Serikali na TCRA chukueni hatua kampuni ya Flex cash

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,451
6,325
Wangudu Leo nikiwa kwenye feri natoka kigamboni kwenda mjini, nilikaa karibu na ndugu mmoja alikuwa busy kuongea na simu

Baada ya muda kidogo nikaona anakosa nguvu kama anataka kuzimia, anatokwa na jasho Sana,

Ikabidi kwenda kumsaidia na kumuuliza shida ya mkasa uliompata

Kumbe bwana ana mkopo wa elf 92 kwenye kampuni ya flex cash na alitakiwa kurudisha huo mkopo kesho, sasa akapigiwa simu, na mwakilishi wa hiyo kampuni na akamwambia kama akilipa deni lake Leo ataongezewa laki tatu na atalipa kwa mwezi mmoja

Yule jamaa alichoamua ni kutumia balance ambayo alikuwa nayo kwenye simu yake alipe 92 apate laki tatu

Kilichotokea after kulipa ni hiyo laki tatu hajapata, hela aliyotoa ni balance yake ya matibabu na haitoshi tena

Presha ikapanda katolewa pale anapelekwa hospitali hana nguvu hata ya kutembea

Ombi langu Kwa serikali please please hata kama kuna wakubwa wanahisa kwenye hayo makampuni kuna Jambo linatakiwa kufanyika

Nadhani kunatakiwa mjadala wa Wadau na hao watoa huduma
 
Pole sana mkuu. Siku hizi hizi kampuni za mtandaoni hazina ethics wanasema lolote ili mradi wapate pesa yao maana mtanzania kukopa anakopa kulipa hataki.

Ila dawa ya mkopo ni kulipa aisee hakuna namna
 
Wangudu Leo nikiwa kwenye feri natoka kigamboni kwenda mjini, nilikaa karibu na ndugu mmoja alikuwa busy kuongea na simu...
Kama ulivyowadanganya wakakupa mkopo na wao wanawadanganya ili mulipe na hiyo ndio namna unaweza kusurvive kibiashara kwenye hii nchi la sivyo inakula kwako..
 
Pole sana mkuu. Siku hizi hizi kampuni za mtandaoni hazina ethics wanasema lolote ili mradi wapate pesa yao maana mtanzania kukopa anakopa kulipa hataki.
Ila dawa ya mkopo ni kulipa aisee hakuna namna

Sio mm, ila kwa maelezo ya huyo Mzee ni kuwa deni lake alitakiwa kulipa kesho na sio Leo that's means wamejipatia ela Kwa njia ya udanganyifu
 
Nadhani raia pia waache upumbavu wa kutaka hela za fasta. Benki sio wajinga kuweka vigezo lukuki ili wakupe mkopo. Halafu pia mkopo utoke 92k hadi 300k ni kitu kigumu sana.

Sasa sio kila mtu ana uelewa wa haraka wa namna hiyo
Kama ulivyowadanganya wakakupa mkopo na wao wanawadanganya ili mulipe na hiyo ndio namna unaweza kusurvive kibiashara kwenye hii nchi la sivyo inakula kwako..

upo sahihi sana bw. covid 19

Umeelewa mkasa mzima? Yule jamaa hadaiwi because muda wa kulipa bado
 
Back
Top Bottom