TCRA na TCU wachukue hatua kali kwa Wasafi TV kutokana na 'kiki' ya mapacha kufanyiana mtihani

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,853
18,268
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Kuna hiki kipande cha video kinachobamba mtandaoni kuhusu mapacha wawili ‘wanaokiri’ hadhrani kufanyiani mtihani ‘chuoni’.

Ukisikiliza kwa makini na kwa utulivu wa hali ya juu, utagundua kuwa hawa watu wanaigiza tu. Haiingii akilini watu wanaojua sheria za nchi kukiri hadharani kufanya uhalifu mkubwa kama huu huku wakifahamu kuwa wanatazamwa na dunia nzima na kwamba kufanya hivyo kunaweza kuwatia matatani kisheria.

Nina mashaka kwamba hii tamthlia itakuwa imepangwa na uongozi wa Wasafi TV ili kutafuta kiki uchwara ambazo pia zinaweza kuwaingiza hatiani ikiwa itabainika walifanya maigizo. Mashaka yangu yamegawanyika sehemu tatu:

Kwanza, mtangazaji Edo Kumwembe anauliza moja kwa moja kama mapacha hawa waliwahi kufanyiana mtihani, na wao wanakiri kweli waliwahi kufanyiana mtihani wakiwa ‘chuoni’. Na pia Edo amesema kufanyiana mtihani kunaweza kumuingiza mtu kwenye tatizo.

Hii inaashiria kuwa Edo anafahamu madhara ya watu kufanyiana mtihani ndio maana ametanguliza kauli ya kuingizana kwenye tatizo. Nafahamu Edo ni mwanahabari mwenye weledi wa hali ya juu na anayezingatia miiko ya utangazaji na utoaji habari. Hili lingekuwa sio igizo, kamwe asingethubutu kuuliza swali hili.

Pili, ukiendelea kusikiliza utasikia huyo mtangazaji aliye upande wa kulia (simfahamu jina) anasema kuwa huo ni uwongo na kuwa wataalamu wasisumbuke kwenda kufanya review (marejeo) kuhakikisha taarifa hii.

Tatu, wakati huyo pacha muongeaji (na ambaye anadai kumfanyia mwenzake mtihani) akijibu swali la Edo, pacha mwenzake anaonekana akimshika bega akiashiria kumkataza asiseme uongo hadharani. Huenda nafsi imemsuta mapema kabla mwenzake hajaongea lakini kwa kuwa huyo muongeaji huenda ndiye amepokea mpunga, anaamua kumpuuza na kuruka hewani.

Kwa mazingira haya, hii habari inaashiria moja kwa moja kuwa ni ya kutunga na imetangazwa hadharani ili kuwapa kiki Wsafi TV wapate watazamaji wengi kwenye mitandao yao ya kijamii, hasa Youtube, ili wapige pesa za kutosha kwa kujizolea watazamaji lukuki.

Turejee kwenye hicho ‘chuo’ ambacho mapacha wamesoma. Ukisikiliza kwa makini, hakuna mahali wametaja kuwa wamesoma Ardhi University. Kwa hiyo kitendo cha uongozi wa chuo kuibuka na hili tangazo wakati wakiwa bado hawajalifanyia kazi, nayo yawezekana ikawa kiki ya kutafuta kujulikana ili kuvutia wanafunzi kujiunga kwenye chuo hicho.

MAONI YANGU
Kwa taharuki hii waliyoisababisha Wasafi TV kwa lengo tu la kutafuta kiki uchwara, naomba TCRA iwafungie na kuwapiga faini ili liwe fundisho kwa vyombo vingine vya habari vyenye tabia kama hii. Wakifungiwa chaneli zao zote walau kwa miaka 5 na kupigwa faini kubwa watajifunza somo.

Aidha, kwa kitendo cha Ardhi University kuibuka kutoa matangazo wakati mapacha hawajawataja, naomba TCU iwapige faini kali, ikiwemo kumshusha cheo Makamu Mkuu wa chuo ili liwe fundisho kwa vyuo vingine vyenye tabia kama hii.

Nawasilisha.
 
Kwanza hawa mapacha hawafanani kihivyo,mmoja ana uso mpana,hii imeshindikana chuo kugundua utofofauti huo?
 
Kwahiyo unamaanisha Wasafi Tv sio sehemu ya kupata taarifa za ukweli?

Huo uchunguzi wako wa "kusikiliza kwa makini" ulifundishwa chuo kipi kinachotambulika hapa ulimwenguni?

Kama unakiri Eddo ni mwanahabari mwenye weledi, kwanini ushangae yeye kuuliza hilo swali kama hao mapacha waliwahi kufanyiana mitihani?

Unajua maana ya "leading questions" kwenye interview?

Hao mapacha wamepelekwa kingi kwa hilo swali la Eddo wakajaa, kama wangekuwa na akili kidogo walitakiwa kujua huo ni mtego waukimbie kwa kusema hawakuwahi kufanyiana mtihani hata kama waliwahi.

Umekurupuka kuja na hii thread kwa kutumia vigezo vyako binafsi, visivyo na uzito wowote kimantiki.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
💩
 
Mkuu, I regret to say your argument is baseless and unfounded. Please disproof me with facts but not with mihemko.

Mimi niweka hoja hadharani, kama unaona haina nguvu, ivunje kwa kutumia strong facts. Kumbuka wazo halipigwi rungu bali hupingwa kwa wazo jingine llilo bora zaidi (JK, 2020).
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Kuna hiki kipande cha video kinachobamba mtandaoni kuhusu mapacha wawili ‘wanaokiri’ hadhrani kufanyiani mtihani ‘chuoni’.
View attachment 2927982
Ukisikiliza kwa makini na kwa utulivu wa hali ya juu, utagundua kuwa hawa watu wanaigiza tu. Haiingii akilini watu wanaojua sheria za nchi kukiri hadharani kufanya uhalifu mkubwa kama huu huku wakifahamu kuwa wanatazamwa na dunia nzima na kwamba kufanya hivyo kunaweza kuwatia matatani kisheria.

Nina mashaka kwamba hii tamthlia itakuwa imepangwa na uongozi wa Wasafi TV ili kutafuta kiki uchwara ambazo pia zinaweza kuwaingiza hatiani ikiwa itabainika walifanya maigizo. Mashaka yangu yamegawanyika sehemu tatu:

Kwanza, mtangazaji Edo Kumwembe anauliza moja kwa moja kama mapacha hawa waliwahi kufanyiana mtihani, na wao wanakiri kweli waliwahi kufanyiana mtihani wakiwa ‘chuoni’. Na pia Edo amesema kufanyiana mtihani kunaweza kumuingiza mtu kwenye tatizo.

Hii inaashiria kuwa Edo anafahamu madhara ya watu kufanyiana mtihani ndio maana ametanguliza kauli ya kuingizana kwenye tatizo. Nafahamu Edo ni mwanahabari mwenye weledi wa hali ya juu na anayezingatia miiko ya utangazaji na utoaji habari. Hili lingekuwa sio igizo, kamwe asingethubutu kuuliza swali hili.

Pili, ukiendelea kusikiliza utasikia huyo mtangazaji aliye upande wa kulia (simfahamu jina) anasema kuwa huo ni uwongo na kuwa wataalamu wasisumbuke kwenda kufanya review (marejeo) kuhakikisha taarifa hii.

Tatu, wakati huyo pacha muongeaji (na ambaye anadai kumfanyia mwenzake mtihani) akijibu swali la Edo, pacha mwenzake anaonekana akimshika bega akiashiria kumkataza asiseme uongo hadharani. Huenda nafsi imemsuta mapema kabla mwenzake hajaongea lakini kwa kuwa huyo muongeaji huenda ndiye amepokea mpunga, anaamua kumpuuza na kuruka hewani.

Kwa mazingira haya, hii habari inaashiria moja kwa moja kuwa ni ya kutunga na imetangazwa hadharani ili kuwapa kiki Wsafi TV wapate watazamaji wengi kwenye mitandao yao ya kijamii, hasa Youtube, ili wapige pesa za kutosha kwa kujizolea watazamaji lukuki.

Turejee kwenye hicho ‘chuo’ ambacho mapacha wamesoma. Ukisikiliza kwa makini, hakuna mahali wametaja kuwa wamesoma Ardhi University. Kwa hiyo kitendo cha uongozi wa chuo kuibuka na hili tangazo wakati wakiwa bado hawajalifanyia kazi, nayo yawezekana ikawa kiki ya kutafuta kujulikana ili kuvutia wanafunzi kujiunga kwenye chuo hicho.

MAONI YANGU
Kwa taharuki hii waliyoisababisha Wasafi TV kwa lengo tu la kutafuta kiki uchwara, naomba TCRA iwafungie na kuwapiga faini ili liwe fundisho kwa vyombo vingine vya habari vyenye tabia kama hii. Wakifungiwa chaneli zao zote walau kwa miaka 5 na kupigwa faini kubwa watajifunza somo.

Aidha, kwa kitendo cha Ardhi University kuibuka kutoa matangazo wakati mapacha hawajawataja, naomba TCU iwapige faini kali, ikiwemo kumshusha cheo Makamu Mkuu wa chuo ili liwe fundisho kwa vyuo vingine vyenye tabia kama hii.

Nawasilisha.
Ardhi university washamba sana hao
 
Back
Top Bottom