TCRA: Hakuna kanuni inayokataza kusoma Magazeti kwa Mbwembwe

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Andrew Kisaka amesema kauli yake imepotoshwa kuhusu wasomaji wa Magazeti kwenye Redio akisema hakumaanisha usomaji wa mbwembwe bali wasomaji kusoma na kuingia ndani.

Akizungumza leo asubuhi na Kipindi cha Good Morning cha Wasafi Fm sehemu ya Magazeti, Bw. Kisaka amesema hakuna kanuni inayokataza kusoma kwa mbwembwe bali kanuni inataka watangazaji wasome vichwa tu vya habari za sio kuingia kwa ndani na kwamba kauli yake imepotoshwa.

Credit - Kitenge
 
Tulimshukia vikali ikabidi arekebishe kauli yake. Mbwembwe ndio kila kitu katika utangazaji zinavutia wasikilizaji
 
Back
Top Bottom