tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Waziri Nape Nnauye awateua Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Machi 21, 2024

    UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) Tarehe 21 Machi, 2024 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb) kwa Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 7 (3) cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003...
  2. Mkoba wa Mama

    JamiiForums Tanzania TCRA waichunguze kampuni ya simu za mkononi ya Halotel

    Mtandao wa Halotel umekuwa na tabia ya kukata salio la muda wa maongezi mara tu unapoongeza salio. Hii imenitokea zaidi ya mara tatu sasa, na nikipiga simu huduma kwa wateja naambiwa kuna huduma nimejiunga inayokata salio hilo, wakati hakuna huduma yoyote ambayo mimi nimejiunga. Mbaya zaidi...
  3. tpaul

    JamiiForums Tanzania TCRA na TCU wachukue hatua kali kwa Wasafi TV kutokana na 'kiki' ya mapacha kufanyiana mtihani

    Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Kuna hiki kipande cha video kinachobamba mtandaoni kuhusu mapacha wawili ‘wanaokiri’ hadhrani kufanyiani mtihani ‘chuoni’. Ukisikiliza kwa makini na kwa utulivu wa hali ya juu, utagundua kuwa hawa watu wanaigiza tu. Haiingii akilini watu...
  4. hp4510

    JamiiForums Tanzania Serikali na TCRA chukueni hatua kampuni ya Flex cash

    Wangudu Leo nikiwa kwenye feri natoka kigamboni kwenda mjini, nilikaa karibu na ndugu mmoja alikuwa busy kuongea na simu Baada ya muda kidogo nikaona anakosa nguvu kama anataka kuzimia, anatokwa na jasho Sana, Ikabidi kwenda kumsaidia na kumuuliza shida ya mkasa uliompata Kumbe bwana ana...
  5. Chizi Maarifa

    JamiiForums Tanzania Kwa jambo hili niliwaunga Mkono TCRA . Nchi hii wenye akili ni wachache sana

    Hakuna Mtangazaji mwenye akili anaweza ongea jambo kama hili. Tanesco wana matatizo yao na pengine ni ya kisiasa zaidi. Hakuna mtanzania mwenye akili timamu atapendezwa na suala hili la kukatika katika umeme. Lakini ni mtu mpumbavu tu anaweza fanyia mzaha jambo hili zito Kitaifa. Ni wakati sasa...
  6. snipa

    JamiiForums Tanzania Precision ya "Tuma kwenye namba hii" na Apps za Mikopo.

    Kuna Thread niliwahi zungumzia juu ya Apps hizi scam za Mikopo. Sasa Leo tujaribu kuangalia kwa upande wa matapeli wa tuma kwenye namba hii ambalo ni gang kubwa na wanafunikwa na kivuli Cha wakubwa. Kama nilivyowahi kueleza kuwa Apps za Mikopo kama vile PesaX, Msafi, Twiga Loans n.k hizi apps...
  7. P

    JamiiForums Tanzania Waziri Nape aruhusu magazeti kuendelea kusomwa kwa mbwembwe. Mpaka matamko yanakinzana huwa hakuna mawasiliano ndani ya wizara?

    Nimeona mjadala wa “Kusoma magazeti”. Nimeelekeza TCRA kuruhusu UBUNIFU kwenye tasnia ya Habari. Staili ya usomaji we magazeti imeongeza MVUTO kwenye usomaji huo, ni jambo linapaswa KUTIWA MOYO badala ya kuzuiwa. Waandishi endeleeni na ubunifu kwenye kusoma magazeti. Maelekezo mengine yeyote...
  8. Mjanja M1

    JamiiForums Tanzania TCRA: Hakuna kanuni inayokataza kusoma Magazeti kwa Mbwembwe

    Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Andrew Kisaka amesema kauli yake imepotoshwa kuhusu wasomaji wa Magazeti kwenye Redio akisema hakumaanisha usomaji wa mbwembwe bali wasomaji kusoma na kuingia ndani. Akizungumza leo asubuhi na Kipindi cha Good Morning cha...
  9. Mjanja M1

    JamiiForums Tanzania TCRA: Vyombo vya habari vinavyochanganya lugha kuchukuliwa hatua, ‘kuna haja ya kukiita kipindi Goodmorning?’

    Meneja huduma za Utangazaji, TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka amesema kuwa tabia ya vyombo vya habari kuruhusu watangazaji kuchanganya lugha kwenye vipindi vyao ni kosa kisheria na watachukuliwa hatua. 📹 TheChanzo Written by Mjanja M1 ✍️
  10. JanguKamaJangu

    JamiiForums Tanzania TCRA yazifungia Laini 21,000 zilizohusika kufanya utapeli

    ZAIDI ya laini 21,788 za mawasiliano ya simu zimefungiwa kupokea na kutoa mawasiliano kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kutumika kufanya uhalifu mtandaoni kwa kipindi cha miezi mitatu iliopita. Kwa mujibu wa ripoti ya mwenendo wa sekta ya mawasiliano iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa...
  11. J

    JamiiForums Tanzania TCRA imesema watumiaji wa internet wapo 35M

    TCRA Wametoa report ya Q2 inaonyesha watumiaji wapo 35M wa internet. Hii ni work force kubwa sana , na ni muda wa serikali kuwaza sasa kutengeneza ajira za mitandaoni nyingi sana. Ukosefu wa ajira za kawaida na ongezeko la watumiaji wa internet inaleta picha ya ama serikali itengeneze ajira...
  12. Mtini

    JamiiForums Tanzania TCRA imeshindwa kuwadhibiti matapeli wa mitandao? Au wanakula nao?

    Walipoleta utaratibu wa kusajiri kwa alama za vidole walituambia ni kwasababu ya kudhibiti matapeli, ila kadri siku zinavyoendelea ndivyo wanavyoongezeka. Je, mfumo ulikuwa wa upigaji umeshindwa kuwadhibiti? Au TCRA wanashirikiana na hawa wapigaji? Je, kwanini wasiweke utaratibu rahisi kabisa...
  13. snipa

    JamiiForums Tanzania Naomba TCRA mlinde taarifa zetu kwa apps zinazodai kutoa mikopo.

    Habari wanajukwaa natumaini mbuheri wa afya. Leo naomba nigusie japo kwa kiasi kuhusu hizi apps za mikopo ambazo kwa Sasa zimekuwa nyingi sana na promotion kubwa inafanyika huko YouTube. Nimeileta hii mada hapa kwenye jukwaa hili kwasababu hii mada sio ya kisiasa Bali kuweka wazi kwa...
  14. The Sheriff

    JamiiForums Tanzania TCRA yawataka Watanzania kutotumia huduma za mawasiliano ambazo hazijaidhinishwa na mamlaka hiyo

    Tamko linasema hivi: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuutaarifu Umma kuwa utoaji wa huduma za mawasiliano, zikiwemo huduma za usalama mtandaoni (cybersecurity services), intaneti, na vituo vya kutunzia data (data centres), katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na...
  15. Jamii Opportunities

    JamiiForums Tanzania Office Attendant at TCRA SACCOS Limited January, 2024

    Position: Office Attendant TCRA SACCOS Ltd is a registered Savings and Credit Cooperative Society whose main objective is to mobilize savings from members and I return provide credit facilities. TCRA SACCOS LTD is an employee-based Society which was established under the current governing...
  16. REJESHO HURU

    JamiiForums Tanzania TCRA mnawezaje kutoa mamlaka kwa kampuni kuingilia mawasiliano ya mtu?

    Bwana nape hii imekaaje kuna hizi tasisi za kukopesha mitandaoni zinaomba namba ya watu wa karibu wawili au watatu ajabu sasa mwisho wa siku wanatuma meseji kwa namba zako za sm zote ulizonazo kwenye sm yako na ambazo ukuwapa hapa mchawi nani. Kampuni ya sm au TCRA maana tumeshahisi hakuna...
  17. A

    JamiiForums Tanzania TCRA kwa nini hamzifungii hizi website au mna kazi za ajabu ajabu

    https://tanesco.tz.onrecruit.site/?m=1#1702207336312 Hawa watu mnaweza mka deal nao mara moja lakini mnafikiria mengine.....
  18. Ndagullachrles

    JamiiForums Tanzania TCRA sasa kutangaza masafa ya redio kwa zabuni

    MAMALAKA ya mawasiliano nchini(TCRA)imetangaza kuwa kuanzia sasa masafa ya radio yatashindaniwa kwa kutangazwa zabuni huku wadau wakitaka kuwepo na uwazi ili kuwa na uwanja sawa. Kwenye kikao cha wamiliki na maneja wa vituo vya radio pamoja na waandishi wa habari kilichokaa hivi karibuni...
  19. benzemah

    JamiiForums Tanzania Rais Samia ateua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kama ifuatavyo:- Amemteua Dkt. Jones A. Killimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano...
  20. Determinantor

    JamiiForums Tanzania Wafahamu Wajumbe wa Bodi ya TCRA iliyovunjwa

    Nasikia Rais kavunja Bodi ya TCRA. Naona hawa hapa ndio walikua Wajumbe wake MAWASILIANO: BODI YA TCRA YAVUNJWA Rais Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa ni takriban mwaka mmoja tangu amteue Mwenyekiti wa Bodi hiyo Kwa mujibu taarifa ya Kurugenzi...
Back
Top Bottom