Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 11,252
- 24,089
Binafisi mimi nimetokea kwenye familia ya wafugaji wa mifugo karibia yote yaani mbuzi,kondoo na hata ng'ombe .
kipindi tukiwa tunachunga ilikuwa ni fahari sana kulisha mazao ya wakulima tena ikitokea mkalisha na msionwe au kukutwa mtajipongeza kweli.
Ukweli usiosemwa ukisikia vita ya wakulima na wafugaji jua tu mchokozi ni mfugaji kwa 97%.
Hii video ukiangalia vizuri ni zaidi ya ng'ombe ya 40 wanachungia kwenye mahindi ya mkulima imagine umelima kwa gharama kubwa then unafika shamba unakuta yameliwa yote na mifugo.
Bahati mbaya sana ukienda kudai haki yako utapewa kiasi kidogo tu maana wafugaji huwa wako karibu sana na ma bwana shamba na viongozi wengine kwa kuwapa maziwa na kuwalimia bure mashamba yao.
Hivyo viongozi wanakuwa hawana meno kabisa kuhukumu kwa haki.
Matokeo yake ndo haya mkulima ananunua asali hata lita3 tu anapaka paka kwenye mazao yake ili ng'ombe akila habari ya uzima inaishia hapo!
Wengine hupulizia sumu pia.
Je wewe utahukumuje hii kesi?