Ukiwa na changamoto yoyote kwenye basi, wasiliana na LATRA 0800110020.
MAGUFULI BUS TERMINAL 0734450010.
Watu wengi au abiria bado hatuna elimu ya kutofautisha haya madaraja ya mabasi licha ya mamlaka kupanga nauli kulingana na vyombo husika bado tunahitaji uelimishwaji wa hali ya juu. Leo...
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Moshi imewakamata wafanyakazi wa kampuni tajwa hapo juu baada ya kujificha maliwatoni na kuwatelekeza abiria pasipo kuwatafutia usafiri mbadala baada ya kampuni yao kufungiwa na LATRA.
Chanzo gazeti la Mwananchi.
Nchi ya Senegal imezindua mradi wa usafiri wa kwanza wa mabasi yaendayo kasi ya umeme (BRT) katika mji mkuu wa Dakar.
Katika hafla ya uzinduzi, Waziri Mkuu wa Senegal Amadou Ba alisema kuwa mradi huu ni miundombinu ya kisasa sana, na pia ni uvumbuzi mkubwa.
Mradi wa Dakar BRT, unaojivunia...
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imeyasimamisha magari yote ya Kampuni ya Kilimanjaro Express kutoa huduma ya usafirishaji kuanzia jumatatu kutokana na kukiuka masharti ya leseni ikiwamo kutotoa tiketi ya kielektroniki na kuzidisha nauli kwa abiria.
Agizo hilo limetolewa leo na...
Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Katavi kimebaini dosari katika mabasi yanayotumiwa kusafirisha Wanafunzi katika Shule za watu binafsi ikiwemo baadhi ya mabasi kukutwa yamefungwa mipira kwenye mfumo wa breki ambayo ni hatari kwa usalama.
Dosari hizo zimebainika wakati...
Nikiwa katika pitapita zangu za kusafiri mwishoni mwa mwaka huu wa 2023 nikajikuta mikoa ya kaskazini, nikatua Stendi kuu ya mabasi ya mikoani pale Moshi mjini na hapo nikakutana na mambo ya ajabu, yaani uchafu, ushamba na ujinga wa kiwango cha juu kupitiliza tena mamlaka za serikali...
Moja kwa moja kwenye mada.
Stendi ya Mabasi Sengerema ni moja ya stendi inayohudumia magari mengi kwa siku. Magari yote yanayokwenda mikoa ya Kigoma, kagera, Geita na wilaya zake kutoka Mwanza yanapita hapo.
Kinachosikitisha stendi imejaa mashimo kama majaruba, gari zinapita kwa shida, Ushuru...
Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha limesema linaendelea na ukaguzi wa magari ya Shule ikiwa ni utaratibu wao wa kila mwaka kabla ya muhula wa masomo kuanza ambapo imekuwa ikifanya ukaguzi wa magari hayo ili kubaini changamoto na kutoa maelekezo ya matengenezo ya vyombo...
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kimechukizwa na kitendo cha baadhi ya wamiliki wa mabasi kuwafukuza madereva kwa kudaiwa kutoa taarifa kwa mabasi mabovu kwa Vyombo vya Usalama Barabarani ambapo limesisitiza sheria kali kuchukuliwa dhidi ya mmiliki atakaye mfukuza dereva.
Deus...
Azam TV wakonga nyoyo za burudani Tanzania baada ya kutambulisha Visimbuzi vya kwenye mabasi. Hivi sasa tutakuwa tunacheki mechi za simba na yanga kwenye mabasi ya mikoani. Kupitia kurasa zao leo wametangaza rasmi kutoa huduma hiyo.
========
Azam TV Revolutionizes Travel Entertainment with...
Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.
• Dar - - Mwanza
• Dar - - Mbeya
• Dar - - Kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar --...
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kupitia Kikosi cha usalama barabarani limeyazuia mabasi matano ya abiria katika Stendi kuu Jijini Mbeya kuendelea na safari baada ya kukutwa na changamoto katika mifumo mbalimbali.
Akizungumza mapema Desemba 26, 2023 Mwanasheria Mkuu wa Kikosi cha usalama...
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limefanya ukaguzi wa mabasi ya abiria katika Stendi Kuu ya Mabasi kabla ya kuanza safari na kuwataka madereva kuzingatia Sheria, Kanuni, Alama na Michoro ya Usalama Barabarani ili kuepuka ajali.
Akizungumza Disemba 23, 2023...
Jamani kwani serikali inakazi gani??inakuwaje inaleta mfumo mpya kwa lengo la kurahisisha na kuleta ufanisi katika anga la usafiri lakini inashindwa kabisa kufata sheria walizoweka wenyewe??
Juzi nimetoka zangu mkoani kuja zangu Daaslamu huku usafiri mkubwa na watabu ukiwa ni...
Serikali imepunguza 50% ya Nauli za Mabasi pamoja na kufuta Nauli za Usafiri wa Treni za Umma kwa lengo la kuwapunguzia Wananchi gharama za Maisha hasa katika Msimu wa Sikukuu za Mwisho wa Mwaka.
Taarifa ya Serikali, imeeleza kuwa Rais Bola Tinubu ameagiza Mabadiliko hayo yaanze leo Desemba 21...
Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) wamefanya ukaguzi wa kushtukiza ili kubaini kama Wananchi wanalipa nauli halali zilizotangazwa na Serikali mapema mwezi huu ambapo wamebaini baadhi ya wamiliki na mawakala...
Mlioko hapo Karibu embu mtujuze iwapo hizi habari ni za kweli.
Wengine wanasema kuna kikundi kimepewa kazi maalum ya kushughulikia legacy. Kimeona umati mwingi wa wageni unafika hapo Toka mikoa mbalimbali na hivyo Jina la Magufuli linaweza lisifutike.
Habari,
Kwa wanaofahamu, naombeni utaratibu wa kufuata nikitaka kupata kibali cha kufanya biashara ya mabasi Tanzania. Nataka nianze na mabasi 4 route ya Dar-Mwanza.
Kidogo tumeanza kubadilika
Majuzi nilisafiri na basi moja to Arusha
Wakataka details zangu hamad nikaweka alarm, yaani sijaamka
Nasikia simu habari naviga toka kampuni fulani safari yako ni saa tukukute kituo fulani muda wa kuamka sasa
Nilipenda sana nikatamani na ndege mtuamshe hivi maana...
Habari!
Nataka kufikisha kero hii kwa niaba ya wasafiri wanaoingia na kutoka katika Stand Kuu ya Mabasi, Dodoma. Kila mtu anajua kuwa ni wajibu wa raia kulipa kodi, lakini ni lazima kuwe na mantiki katika hiyo kodi. Nimeshangazwa sana na utaratibu wa ushuru uliowekwa katika stand hii ambao...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.