Udalali stendi za mabasi too much

Ricky Blair

JF-Expert Member
Mar 13, 2023
391
873
Ifike muda udikteta tu uje na kuwaondoa hawa madalali kwa nguvu hata km damu ikimwagika coz imezidi. Mtu hata raha huna ni harassment daily tu hata uwe na tiketi yako au la kwenda mikoani. Na pia ifike muda sio kila basi lipewe leseni ya kusafiri km halikidhi hadhi. Unakuta kampuni km 100 98 zote utumbo; na kila kampuni marufuku hao madalali; mtu ofisi naiona bado mimtu inakuja kunisumbua? Maana yake nn labda??na yote yanatoa ahadi ambazo mabasi hayana? Kwanini hawa watu serikali wanawaacha watusumbue sisi tu? Kwanini msiwapeleke Airport tuone wawasumbue na nyie; ethiopian airlines uku Qatar airlines uku tuone km kuna mgeni wa maana atashuka Dar airport. Na kila basi even luxury yamegeuka makosta jaman hata ham ya kusafiri mkoani sina. Bora niweke budget nipae tu yaani ukiachana na Abood na Shabiby na Tahmeed yote yaliyobaki ni utumbo tu. Hawa watu waondolewe jaman na wakatazwe kuwepo kw stend km hamna cha maana wanafanya stend kubwa zilizowekewa mageti km Mbezi Luis na zingine.
 
Sijakataa watu kujipatia riziki. Ila kuna udalali mwingine hauna maana km mtu mw macho anaona anapoenda. Narudia waende Airport km watavumiliwa hata robo; hii yote coz izo ni sehem za masikini au watu wa kawaida kwaiyo hata watu wangekuwa wanamwagiwa tindikali, kubakwa au kuchinjwa isingewastua watu
Tuvumiliane tu bwa shee...tuna familia, Leo unatusema hivyo, hata wewe dalali ajaye.....kazi ya wahindi sio kazi ndugu yangu....SEMA Amina na mungu atakubariki
 
Wale wa pale mbezi ndo huwa wananichosha. Daladala/mwendokasi ikiwa inaingia stendi inavokimbiliwa na wapiga debe unaweza dhani mtu kaibiwa na wamemuona mwizi wao.
 
Jitathimini kijana ukiona unapata harassment za namna hiyo ktk maisha basi tambua watu wa aina hiyo wameona udhaifu wako wa kiakili au kimuonekano...
Mtu hakujui humjui hawez kukufanyia hayo yote...
 
Wale wa pale mbezi ndo huwa wananichosha. Daladala/mwendokasi ikiwa inaingia stendi inavokimbiliwa na wapiga debe unaweza dhani mtu kaibiwa na wamemuona mwizi wao.
😄😄😄😄 Hadi kushuka unawaza unashukaje ukikaa kiboya wanakuibia.
 
Jitathimini kijana ukiona unapata harassment za namna hiyo ktk maisha basi tambua watu wa aina hiyo wameona udhaifu wako wa kiakili au kimuonekano...
Mtu hakujui humjui hawez kukufanyia hayo yote...
nenda stend ya Magufuri , tujifunze kufanya tafiti kabla ya kuhukumu mtu
 
Ingekuwa amri yangu inchi hiii isingekuwa na mpiga debe!
Sujatembea hivi huko u.k, ulaya,na inchi zingine Kuna wapiga debe??
 
Abood, Tahmeed, Shabiby hazitoi posho a.k.a loto kwa hao wasumbufu.

Na endapo kampuni zote zingefanya kama wafanyavyo hizo tatu na nyinginezo wasingekuwepo hao watu, kisa na mkasa kuwepo kwao hapo ni kwa sababu kuna mabasi yasipofanya huo mtindo hayataondoka stendi sababu yatakosa abilia.

Na kinachofanyika wanalipwa 1000 au zaidi kwa kila abilia anayepelekwa ktk kampuni anayoona inatoa loto ndefu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom