TCRA waichunguze kampuni ya simu za mkononi ya Halotel

Mkoba wa Mama

Senior Member
May 5, 2021
113
45
Mtandao wa Halotel umekuwa na tabia ya kukata salio la muda wa maongezi mara tu unapoongeza salio.

Hii imenitokea zaidi ya mara tatu sasa, na nikipiga simu huduma kwa wateja naambiwa kuna huduma nimejiunga inayokata salio hilo, wakati hakuna huduma yoyote ambayo mimi nimejiunga.

Mbaya zaidi wanaposema kuna huduma nimejiunga (kupata hadithi au taarifa za michezo kila siku) taarifa hizo nakuwa sijawahi kuzipata lakini pesa yangu wanakata.

Naomba TCRA na mamlaka nyingine zinazohusika walichunguze jambo hili. Halotel wamekuwa wahuni sana
 
Hata mimi imenitokea mara nyingi tuu. Unaninua bando hata hujawasha data wanakutumia msg umeshatumia 75% ya kifurushi ulichojiunga
 
Mimi wakinifanyia hivyo mara moja tu, napiga chini hiyo line yao. Hakuna mtandao wenye umaalum wowote sasa hivi, wote wanakaa na kukubaliana bei ya vifurushi. Mtandao ukinizingua tu naachana nao
 
Wasilisha malalamiko TCRA unaweza kupata milioni 2 kwa sababu ulikatwa Tshs. 300 tu
 
Back
Top Bottom