Naomba TCRA mlinde taarifa zetu kwa apps zinazodai kutoa mikopo.

snipa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
4,215
1,656
Habari wanajukwaa natumaini mbuheri wa afya.

Leo naomba nigusie japo kwa kiasi kuhusu hizi apps za mikopo ambazo kwa Sasa zimekuwa nyingi sana na promotion kubwa inafanyika huko YouTube.

Nimeileta hii mada hapa kwenye jukwaa hili kwasababu hii mada sio ya kisiasa Bali kuweka wazi kwa watanzania wote ikiwa hii mada inagusa teknolojia.

Apps za mikopo zimekuwa nyingi na sizungumzii uwingi wa hizi apps Bali nagusia access ya hizi apps ambapo mtumiaji ili apate mkopo anatakiwa kukubali Terms and conditions.
Terms and conditions ambazo mtumiaji anatakiwa kuzikubali ni pamoja na kuruhusu access ya jumbe fupi ambazo anakuwa akitumiwa ikiwemo SMS, Contacts n.k

Kwa wasichokijua wengi hizi apps zinafanya analysis ya miamala ya kutuma/kupokea pesa ambayo ulikuwa unafanya ili kujipa uwezo wa wao kukupa mkopo,
Sasa ikiwa umeruhusu hizi apps ziwe na access ya taarifa zako za miamala Huwa pia Wana uwezo wakuangalia taarifa zisizohusiana na miamala, Je taarifa zisizohusiana na miamala wanazipeleka wapi, na hizi apps zipo audited au la ?

Je inakuaje kwa mtanzania asie elewa chochote kuhusu terms and conditions anazo zikubali ?
Na je inakuaje kama taarifa zinauzwa ili kuwezesha AI zifanye kazi kikamilifu n.k mbali na AI ?

Ombi langu ni kwamba hizi apps ziwe audited mana nimegusia technically Bado psychologically ikiwa watoa mikopo wanadai hata kwa namba zisizo rasmi, wanakupigia na wengine kukutisha.

TCRA naomba muangalie hili swala.

Ahsante snipa
 
Kuna makala ya BBC kuhusiana na athari za hizi apps za mikopo nchini India, iliangazia matumizi mabaya ya hizi ridhaa walizopatiwa kwenye simu za watu; ikiwa ni pamoja na kusoma sms, kuona orodha ya namba za watu kwenye simu yako na kufikia picha zilizopo kwenye Gallery.

Watu wamejiua, kupoteza ajira, kuathirika kisaikolojia n.k., kisa ya hizi apps nchini humo. Naona sasa muda si muda haya mambo yataanza na hapa.

Link ya documentary hiyo:
View: https://youtu.be/JilJhn_tP-c?si=6Frm17K6E_naILap

Naamini elimu ya kina itolewe kwa watu juu ya athari ya kuzipatia App hizi ruhusu ya kufikia taarifa zako nyeti za kwenye simu.
 
Habari wanajukwaa natumaini mbuheri wa afya.

Leo naomba nigusie japo kwa kiasi kuhusu hizi apps za mikopo ambazo kwa Sasa zimekuwa nyingi sana na promotion kubwa inafanyika huko YouTube.

Nimeileta hii mada hapa kwenye jukwaa hili kwasababu hii mada sio ya kisiasa Bali kuweka wazi kwa watanzania wote ikiwa hii mada inagusa teknolojia.

Apps za mikopo zimekuwa nyingi na sizungumzii uwingi wa hizi apps Bali nagusia access ya hizi apps ambapo mtumiaji ili apate mkopo anatakiwa kukubali Terms and conditions.
Terms and conditions ambazo mtumiaji anatakiwa kuzikubali ni pamoja na kuruhusu access ya jumbe fupi ambazo anakuwa akitumiwa ikiwemo SMS, Contacts n.k

Kwa wasichokijua wengi hizi apps zinafanya analysis ya miamala ya kutuma/kupokea pesa ambayo ulikuwa unafanya ili kujipa uwezo wa wao kukupa mkopo,
Sasa ikiwa umeruhusu hizi apps ziwe na access ya taarifa zako za miamala Huwa pia Wana uwezo wakuangalia taarifa zisizohusiana na miamala, Je taarifa zisizohusiana na miamala wanazipeleka wapi, na hizi apps zipo audited au la ?

Je inakuaje kwa mtanzania asie elewa chochote kuhusu terms and conditions anazo zikubali ?
Na je inakuaje kama taarifa zinauzwa ili kuwezesha AI zifanye kazi kikamilifu n.k mbali na AI ?

Ombi langu ni kwamba hizi apps ziwe audited mana nimegusia technically Bado psychologically ikiwa watoa mikopo wanadai hata kwa namba zisizo rasmi, wanakupigia na wengine kukutisha.

TCRA naomba muangalie hili swala.

Ahsante snipa
Hivi hii imekaaje kuna mshikaji katumiwa hii kwenye phone book contact zake zote.

HABARI NDUGU AMA JAMAA WAKARIBU WA XXXX XXXXXXX. MWENYE NO;0XXXXXXX. NI TAPELI AMEKOPA KIASI CHA SHILLINGI 105,900/= KUTOKA KAMPUNI YA PESA M LOAN NA ANATAKA KUTUTAPELI, UKIWA KAMA MTU WAKE WA KARIBU TUNAOMBA UMUAMBIE ALIPE DENI LAKE KABLA HATUJAANZA KUCHUKUA HATUA NYINGINE JUU YAKE.
 
Hawa jamaa wanandai nasubr watext contact tu
 
Hao jamaa ni matapeli haswaa, muhim ni kutulia hakuna kuwalipa mpaka waende mahakamani.
 
Back
Top Bottom