Mjue Mbunge Maganga Aliyekuwa Dereva wa Malori na Mabasi na Sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MBUNGE NICODEMAS MAGANGA: NILIKUWA DEREVA WA MALORI NA MABASI, SASA NIMEKUWA MBUNGE WA JIMBO LA MBOGWE

"Nimetokea familia ya maisha ya kati sana. Baba yangu ni mkulima na Mfanyabiashara, nimebahatika kuwa mtoto wa nane katika familia yetu. Tulikuwa tunaishi Shinyanga Vijijini lakini baadaye tukahamia Mkoa wa Geita" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Nilianza na Biashara ya Dagaa, nikarudi Masumbwe, nikafanya Biashara ya Ng'ombe. Baba yangu alitajirika akawa na Malori nikaanza kuwa naendesha Malori na Mabasi ya baba yangu. Nimekuja kujulikana kwenye jamii kama dereva wa Malori na Mabasi ambayo yalinipa umaarufu mkubwa sana mjini" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Mwaka 2015 niliingia kwenye harakati za kisiasa nyota iling'ara watu wakawa na imani na mimi. Sikuwa na mtaji kuwapa watu waliokuwa wananishika mkono ila walipendezwa na jinsi nilivyokuwa nazungumza kwenye majukwaa ikiwemo kuwatetea watu pale walipokuwa wanaonewa" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Kwenye Serikali kuna watu hawajapitia maisha ya misukosuko, hawazijui shida. Unawakuta wanaumiza sana wananchi wa hali ya chini na mimi nikawa kipaumbele kuwasaidia na kuwatetea" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Nimepata ubunge kiurahisi kwasababu nimejikuta jamii nyingi nimeisaidia na ikaweza kunishika mkono mpaka leo nikawa mtetezi wao kama Mbunge na Mwakilishi katika Jimbo la Mbogwe" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Maisha ni Mipango ya Mungu, sikutegemea kama nitakuja kuwa mwanasiasa. Siku moja nilala nikaota ndoto naona nimekuwa Mbunge. Nikajaribu kuzungumza na watu nikaona mwelekeo naelekea kwenye ubunge. Mungu alipanga niwe Mbunge, kwahiyo sikuhangaika sana kuishika hii nafasi" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Namuomba Mungu azidi kunipa hekima na busara ili popote ninapokuwa nasimamia majukumu yangu ya Kibunge niweze kutembea na watu wangu wa chini. Kilichonishawishi kuishika nafasi ni ili niweze kuwatoa watu wakiwa wanaonewa" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Watu wengine wananichukia sana. Unaweza kukuta kituo cha Polisi kina mtu siyo mwaminifu, kazi yake ni kula rushwa ambayo ni kinyume na Sheria. Ninapokuwa Mbunge ni rahisi kusema wewe usifanye hivi kwasababu Katiba inakataa kutokana na nguvu ya kuchaguliwa na watu ni lazima waogope na waweze kuwatendea watu haki" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Nina Biashara zangu, nina vituo vya mafuta ambavyo kabla sijawa Mbunge nilikuwa navisimamia kama Msimamizi mkuu wa Kampuni kuhakikisha hesabu zinaenda sawa. Wakati mwingine huwa naendesha Malori nikiwa na madereva wangu nawasaidia ili nione hali halisi ya njiani ni jinsi gani madereva wanakutana na changamoto ikiwemo kuombwa rushwa" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe

"Cheo ni dhamana, najua siku moja naweza kuicha hii nafasi nikarudi kwenye kazi zangu. Sitaki kubweteka kwasababu mimi ni Mheshimiwa niache kufanya shughuli zangu ambazo zimenifanya kuwa Mbunge. Nikarudi nyumbani huwa nafanya shughuli nilizokuwa nazifanya" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-01-19 at 19.58.06.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-19 at 19.58.06.jpeg
    59.4 KB · Views: 5
  • WhatsApp Video 2024-01-19 at 19.58.08.mp4
    32.8 MB
  • WhatsApp Video 2024-01-19 at 19.58.09.mp4
    17.1 MB
  • WhatsApp Video 2024-01-19 at 19.58.10.mp4
    18.1 MB
  • WhatsApp Video 2024-01-19 at 19.58.10(1).mp4
    20.1 MB
  • WhatsApp Video 2024-01-19 at 19.58.11.mp4
    12.4 MB
Hawasemagi pesa wamepata Kwa njia gani, dereva wa maroli hawezi kutunza pesa mpaka amiliki over million 100 za kuwahonga CCM kwenye Kura za maoni.
 
Back
Top Bottom