Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,099
- 156,890
Kùjifunza ni kitu kisicho na mwisho wala mipaka. Serikali yetu na watendaji wake hawajàona haja ya muda mrefu kujifunza na kuchukua tahadhari dhidi ya fainali ya Ligi Kùu ya mbio za mabasi Tanzania kati ya New Force/ Golden Deer vs Sauli.
Maafa tumeanza kuyaona, leo mabasi yamegongana na Lori la mafuta, watu wamekufa, wengine kujeruhiwa. Lakini kesho makosa haya haya yatajirudia na watendaji wa serikali wenye wajibu wa kuwadhibiti wasafirishaji hawa wataendelea kushabikia fainali hiyo.
Polisi wa usalama barabarani na LATRA wanahusika kwa kiasi kikubwa kutokana na udhalimu huu unaoathiri maisha ya abiria wasio na hatia.
---
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bw.Abubakar Kunenge, amezungumza na #ITVDigital ambapo amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu wawili katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya New Force, basi la Kampuni ya Sauli pamoja na Lori la mafuta, katika eneo la Ruvu, mkoani humo.
Kunenge amesema abiria walifanikiwa kutoka kwenye mabasi hayo isipokuwa abiria wawili ambao walikuwa wamebanwa kwenye moja ya mabasi hayo na wakati Jeshi la Zimamoto na Jeshi la Polisi wakiendelea na juhudi za kuwaokoa ndipo moto ukalipuka na kusababisha abiria hao kufariki dunia.
Soma:
- Kugongana kwa mabasi Sauli na New Force lilikuwa jambo la Muda tu