TCRA mmeshindwa kufuatilia uhuni unaofanywa na Vodacom upande wa M-Pesa?

JITU BANDIA

JF-Expert Member
Feb 5, 2023
2,683
6,036
Ni wiki ya pili sasa nimekuwa nikifuatilia hiki kitu kwa namba tofauti tofauti. Iko hivi:

Sasa hivi ukiweka pesa kwa wakala yeyote yule, iwe unamtumia mtu, ama unaweka kwako hautumiwi sms kuonesha ya kwamba umewekewa kiasi fulani, wala kwa mpokeaji!

Wakala anachoweza kukwambia ni kwamba angalia Salio lako. Ili ukatwe pesa pasipo sababu!

Huu ni uhuni unafanywa kwa makusudi na Vodacom Tanzania kuwaibia Wateja kwa kuwalazimisha wateja waangalie Salio wakatwe pesa pasipo sababu ya msingi.

Hawawazi kuhusu adha anayoipata mtu anaesafiri akitumia Mpesa akiwa sehemu ya kupata huduma kama chakula (kuchimba dawa!?), Mpaka akija kugundua si pengine gari imemuacha?

TCRA wanaangalia kama hawalioni hili!?

Kunilazimisha niangalie Salio kwa lazima, haikiuki mkataba wa Sheria ya huduma kwa mteja. Ni sahihi!?

Ni Wateja wangapi wanatumia hii Mpesa wanakumbana na hii adha ya kulazimishwa kukatwa hela ili kujihakikishia kiasi kilichowekwa na wakala kwa simu ya mhusika?

Kwa hizo wiki 2 Vodacom wameiba kiasi Gani kwa hii kitu? Tsh. 40 ×watu milioni 10 tu ni sawa na Tsh. 40,000,000,000.

Hii nchi aisee basi tu. Ni kwakuwa tu hakuna namna ya kuihama kabisa!
 
Voda wana mapungufu yao ila sio hilo. Hizo cases zinatokea mara chache sana.

Wanapinikera ni speed ya intanet tu, siku hz ipo chini sana. Nipo sehemu inasoma 4g lkn speed very low
 
Ni wiki ya pili sasa nimekuwa nikifuatilia hiki kitu kwa namba tofauti tofauti. Iko hivi:

Sasa hivi ukiweka pesa kwa wakala yeyote yule, iwe unamtumia mtu, ama unaweka kwako hautumiwi sms kuonesha ya kwamba umewekewa kiasi fulani, wala kwa mpokeaji...
Mkuu afadhali hata hao Vodacom. Kuna hawa wahuni wa kutoka Vietnam wanaitwa HALOTEL ni pasua kichwa kwenye wizi wa bando. Yaani hawa jamaa ni majizi sijapata kuona. Muda mfupi ujao, nitahamia tiGO.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Ni wiki ya pili sasa nimekuwa nikifuatilia hiki kitu kwa namba tofauti tofauti. Iko hivi:

Sasa hivi ukiweka pesa kwa wakala yeyote yule, iwe unamtumia mtu, ama unaweka kwako hautumiwi sms kuonesha ya kwamba umewekewa kiasi fulani, wala kwa mpokeaji...
Hiyo hesabu utajuwa umeikosea sio bure.
 
Umefanya utafiti Wa kutosha na je ni Kwa watu wangapi au ilo tatizo lipo kwako au eneo Hilo tu Acha kukurupuka
 
Back
Top Bottom