tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. Kingsmann

    JamiiForums Tanzania Uteuzi: Rais Samia ateua Mabalozi pamoja na kuvunja Bodi ya TCRA

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi na kuvunja bodi kama ifuatavyo: 1. Amemteua Balozi James Gilawa Bwana kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika kusini. Balozi Bwana anachukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Gaudence...
  2. kavulata

    JamiiForums Tanzania TCRA fungia mitandao ya kichochezi kabla hamjachelewa

    Kuna mitandao nchini kama Jambo tv ambayo inashabikia kutoa taarifa zinazowachanganya na kuwagawa wananchi. Serikali inasubiri hadi wapi ili kuifuta? Kule Marekani kulikuwa na mtandao wa you tube the Dive wa kijana anaeitwa Jackson Hinkle ambao ulikuwa ukiripoti habari za vita ya Ukraine...
  3. Meneja Wa Makampuni

    JamiiForums Tanzania TCRA wachunguzeni AIRTEL wameajiri watoa huduma kwa wateja wasio na qualification na hawawezi kutoa huduma za kitaalamu

    Ninaandika andiko hili kutoa malalamiko yangu kuhusu huduma za wateja zinazotolewa na kampuni ya Airtel Tanzania. Nilipojaribu kupata msaada kuhusu masuala yanayohusu mawasiliano, nilikumbana na changamoto kubwa. Inaonekana kwamba wafanyakazi wa huduma kwa wateja wa Airtel hawana ujuzi wala...
  4. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania 2018 kamati ya malalamiko ya TCRA iliitaka Voda imlipe Aboubakar Tsh 1.5m kwa kumtumia SMS bila ridhaa yake

    Aboubakar Ally alienda kamati ya malalamiko ya TCRA kulalamikia suala la kupokea sms kutoka Umojabet bila ridhaa yake. Suala hilo alilalamika Voda lakini hawakuchukua hatua. Walipofika kamati ya malalamiko Vodacom walikubali kuwa mteja wao alikuwa anapokea sms hizo lakini wao hawahusiki na...
  5. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania Ujue mchakato wa kuwasilisha malalamiko katika Kamati ya Malalamiko ya TCRA

    Ikiwa umepata huduma mbovu ya kimawasiliano, iwe kwenye kisimbuzi au mtandao wa simu ambao wote wanaratibiwa na TCRA. Ziko hatua kadhaa za kufuata ili uweze Kamati ya Malalamiko ikusikilize. 1. Kwanza ni kuwaambia kampuni yako (i.e tigo, voda au azam) ili muelezane vizuri 2. Mkishindwana hapo...
  6. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania Mwaka 2019 Kamati ya Malalamiko ya TCRA iliitaka Vodacom imlipe mteja Faini ya Tsh. Milioni 1.2 kwa kufanya SIM swap kiholela

    Bahati Mekene alipeleka malalamiko katika kamati ya malalamiko ya TCRA kuhusu Vodacom kufanya swap ya laini yake ambapo ilimletea shida hata kwenye mahusiano yake kwani aliashindwa kuendelea na mpenzi wake baada ya mwenza wake huyo kupiga simu na kupokelewa na mwanaume. Tukio hili lilitokea...
  7. mshale21

    JamiiForums Tanzania TCRA: Hatujakataza matumizi ya VPN bali ni kusajili na kutoa taarifa ya matumizi ya VPN

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia kwa Mkuu wake wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Rolf Kibaja imesema taarifa kwa Umma iliyotolewa juzi October 13,2023 haijakataza matumizi ya VPN kama baadhi ya Watu wanayopotosha kupitia mitandao ya kijamii. Kibaja ameiambia Ayo TV...
  8. Nobunaga

    JamiiForums Tanzania TCRA hili la VPN nalo litawashinda kwa sababu hamtaki kuukabili uhalisia wa mambo

    Swali kwa TCRA: Mnajua sababu ya matumizi ya VPN kuwa makubwa nchini? Uhalisia ulivyo: Kwenye teknolojia ukiwabinya sana wananchi pale, wao wanatokea kule kwa sababu ya kukua kwa teknolojia kila siku, kila kitu kina option B. Katika mambo ambayo serikali ilikuwa haijawahi kuwaza basi ni...
  9. ACT Wazalendo

    JamiiForums Tanzania Macheyeki: Zuio la TCRA Matumizi ya VPN linakandamiza uhuru wa habari Nchini

    Zuio la TCRA Matumizi ya VPN linakandamiza uhuru wa habari Nchini. Chama cha ACT Wazalendo kupitia Wizara Kivuli ya Habari na Mawasiliano tunapinga vikali taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA ya kukataza matumizi ya Mtandao binafsi maarufu kama VPN (Virtual Private Network)...
  10. G

    JamiiForums Tanzania TCRA angalieni Airtel wanavyowaibia wateja

    Leo nimepiga simu airtel huduma kwa wateja kupitia namba 100 kama wenyewe wanavyoelekeza. Ajabu hadi dakika 10 zinakwisha, sijaunganishwa na mtoa huduma, napewa tu maelekezo, bonyeza 1, mara bonyeza 6. Baada ya maelekezo hayo, napata sms kuwa nimetumia dakika 10, na kweli dakika 10 hizo...
  11. S

    JamiiForums Tanzania Je, TCRA wana mamlaka yoyote ya kutunga sheria?

    Naomba kufahamu kwa wajuvi wa sheria hapa JF. TCRA ni taasisi inayosimamia mawasiliano hapa TZ. Je hawa watu wanahusika na kutunga sheria? Mfano ni kuhusu hili suala la VPN
  12. M

    JamiiForums Tanzania TCRA watakagua simu za Watanzania wote kuwajua wanaotumia VPN?

    Nimeona katazo la Tcra kuzuia matumizi ya Vpn nakusema kuwa kuna faini ya mil 5. Sasa kwa sababu karibu kila Mtanzania mwenye smart foni amedownload VPN na anaitumia kuangalia mambo yake binafsi ya kifaragha . Je, TCRA itawag'amua vipi watu wakiwa na simu zao mkononi. Msaada wa kitalaamu
  13. Cannabis

    JamiiForums Tanzania TCRA: Ukikutwa unatumia VPN Tanzania, faini milioni 5, kifungo mwaka mmoja

    Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imewataka wananchi na makampuni kiujumla ambazo kwa asili ya kazi zao hawawezi kuepuka matumizi ya VPN kutoa taarifa juu ya VPN wanazotumia na taarifa muhimu kabla ya Oktoba 30 mwaka huu. Aidha mamlaka hiyo imesema iwapo itabainika umetumia VPN kinyume na kanuni...
  14. MSAGA SUMU

    JamiiForums Tanzania Chadema tuwahi TCRA kuzuia leseni ya Nape

    Tuna siku 14 pekoe, japo kuwa hatuna sababu ya muhimu twendeni kuizuia hivyohivyo.
  15. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania TCRA bado mnaendelea kufanya kosa kwenye jina lenu

    TCRA mimi ni mtumiaji wa takwimu zenu, ila angalieni ripoti zenu nyingi mnakosea jina lenu, badala ya kuwa "Authority" mnajiita "Authory" hii inanipa mashaka kama data mnazotoa ziko sahihi ikiwa jina lenu tu mnakosea. Ripoti ya June 2023, mmejiita "Authory" June 2022, mmejiita "Authory"...
  16. GENTAMYCINE

    JamiiForums Tanzania TCRA mmebariki huu Upuuzi wa Viongozi wa Timu za Ndondo Cup Kusifia kufanya Ushirikina Mubashara Redioni Clouds FM?

    "Hela tuliyopata tumeenda kununua Mayai Viza, Kuku Mweusi na Udi na kumpelekea Mganga wetu wa Kienyeji na kwa jinsi tunavyoenda Kuwaroga Watatukoma" Shabiki wa Timu Moja inayoshiriki Michuano iliyosifiwa na inayosapotiwa na Rais wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya Ndondo Cup' kwa Mikoa...
  17. S

    JamiiForums Tanzania TCRA kuufungia wimbo "Amkeni" wa Ney wa Mitego na kuacha nyimbo za matusi ni uchawa, kujipendekeza na unafiki

    TCRA acheni kutumika vibaya. Mmeufungia wimbo wa Ney Wamitego "Amkeni" kwasababu tu umemparura aliyewateua lkn mmeacha nyimbo kibao za matusi zkiendelee kwenda hewani. .....sijui kutongoza.... .....ikiiingia inateleza.. ....paka mate niteleze.. .....nampatia sukari ananambia ongeza.. n.k, n.k...
  18. Hismastersvoice

    JamiiForums Tanzania TCRA, hivi kwanini hamtulindi wananchi dhidi ya dhuluma? Badala yake mpo kwa kutukandamiza!

    Nilinunua kifurushi cha wiki cha Airtel nikiwa safarini Marangu Moshi, nilipofika nikakuta Airtel haipatikani hivyo kifurushi kikaisha kwa muda niliokuwepo hapo! TCRA wao wanajionea sawa tu. Nilitika Marangu nikaenda Moshi mjini eneo la KCMC ah! Nako ni shida tu mpaka mwenyeji akuelekeze...
  19. NostradamusEstrademe

    JamiiForums Tanzania TCRA naomba mchunguze namba hii inanisumbua

    Kuanzia jana napata message kutoka namba 0738264152 inaniambia naomba unitumie hiyo hela kwenye namba hii ya Airtel 0695662564 jina AGNES ALKADO nakusubilia kwa wakala. Naomba fuatilieni tukomeshe usumbufu huu
  20. lufungulo k

    JamiiForums Tanzania TCRA itoke hadharani kukiri kuwa muziki wa matapeli wa mtandaoni umewashinda

    Sasa imekuwa KERO, KERO KERO jumbe za kitapeli mtandaoni zimekuwa nyinginyingi mno! Hapa nadhani TCRA umefikia wakati watoke hadharani na kukubali kuwa muziki wa matapeli umewashinda. Kama kupata line za simu lazima uwe na namba ya NIDA, iweje tabia hii ya kitapeli izidi kushika kasi? TCRA...
Back
Top Bottom