuwa na soko la viazi vilivyochemshwa na kukaushwa, kwa kinyamwezi viazi hivyo huitwa matobolwa au nhobholwa.
Hadi leo mji huu kwa kinyamwezi huitwa "nhobholah" ndiyo Tabora. Matamshi haya yaliletwa na wageni
Nihivyo tu.
Karibuni wanahistoria 'tushee'.
 
Wakuu habari za muda huu na poleni pia kwa uchovu wa kazi za kutwa.

Wakuu bila kupoteza muda nije moja kwa moja kwenye mada,
Naomba wanajamvi mnisaidie kufahamu asili Nyegezi na Makunduchi kupewa hayo majina pia historia hasa ya hayo majina ni ipi,
kila nikisikia hayo majina natamani kuijua chanzo hasa cha hayo majina , wale wanajua historia yake tupia neno hapa .
Asanteni naamini nitapata darasa na ushirikiano mzuri hapa.
 
Makunduchi ipo Zanzibar iro jina linatokana na wavuvi enzi ya utawara wa kisultwani walikuwa wakipenda sana kuanika nyavu zao na kuzishona huku wakiwa wamevaaa misuri ire rain a wengine mapajama mithiri ya mwanamke aliye vaa khanga moko unajuwa msuri ukirowa na zire nyavu zina maji maji inaperekea misuri kuwavuka na walikuwa awajari at a ikiwavuka wanaendelea na kazi yao kwaiyo mahala pare pakaitwa makunduchi
 
R na L ni tatizo.... ila poa tu, nmekuelewa!!!
 
Makunduchi ipo Zanzibar iro jina linatokana na wavuvi enzi ya utawara wa kisultwani walikuwa wakipenda sana kuanika nyavu zao na kuzishona huku wakiwa wamevaaa misuri ire rain a wengine mapajama mithiri ya mwanamke aliye vaa khanga moko unajuwa msuri ukirowa na zire nyavu zina maji maji inaperekea misuri kuwavuka na walikuwa awajari at a ikiwavuka wanaendelea na kazi yao kwaiyo mahala pare pakaitwa makunduchi
Mkuu matumizi ya R na L yanakusumbua tafuta mwalimu tena wa kiswahili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom