Precision ya "Tuma kwenye namba hii" na Apps za Mikopo.

snipa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
4,215
1,656
Kuna Thread niliwahi zungumzia juu ya Apps hizi scam za Mikopo.

Sasa Leo tujaribu kuangalia kwa upande wa matapeli wa tuma kwenye namba hii ambalo ni gang kubwa na wanafunikwa na kivuli Cha wakubwa.

Kama nilivyowahi kueleza kuwa
Apps za Mikopo kama vile PesaX, Msafi, Twiga Loans n.k hizi apps zinakusanya taarifa za watumiaji, hata kama hawajapewa mikopo.
Na watumiaji wamekuwa wakikubali permissions wanazoombwa na apps hizi, ikiwemo contact, calls, messages na storage access, kwahiyo data zikiwa on hizi apps Zina upload kwenye server zao taarifa za muhusika zote, ikiwemo calls, sms n.k

Sasa matapeli wanaojiita tuma kwenye namba hii Kuna namna wanaweza kuwa Wana access ya data kutoka kwenye hizi apps,
Mfano unapochat na mtu kuhusu kutumiana pesa hizi apps zinachukua taarifa na kuweza kufanya middlemen attack kwa kutumia namba nyingine ili tu utume pesa na wapite nazo.

Sasa Bado hatujui kama wamiliki wa hizi apps baadhi Yao ndio gang hii kubwa au ni watu gani,
Hivi Sasa kama mnavyoona baadhi Yao usipolipa deni wanatuma sms na upigia watu wako uliokuwa ukiwasiliana nao.

Sasa hebu imagine uhalifu wanaoufanya Hawa watu unavyoweza athiri watu kisaikolojia, Leo hii umewakopa elfu 50 afu wanamtumia sms mama yako mzazi kule kijijini kuwa wewe ni tapeli, mama yako atajiskia vipi si atahisi hata kidogo kitu ulichokuwa unatumia vyote ni wizi.

Bado Kuna haha ya TCRA kuwabana Hawa watu.

snipa
 
Moja ya sababu Android wanazidi kuondoa access ya Apps, app haziwezi kusoma SMS unless wapewe special permission na Google, pia storage ile ya zamani ambayo unapata storage yote inaondoka, inabidi uchague unawapa nini
 
Meseji za Aina hii zinawafikia hata wamiliki WA viswaswadu na ambao hawajawahi kupakuwa app za mikopo.

Wanachokifanya hao jamaa wanaweka namba nyingi randomly bila kumjua wanayetumia wanachofanya ni ku-guess, kama ni precision ya kujua MTU aliyetaka kutumia hela naamini ni ndogo Kwa 5% Ila kama wametuma Kwa watu 100,000 wanaweza wapata watu 5,000.

Kudhibiti hili tatizo makampuni ya simu hawana budi kuboresha software zao Kwa kuanza kutumia AI/ML za kudetect fraud/spam meseji kabla ya kumfikia MTU

Uzuri Wana data nyingi za meseji halisi na meseji za utapeli zenye ufanano na orijino, kama Wana miundo mbinu na watu sahihi(wataalamu) ni rahisi kutengeneza model ya kutambua SMS za kitapeli
 
Sms wanatuma kama bug hunters in a bulk or whatever, lakini now wanakuwa very targeted.
Kwasabu huko nyuma kipindi Cha TALA walitumia NGO lakini Sasa ni in personal mtu anakutarget kwasabu anakuwa updated na txt zako zote not to mention calls kupitia hizi apps.
 
Back
Top Bottom