Aisee. Kumbe ZITO ndivyo. Achana kutaka data sijui za kimahesabu sawa, lakini kitendo cha KUCHUKIA kile wengi tunapenda ni TATIZO amechukia watu au mtu anadhani ameumizwa WASAMEHEANE yaani hili ndilo kachukia maana yake anatamani VURUGU tu basi.

Hoja fikirishi ni hii ni Tz wa kuzaliwa lkn sio asili yetu. Japo wengi wakifuatwa asilia yao inaweza kutokea nchi nyingine lkn hili ni maalum maana Wazazi wake wa karibu yaani Baba na mama si watanzania sio tu babuzake No ni Baba na Mama. Hivi vyombo vyetu vya usalama mbona vinarahisisha mambo? Huyu alihitajika kumulikwa sana au hata sasa nyendo zake ziratibiwe ni rahisi kupandikizwa , maana anao baba zake wakubwa au shangazi na wajombo huko kwao sio Tz.
Ajenda zake nyingi ni kusimama kinyume. Hata unakumbuka mgomo wa Upinzani Ubungeni alijifanya yeye msamaria, tena wakati wa UKAWA alijitoa , kimsingi haitakaa aside upande wa serkali wala upinzani.

Anatumia weakness anazoziona na kutuaminisha ni mkweli anakuja na data za weza kuwa za Kweli ili tumkubali. Sasa ileweke Tz sasa haiitaji takwimu za makaratasi la sivyo utapoteza mvuto sisi ni TOMASO tunataka kuona au kugusa.
Kama serkali inafanya kitu tunaona hata ukitumbia kwa data zako kuwa hakuna hosp iliyojengwa tunakunyamazia ,

Mbowe anaenosha ukomavu eandelee tu asiogope tuko nyuma yake hata kama ni KUTUBU atubu huyu ni Mzalendo wa kweli kabisa.
Ukivuliwa nguo chutama.
 
suala la JPM kuja kuwasema CDM mbele ya safari ni kusubiri na kuona, but muhimu CDM wameonesha motive ya kutafuta maridhiano, kama yeye anavyopenda kujinasibu anamjua Mungu sasa ndio aoneshe kwa vitendo, vinginevyo akipuuzia halafu aendelee kumtaja Mungu kwenye shughuli zake, sijui atakuwa anamtaja mungu wa wapi!, na wastaarabu wote watakuwa wamejionea aina ya mtu alivyo.
Maridhiano hayaombwi, bali yanadaiwa naupande wa mtawala ndio huomba kukutanishwa na upande wapiili ili waridhiane.

Wote humu hata wewe mkuu unaifaham hulka ya JPM sio mtu wakuomba maridhiano akakubali.

Mazingira ndio hulazimisha maridhiano na sio matakwa ya viongozi.Kwa Mazingira yaliyopo bado wakati wa maridhiano haujafika, mimi na wewe tusubiri tuone mikutano ijayo asipowananga cdm basi ntaamini walikuwa sahihi ingawa naamini kwa zaidi ya asilimia miamoja hatawapa nafasi ya maridhiano.

Bado nawaza walichofanya Cdm angekifanya Zitto ingekuwaje kwa wafuasi wengi wa vyama vya upinzani?.

Kitakacholeta maridhiano ni ukuta ukuta ukuta.
 
Siasa haina kanuni maalum. Una gangamala havieleweki, unajaribu maridhiano, isipoeleweka ukirejea kugangamala una hoja na lipo ulilojifunza. Mbinu za uwanjani ni nyingi, ni pamoja na kushambulia sana na kuruhusu kushambuliwa pia. Na siku zote ni kucheza kadiri timu pinzani inavyotoa changamoto.
 
Mkuu
Hata hivyo sijawahi kusoma andiko lako ambalo umetofautiana na Zitto! Inawezekana nikawa siko sahihi!

Nakumbuka sakata la Zitto na CHADEMA/Mbowe ulivyokuwa unapambana na Ben Saanane!
umenikumbusha mbali, jamaa alipambana haswa!.mwisho wa siku wote tupa kule, hawa wanaojiita waandishi wa habari wa kujitegemea wakuangalia kwa makini!.
 
Kabisa maana anafanya mambo ambayo mwisho wa siku yatamufurahisha yeye na familia yake. Haishi kutufarakanisha kila siku.
 
Zitto kapanic kwa lile walilofanya CDM jana, kashtukizwa hakutegemea, anatamani ile nafasi ingekuwa yake kwa tabia zake za ki_opportunist, toka jana ni twitter, insta habanduki huko, eti leo Zitto anataka siasa za mapambano anawafundisha CDM!, wonders shall never end, wakati ule anaenda kukutana na JK watu wanamuuliza kulikoni anasema JK ni sawa na babake, vipi leo Magufuli sio sawa na babake pia?!
Zitto kachukia sana alivyo ona Mbowe amechukua credit na ametrend sana kwenye mitandao na vyombo vya Habari dunia nzima.
 
Mkuu
Hata hivyo sijawahi kusoma andiko lako ambalo umetofautiana na Zitto! Inawezekana nikawa siko sahihi!

Nakumbuka sakata la Zitto na CHADEMA/Mbowe ulivyokuwa unapambana na Ben Saanane!
mkuu umempatia kabisa...hlf utakuta siku zote anaunga mkono maridhiano ya wakenya, huku anapinga haya, sasa hapo mbowe anatofauti gani na Raila? kama mty anamsifia Raila kuwa amekomaa kisiasa hapo hapo anaona ajabu kwa Mbowe kutumia njia hiyo hiyo ni maajabu!
 
Mkuu
Hata hivyo sijawahi kusoma andiko lako ambalo umetofautiana na Zitto! Inawezekana nikawa siko sahihi!

Nakumbuka sakata la Zitto na CHADEMA/Mbowe ulivyokuwa unapambana na Ben Saanane!
Kama nakumbuka vyema, alichokuwa anapinga Pascal ni zile njia haramu walizotumia Ben na wenzake kumshughulikia Zitto. Leo hii tunalia watu wanapodukuliwa mawasiliano yao (and we should), lakini wakati udukuzi anafanyiwa Zitto tulishangilia.
 
Ni kweli kabisa lakini ujumbe ule wa kiinjili mbele watanzani wengi unaweza kumbadili mtu kuliko pambano la kivita. Pia hauzuii kuleta pambano ikiwa sikio la kufa halikusia dawa. Namuunga mkono Mbowe.
Kaika hali ile wanaopinga wangetaka Mbowe asemeje?

Wastaafu wakuu wote wanasifia mtawala na wananchi wanapokea. Kati ya na Mbowe wastaafu nani mkweli zaidi.
Na je, mbona hatusemi lolote kuhusu wao kuitakia nchi yote mema. Ina maana wanafurahia wapinzani kuonewa?
Mbowe yuko sahihi kuliko wote waliopewa nafasi ya kusema na ujumbe wake umefika japo wenye kiburi watakomaa Pascal Mayalla,
 
Sasa ndugugu yangu Zito huwa anaongea kwa takwimu ila wewe unaleta porojo hapa.Huyo raisi wako sisi majirani zake tunaomjua asili yake ni Rwanda kwahyo tukikaa kwa kuanglia asili tutakwama aisee.Muache zito atoe uchambuzi ndoo kazi ya msomi ,sio wewe akili yako imekaaa kwenye kusifia tu.
 
RUSTEM PASHA, mkuu bora ufanye effort kuyatafuta kuliko kusema waendeleze jino kwa jino, hivi wakiendeleza jino kwa jino unadhani ni nani atakaeumia, Mbowe au Magufuli!, watakaoumia ni wananchi wa kawaida, hili walilofanya CHADEMA ni hekima iliyopitiliza. Tuliona Lowassa akiwaambia CHADEMA 2015 wakubali matokeo, ile nayo ni hekima, Lowassa angesema wasikubali unadhani kingetokea nini na angeumia nani, ni mimi na wewe huku mtaani, tusijidanganye na jino kwa jino, hakuna anaependa vita aje kuona ndugu, jamaa, na marafiki zake wakiumia, haya mambo ni kuzungumza tu, hata akigoma kwa uamuzi mapenzi yake binafsi poa, hamna tatizo.
 
Mimi mwenyewe moyo wangu umesononeka na kuumia Sana wakati naona Magufuli hayuko tayari kuona upinzani nchini.
Magufuli ameua,amefunga wapinzani,amepoteza watu na kujeruhi wapinzani kwa Risasi Leo CDM kirahisi wanasema wanataka maridhiano na CCM hapo wameingizwa chaka,umehalilisha utawala unaokandamiza haki za watanzania.

Vitu vingine ni kutumia busara tu, kwani anapungukiwa na nn kwa alichofanya jana?
Wakati Mbowe anatukanwa anasemwa vibaya ww na familia yako mko Beach mnachoma nyama tu

Jana ni sikukuu ya uhuru, mgen rasmi ni rais wa inchi na sio mwenyekiti wa chama flan sasa ulitaka mbele ya rais wa inchi aongee serikali za mitaa? Kwamba pale ni mahala pake au...

Hata kama uko tofauti na rais but uwez kuonesha tofauti zenu kwenye hadhara kama ile
 
Japo huwa simkubali Mbowe na kamwe sitarudi CDM lakini Zito ni hovyo zaidi bora Mbowe. Mbowe anaweza kuaminika na huwa ana residual za uzalendo hivyo vitu kwa zzk hakuna
Mbowe Ukiacha umugabe wake ni kiongozi mzuri sana!

Hana matusi kama ya akina Tundu Lisu na kina Lema, na wenzao wale wa ccm.
Sijawahi kusikia Mbowe katukana jukwaani au popote.
 
Ni kweli kabisa lakini ujumbe ule wa kiinjili mbele watanzani wengi unaweza kumbadili mtu kuliko pambano la kivita. Pia hauzuii kuleta pambano ikiwa sikio la kufa halikusia dawa. Namuunga mkono Mbowe.
Kaika hali ile wanaopinga wangetaka Mbowe asemeje?
Wastaafu wakuu wote wanasifia mtawala na wananchi wanapokea. Kati ya na Mbowe wastaafu nani mkweli zaidi.
Na je, mbona hatusemi lolote kuhusu wao kuitakia nchi yote mema. Ina maana wanafurahia wapinzani kuonewa?
Mbowe yuko sahihi kuliko wote waliopewa nafasi ya kusema na ujumbe wake umefika japo wenye kiburi watakomaa
Yupo sahihi kwenye jambo gani?
 
Back
Top Bottom