Huduma ya choo ndani ya Mabasi ya masafa marefu iwekwe kwenye Mabasi ya madaraja yote

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Salaam ndugu zangu,

Kuwapo kwa choo kwenye basi lolote la masafa marefu ni muhimu na ni huduma inahitajiwa na abiria wote. Kitu cha kushangaza huduma hii ya lazima imetengwa na kuwekwa kwa mabasi ya Luxuary pekee.

Huduma ya choo ni muhimu kama ilivyo huduma nyingine, kwa jinsi binadamu alivyo atahitaki kwenda kujisaidia baada ya muda fulani.

Kufanya huduma ya choo iwe tu kwenye mabasi ya luxury ni ubaguzi usio wa kiungwana kwa abiria wasiomudu nauli za mabasi Luxuary. Ni kama unamwambia mtu usibanwe na haja yoyote mpaka muda ambao sisi tutaamua kusimama kuwaruhusu kuchimba dawa.

Rai yangu ni kwamba Mabasi yote yanapaswa kuwa na huduma ya choo kama huduma ya msingi kwa abiria wote. Huduma nyingine kama chai, juice, chakula ndio ziwe za zaida na mtu kama anazitaka atakiwe kulipia zaidi kuzipata.

Nawasilisha
 
Adventure ya Kigoma- Dar ikiwekewa choo kutakalika kweli..?

Kuna chuma kimoja kinaitwa Lushanga lile basi likiwekewa choo itakua balaa 😄
 
Back
Top Bottom