JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums
Mdau wa JamiiForums analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni. Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu. Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
JamiiCheck ni Moja kati ya Majukwaa yanayopatikana ndani ya tovuti ya JamiiForums.com. Jukwaa hili limewekwa mahsusi kwa ajili ya kufanya uhakiki, kutafuta uthibitisho au uhalisia wa habari, taarifa, matukio, picha au video mbalimbali zinazojitokeza au kuibuka kutoka katika vyanzo mbalimbali ndani na nje ya mtandao. Tofauti na Majukwaa na vyombo vingine vya kuhakiki ukweli wa habari, JamiiCheck ni Jukwaa pekee linalotoa fursa kwa watumiaji wake (Wanachama wa JamiiForums.com) kushiriki katika uhakiki kwa kuleta taarifa, picha au Video mbalimbali ambazo wanahitaji kuzichunguza kupata ukweli au chanzo chake pamoja na kuchangia/ kutoa maoni kwenye taarifa nyingine zilizohakikiwa. Ikiwa utakutana na habari au taarifa yoyote inayokutatiza...
Nina swali ndugu zangu hivi inawezekana siku za hatari zikaangukia katika mzunguko kuingiliana na siku za hedhi? Mfano, siku za hedhi ni tano ile siku ya 4 au 5 ikiwa siku ya hatari?🤔
Pamekuwa na maneno kuwa Wananchi wa FIJI wana asili ya Tanganyika. JamiiChek tusaidieni kufanyia kazi suala hili. Wakazi wa Fiji (Chanzo: Mtandao)
Hivi ni kweli kuwa ukomo wa kurefuka na kunenepa kwa uume ni miaka 20? Yaani mtu mwanaume mwenye umri wa miaka 25 au 30, kamwe hawezi ku experience ongezeko la ukubwa wa uume wake? Kwa maana nyingine, ukubwa wa uume wa mwanaume akiwa na miaka 20, ndio atakaokuwa nao akifikisha miaka 35?
Salaam Wakuu, Nimeona taarifa imepostiwa na Boniface Jacob kupitia ukurasa wake wa X ikiambatana na video inayoonesha maji mengi ya mvua yakitiririka katika barabara ya Mlima Kitonga. Video hii imepostiwa pia na Change Tanzania pamoja na MwanaHabari. Je kuna ukweli wowote kwenye hili?
Salaam Wakuu, Kupitia WhatsApp yangu nimetumiwa ujumbe wa tahadhari kuhusu kuwepo kwa Mvua katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Ujumbe huo unaeleza: Shinyanga, Dar, Pwani, Mafia,Tanga, Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kigoma na Kagera tujiandae, kutakuwepo na Pacific El nino na Atlantic El nino, mvua zitakuwa kubwa na hatari sana, Mungu atunusuru. Hali ya hewa tayari imebadilika kuanzia juzi, upepo umeanza katika bahari za Atlantic, Pacific na Hindi, Wavuvi wameanza kuzuiwa kwenda kuvua na Meli za tafiti zimeanza kukumbana na dhoruba kali sana Baharini, picha za satellite sio nzuri kabisa. Tunatarajia magonjwa ya Kuharisha, Dengue, Malaria na Homa kuongezeka, tuchukue tahadhari mapema. Tuangalie nyumba zetu kama zinavuja...
Msiwakate watoto vimeo kwa sababu zozote, inaweza pelekea mtoto kupoteza maisha kutokana na kuvuja damu; kama mtoto ana shida yoyote muone daktari atakushauri tiba sahihi.
Nimesoma sehemu kuwa ndege aina ya Bundi, licha ya kuhusishwa na imani za kichawi kama mikosi, mtu kufariki akionekana au kusikika akilia jirani, kutokea ghafla nk eti si kweli kwamba ni mchawi bali ana uwezo wa kunusa mtu aliyekaribia kufa. Je, ukweli wake ni upi?
Mwanamke asipo mnyonyesha mtoto kwa zaidi ya siku moja maziwa yake huchacha na kuharibika. Wanawake hushauriwa kumwachisha mtoto ziwa ili asidhurike kwa sababu maziwa hayo hukosa tena sifa ya kutumiwa na mtoto. Ukweli upoje?
Akili Mnemba ni teknolojia iliyosambaa ulimwenguni ikiwa imerahisisha kazi za binadamu kutokana na kwamba inaweza kufikiri kama binadamu. Lengo la AI ni kuweza kufanya mambo kama vile kutambua mifumo, kufanya maamuzi, na kuhukumu kama binadamu. Pamoja na lengo zuri la teknolojia hii ya Akili Mnemba (AI), watu wasio wema wamekuwa wakiitumia katika kupotosha habari mbalimbali katika Jamii. Baadhi ya nchi Ulaya zimechukua hatua ya dhati kukabiliana na matumizi ya akili mnemba ambapo zimeyataka makampuni yenye majukwaa makubwa ya kimtandao, kuziwekea alama maalumu video, sauti na maandishi vilivyotengenezwa kwa kutumia akili bandia ili watumiaji wavitambue. Zinahofia kuwa teknolojia ya akili Mnemba inaweza kuwa ardhi yenye rutuba ya...
Utengenezaji wa taarifa potofu (feki) unapingwa katika nchi mbalimbali. Baadhi ya watu katika jamii nyingi wamejikuta matatizoni kwa kuingia vifungoni au kulazimika kulipa fidia kwa sababu ya kutoa taarifa potofu kuhusu watu, kampuni na taasisi mbalimbali. Tanzania, kama nchi nyingine, ina sheria zinazodhibiti uzalishaji na usambazaji wa habari feki au za uongo. Sheria zinaweza kutofautiana kidogo kulingana na nchi, lakini lengo ni kudhibiti habari ambazo zinaweza kuleta madhara kijamii, kisiasa, au kisheria. Kwa mfano, Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 kifungu cha 16 (1)(2) ya Tanzania nchini Tanzania inadhibiti matumizi mabaya ya teknolojia ya habari na mawasiliano. Sheria hii inaweza kutumika kufuatilia na kuchukua hatua...
Nimeona kwenye mitandao ya kijamii video ya kijana akitapika damu wakidai kuwa tatizo ilo limemkuta baada ya kutumia dawa inayo itwa carbotoux je, taarifa hizi niza kweli?
Wakuu habari, Leo katika pita pita zangu nikakutana na uvumi kuwa mtu akila Tango na Asali anaweza kufa. Je kuna ukweli wowote juu ya hilo? Na kama kuna ukweli chanzo kitakuwa nini?
Akiwa anatoa hija yake kuhusu athari za habari potofu Mwandishi w Urusi Julia Loffe anaeleza: Habari Potofu inaweza kugeuza Maoni ya Umma na kusababisha uungwaji mkono wa Sera na Viongozi wa Kisiasa wasiofaa. --- Habari Potofu huathiri Michakato ya kupata Viongozi wa Kisiasa, hushusha Imani ya Wananchi kwenye Mifumo ya Kidemokrasia pamoja na kusababisha kuchaguliwa kwa Viongozi wasiofaa au wenye uwezo Mdogo. Hivyo kutokana na hoja ya Mwandishi huyu ni Muhimu kupata Habari kutoka Vyanzo vya Kuaminika pamoja na kuzithibitisha kabla ya Kuziamini au Kuzisambaza ili kuepuka athari hizi ambazo huchochea Mgawanyiko kwenye Jamii na Kurudisha nyuma Mshikamano wa Kitaifa.
Usambazaji wa taarifa potofu umekuwapo muda mrefu sana, usambazi wa taarifa potofu umekuwa ukifanywa kupitia njia mbalimbali kama; Mitandao ya Kijamii Mitandao ya kijamii imekuwa ni njia ya haraka na inayoweza kufikia watu wengi zaidi ndani ya muda mfupi, hii imekuwa ni moja kuu ya kusambaza habari. Kupitia njia hii watu waovu wamekuwa wakiitumia kusambaza habari potofu kwa manufaa yao. Wamekuwa wakitumia majukwaa kama Facebook, Twitter, WhatsApp, na Instagram kusambaza habari za uwongo au uzushi. Barua pepe na Ujumbe Njia hii imekuwa ikitumiwa kwa muda mrefu kusambaza jumbe za uongo, mara nyingi imetumiwa a matapeli kuibia watu. Watu wamekuwa wakitumiwa barua pepe zenye jumbe zushi za kulaghai huku zikiwataka wasambaza zaidi ili...
Nimekuwa nikisikia kuwa Rais wa zamani wa Malawi, Dkt. Hastings Kamuzu Banda aliwahi kuwa Daktari wa Malkia wa Uingereza na alihasiwa asije akatembea na Malkia Elizabeth na kuzaa naye. Kuhasiwa kwake huko kulipelekea Dkt. Kamuzu Banda mpaka anafariki dunia mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 99 kutobahatika kupata mtoto yeyote. Malkia Elizabeth ii akiwa na Dkt. Kamuzu Banda (Mwaka 1985)
Takwimu ni taarifa (data) zilizokusanywa, zikahesabiwa, na kuchambuliwa ili kutoa ufahamu au maelezo kuhusu kitu fulani. Kwa mfano, takwimu zinaweza kuwa idadi ya watu katika eneo fulani, matokeo ya utafiti, au hata vipimo vya kisayansi. Takwimu zinaweza kutumika katika nyanja mbalimbali kama vile sayansi, biashara, sera, elimu nk ili kusaidia katika kufanya maamuzi mbalimbali na ikiwa takwimu hizo zitakuwa potofu zitasababisha kupatikana kwa matokeo potofu yatakayoharibu malengo na mipango ya jambo kusudiwa. Udanganyifu wa takwimu huweza kutokea au kufanywa katika uchambuzi wa data au utafiti. Wakati data zinakusanywa, kuchakatwa, na kuanaliziwa kunaweza kufanyika upotoshaji au udanganyifu wowote ili kutimiza lengo lolote...
Taarifa potofu ni habari ambayo si sahihi. Taarifa potofu inaweza kuwa na athari hasi au kuwachanganya watu kutokana na ukosefu wa usahihi au udanganyifu. Athari za taarifa potofu yanaweza kuwa makubwa au vinginevyo kulingana na unyeti wa taarifa iliyosambazwa ikiwa haina usahihi. Kadiri inavyozidi kusambaa na kuchukua muda mrefu bila kukanushwa au kutolewa ufafanuzi wa upi usahihi wake ndivyo huweza kuathiri kundi kubwa zaidi na kuleta madhara zaidi. Pamoja na hatari iliyopo juu ya usambazaji wa taarifa potofu bado jamii hailichukulii kwa uzito suala la kufanya uhakiki wa taarifa unozopokea wala kusambaza wala kutilia mkazo elimu ya ya kutambua ubaya wa taarifa potofu, lindi la kusambaa kwa taarifa potofu kupitia mitandao ya kijamii...
Upotoshaji kwa kutumia jina ni kitendo cha kutumia jina la mtu, kundi, taasisi au kampuni ambayo si wewe na kulifanya kama lako. Upotoshaji wa jina mara nyingi huwalenga watu, kampuni au taasisi maarufu ili lengo la mpotoshaji litimie kwa urahisi. Upotoshaji wa jina umekithiri sana katika mitandao ya mbalimbali ya kijamii ambapo ukimtafuta mtu fulani maarufu utaona jina lake linatumiwa na watu wengi. Sababu za upotoshaji wa jina Upotoshaji wa jina huweza kuwa kwa sababu mbalimbali miongoni mwa hizo ni: Kujinufaisha au kuingiza kipato - Huu ni upotoshaji wa jina unaohusu zaidi matumizi ya jina la biashara au Kampuni ya kutoa huduma fulani. Mpotoshaji wa jina anatumia jina la Kampuni fulani kama lake Ili aweze kupata wateja wanaopenda...
Wataalamu wa afya huelezea umuhimu na faida za kufanyika kwa tendo hili kwa wanaume. Baadhi ya sehemu wanaume huwa hawatahiriwi kabisa, na wengine wanaotahiri husubiri hadi mtoto afikishe walau miaka 12 ndipo afanyiwe tendo hilo kwa uoga wa kupunguza ukubwa wa viungo hivyo. Madai haya yamekuwepo kwa muda mrefu, na majibu sahihi bado hayajatewa. Ni kweli kuwa tohara hupunguza ukubwa wa via vya uzazi vya mwanamme?
Vichwa vya habari vinaweza kuwa sehemu muhimu katika kusambaza habari potofu kwa sababu vinaweza kuvutia umakini wa wasomaji, kuchochea hisia, na hata kutoa taswira isiyo sahihi ya habari kamili. Katika dunia ya sasa ambayo teknolojia ya habari imekua kwa kiasi kikubwa, baadhi ya watu wanaweza kutumia uandishi wa vichwa vya habari kama njia ya kuhadaa umma ili kufikisha ujumbe wanaokusudia. Hapa kuna njia kadhaa ambazo vichwa vya habari vinaweza kuchangia katika kusambaza habari potofu: 1. Kuchagua Maneno yanayovuta Upande Mmoja: Vichwa vinavyoleta hisia ya upendeleo au kuunga mkono upande fulani wa habari vinaweza kusababisha upotoshaji wa mtazamo wa habari. Mfano: Wakristu (au waislam) wanyayasika huko XYZ Jinsi inavyopotosha...
Back
Top Bottom