philltaya
Member
- Sep 5, 2015
- 53
- 11
Mh. Mkuu wa Wilaya mnatuhamasisha kulima ili kuepuka njaa na kujipatia kipato lakini hakuna haki kwa mkulima ila kinachoonekana mfugaji ndiyo mwenye haki. Au sheria inamsimamia mfugaji pekee? Wanapata wapi ujasili wa kuingiza mifugo kwenye shamba la mkulima, hiko kiburi anatoa wapi?
Kama unasoma ujumbe huu hii ni mara ya pili mimi binafsi kukuandikia katika ukurasa huu lakini inaoneka hakuna jitihada za kulimaliza hili. Shamba langu la heka sita mazao yote ya mahindi yameliwa na ng'ombe, kwanini hamko tayari kuwadhibiti wafugaji katika maeneo ya wakulima?
Mimi ni mkulima kijiji cha Menge kitongoji cha Vianzi