Kijiji cha Soliwaya- Njombe kuna eneo wanaliita Karasha, ni eneo ambalo wajenzi wa barabara huvunjia mawe. Na hiyo Karasha imetokana na neno Crusher, wabena na baadhi ya wachina kutamka ikawa ishu wakarahisisha hivyo.
 
Kijiji cha Soliwaya- Njombe kuna eneo wanaliita Karasha, ni eneo ambalo wajenzi wa barabara huvunjia mawe. Na hiyo Karasha imetokana na neno Crusher, wabena na baadhi ya wachina kutamka ikawa ishu wakarahisisha hivyo.
Isoliwaya ipi, ya njia ya Makete au ile karibu na Matembwe Lupembe?
 
MUSOMA limetokana na neno OMUSOMA kwa Lugha ya Wenyeji Wakwaya/ ajita na Waruli kwa Maana ya Sehemu ya Nchi Kavu iliyochongoka na kuingia Majini/ Ziwa Victoria.
 
Kijiji cha Soliwaya- Njombe kuna eneo wanaliita Karasha, ni eneo ambalo wajenzi wa barabara huvunjia mawe. Na hiyo Karasha imetokana na neno Crusher, wabena na baadhi ya wachina kutamka ikawa ishu wakarahisisha hivyo.
hii ya "KARASHA" ipo maeneo mengi. Ukitoka Mlowo Mbozi, mkoani Songwe, kama unaenda Tunduma, kuna eneo ambalo kuna kiwanda cha kubonda mawe ili kutengeneza kokoto (crusher), panaitwa KARASHA.
 
I doubt if this history is correct. Is 'Daru salaam' also arabic? Dar es Salaam is arabic for a safe habour Bandari (dar) ya(es) Salama (Salaam). By then most of the hobours along the indian coast were not safe for arab merchants.
That is what we were told at school in those days and that is what it is.
 
Wajuzi wa historia,
Maranying majina ya sehemu huhusishwa na maana ya lilipo eneo, mgunduzi wake au mtu maarufu, au kitu cha ki historia kilichowahi kutokea hapo. Kwa mikoa yetu ya Tanzania, wilaya na miji mbali mbali, nini asili ya jina lake?
Naombeni kwa kila anayejua a comment kwa jina na asili yake. Itasaidia wengi kujua maana ya hayo majina. Karibuni.
 
Nilipata simuliwa kuhusu kijiji chetu cha KANTARE, kwamba zamani kijiji kile kilikuwa na SIMBA ambaye kwa kihaya anaitwa NTARE, hivo kijiji kile kupewa jina la KANTARE. Kipo wilaya ya Misenyi,Bwanjai
 
Katerero
Screenshot from 2016-11-28 10:53:27.png
 
Duh, uzi wa siku nyingi huu! Inawezekana kuna wachangiaji wa huu uzi wamesharest in peace hapa! Live longer mliopo hai, R. I. P waliokufa. Shekilango=sheikh kilango. Kawe=car way.
Hivi umepata kujiuliza unapopita katika mitaa mbalimbali ya mjini Dar au mji mwingine wowote Tanzania, jina la mtaa au eneo husika limetokana na nini?

Kwa mfano, Kijito Nyama limetokana na nini? Au Mlalakuwa, Au Mtoni kwa Aziz Ali n.k, n.k. Labda utadhani imetokea tu ... just ipo ipo, hapana! Baadhi ya majina ya mitaa yana historia ndefu na yenye kukumbukwa hata kwa vizazi vijavyo.

Hapa napenda kuwahabarisha maana ya mtaa au eneo la nje kidogo ya jiji la Dar liitwalo Gongo la Mboto.Jina hili limetokana na nini? Nakumbuka nilipata kusimuliwa na mwalimu wangu mmoja miaka ile pale Tambaza Sekondari nikiwa kidato cha pili.

Alisema palikuwa na mzee mmoja mashuhuri ambaye alipata kuishi katika eneo hilo.Huyu jamaa alikuwa mkulima. Jina lake aliitwa Mboto. Siku moja alijilawa kwenda katika konde lake kwa ajili ya kujipatia riziki.

Wakati ule, maeneo yale yalikuwa na giza la mapori na vichaka kadhaa. Jioni yake asirudi nyumbani. Kesho yake hadi mchana Mboto haonekani.

Mbiu ikapigwa watu wakakusanyika,kilichofuata ni msako mkali wa kumtafuta mzee huyu.Baada ya siku kadhaa wakakuta nyayo za mnyama mkubwa mithili ya Simba na ishara ya purukushani kadhaa.

Walipochunguza zaidi wakafanikiwa kukuta Gongo ambalo alipenda kutembea nalo mzee huyu.Wakahisi kuwa Mboto huenda amekutwa na maafa ya kuliwa na Simba. Walichokiona pale ni Gongo lake,Ndipo hilo eneo hadi leo lajulikana kama Gongo la Mboto.

Tuhabarishane maana ya maneno mengine kama Msasani, Mikocheni,Mto wa Mbu n.k.
 
Back
Top Bottom