MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 12,694
- 2,000
Zitto Kabwe amewashutumu viongozi wa upinzani walioenda kwenye sherehe za uhuru, Mwanza na kupanda jukwaani kuomba maridhiano ya kisiasa kwa Rais Magufuli.
Ametoa shutuma hizo kupitia mitandao ya kijamii akidai walichofanya ni kujipendekeza kwa Rais ili waachiwe nafasi chache za ubunge mwaka 2020 huku wakiwaacha njia panda wanachama wa vyama vyao waliowaambia wajitoe kwenye chaguzi za serikali za mitaa.
Zitto ameenda mbali zaidi na kudai kinachohitajika kwa sasa Tanzania Bara ni siasa kali kama zilizofanywa na wapinzani huko Zanzibar mwaka 2001 ambako kulipelekea CCM kutaka maridhiano (ametumia neno kuomba poo).
Amemaliza kwa kusema, maridhiano hayaombwi bali yanadaiwa.
====
Hoja za wadau

Mimi namuunga mkono Zitto, haki haiombwi wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, inadaiwa.
Kama upinzani nchini unacholilia ni kutendewa haki, hadi ukajitoa uchaguzi wa serikali za mitaa, tulitaraji huo upinzani uidai hiyo haki, lakini sijaona juhudi za upinzani wowote nchini Tanzania ukifanya juhudi zozote kudai haki.
Magufuli alipoingia tuu alipiga marufuku mikutano ya siasa kinyume cha katiba, kilichotokea kwenye ushawishi/ununuzi wa viongozi wa upinzani kuunga mkono juhudi, sote tunakijua. Kilichotokea uchaguzi wa serikali za mitaa, sote tunakijua.
Mbowe akaona inatosha, Chadema haina uwezo wa kudai haki, hivyo ameomba poo kwa Magufuli kumaanisha sasa uendeshaji wa siasa za Tanzania ni kwa hisani ya Magufuli. Badala ya mapambano ya kudai haki, Mbowe ame opt kutafuta suluhu kwa maridhiano ya kisiasa.
P
Mkuu mie kwa hili naona Mbowe yuko sahihi, ni miaka 4 imepita ambayo siasa za upinzani zimepitia shida kubwa na kwa uchaguzi ulivyokuwa ni proof kuwa mwakani hakuna hopes za mpinzani yeyote kurudi.
Sasa kwa muda uliobaki (miezi 10) suluhu ya kisiasa inatakiwa ili uchaguzi huru na haki uhakikishwe so maridhiano ni jambo jema kama upinzani watatala CCM isikilize maoni yao ila siasa za mapambano kwa mtu kama Rais wetu haziwezi saidia sababu ana ego so yuko tayari hata kuua waandamanaji wote kuprove nguvu yake na hyo itakuwa na faida gani kwa upinzani?
Hata wakiandamana wataundiwa kesi nyingine kama ya Akwilina na mwaka unao wote wataishia selo tu. So kama Violent option sio viable ni heri njia zote za kidiplomasia zitumike ili zikifeli basi watakuwa hawana la kupoteza wakianza siasa za kibabe kama ODM kenya.
Zitto Kabwe has called out opposition leaders demanding political reconciliation from President Magufuli, saying reconciliation is owed.
On his Twitter, Zitto goes on to say opposition leaders did that in order to defend their seats in the Parliament. This is after Freeman Mbowe and other leaders from CHADEMA attended the Independence Day Celebrations and demanded reconcilliations from the government on their speech.
He insisted that what mainland Tanzania needs moving forward is radical politics.
On this, many say Zitto is on a ‘social media rant’ because what happened during the Independence Day celebrations caught off guard. Others have expressed that he is right, and they stand with him.