Leo nimekutana na clip ya Chars Hilary akiongea akitanabaisha kuwa kuna hekta elf 6 wilayani Bagamoyo ni mali ya serikali ya Zanzibar na mtu kutoka bara haruhusiwi kufanya shughuli za aina yoyote ndani ya ardhi hiyo kwani sio mali ya serikali ya Tanzania bara.

Jambo hili limenisikitisha sana and sijajua inakuwaje wazanzibari wawe na ardhi yao Tanganyika wakati mtanganyika ukifika Zanzibar ni sawa umeenda Kenya tu.

=======

Msemaji wa Serikali ya Zanzibari, Charles Hillary amesema Shamba la Zaba lililoko Makurunge wilayani Bagamoyo ni mali ya Serikali ya Zanzibar hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya shughuli yoyote eneo hilo.

Msemaji amesema Zanzibar imemiliki eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 6000 tangu mwaka 1977. Na amesema yoyete atakayeuziwa eneo katika ardhi hiyo hatalipwa fidia.

Pia soma: Zanzibar ndani ya Tanganyika ilianzia huku na 4,000 Coast villagers face land loss to investor
Chukueni na Magogoni!!!
 
Wewe ni wa dini yake hivyo huambiwi lolote, huwezi kufikiri kwa sababu ubongo umefungwa na uzanzibari. Unadhani hawa hawaoni kuwa wanauzwa na mabunduki yao? Unadhani wanafurahia kuuzwa bandari. It is a matter of time.... common sense and intuition point to that direction
Huu mnakasha ni kuhusu zanzibar kumiliki shamba la mukurunge sio Bandari
 
Mamlaka alikua nayo ndio maana aliwapa
Ardhi ya Tanganyika ni mali ya Serikali ya Tanganyika ni kuwa inakodishwa tu.
Hata hiyo ya Bagamoyo, Zanzibar ilikodishwa ili kunenepeshea mifugo tu.
Ila awamu hii mnaongea kwa ubabe sana. Mjue Kuna kesho pia.
Na hiyo hati mnayo ihangaikia sasa siyo ya milele.
Sana sana mtapewa ya miaka 90 ila kisheria ni miaka 30 tu.

Zanzibar hamna kipande cha ardhi Tanganyika. Na hamta kuja kuwa nacho.
 
Tanzania ni nchi moja ya JMT, ambapo Zanzibar ni sehemu ya JMT, SMZ na Mzanzibari yoyote yuko huru kumiliki Ardhi huku kwasababu kila Mzanzibari ni Mtanzania, ana haki zote za Utanzania ikiwemo kumiliki Ardhi.

Ranchi ya Makurunge iliyopo Bagamoyo ni mali halali ya SMZ. Tena tuna bahati wakoloni Wajerumani walitusaidia, ukanda wa maili 10 za Pwani yote ya bahati ya Hindi kuanzia Sofala hadi Mombasa ilikuwa ni mali ya Sultan of Zanzibar!. Sultan alipewa eneo hilo na mkutano wa Berlin kugawana Africa ile 1884. Miaka 6 baadae 1890, ndipo Ujerumani, na Uingereza wakaingia mkataba za Sultan of Zanzibar awaachie, na wao wakaahidi kumlinda.

Mkataba huo unaitwa The Zanzibar Treaty, huku Ujerumani na Uingereza wakiachiana maeneo, visiwa vya Witu na Helingoland, na ni mkataba huu ndio wakahamisha mipaka ya Ziwa Nyasa kulifanya la Malawi!.
P
Hao Wajurumani walikuwa na uhalali gani wa kumiliki na kuigawa ardhi ya Tanganyika kwa Sultan?
Unadhani kwa nini Wajerumani hawakumgawia Sultan kipande cha ardhi pale Berlin au Born au Frunkfurt?
Elimu ikusaidie kufikiri bhana.
 
Mlipoambiwa kuna siku nchi itapigwa mnada na aliyesema akalazimishwa kujiuzulu unadhani ilikuwa bongo movie?
"Ipo siku mtanikumbuka, na najua mtanikumbuka kwa mazuri"
Kuna nwanasiasa mzalendo wa upinzani aliwahi kuonya kwamba" ikitokea tukapata rais mwenye mpenzi nje ya Tanzania ,akapewa mapenzi akanogewa,basi atagawa rasilimali zetu kama njugu." Je ,ndo unabii unatimia?

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Ardhi ya Tanganyika ni mali ya Serikali ya Tanganyika ni kuwa inakodishwa tu.
Hata hiyo ya Bagamoyo, Zanzibar ilikodishwa ili kunenepeshea mifugo tu.
Ila awamu hii mnaongea kwa ubabe sana. Mjue Kuna kesho pia.
Na hiyo hati mnayo ihangaikia sasa siyo ya milele.
Sana sana mtapewa ya miaka 90 ila kisheria ni miaka 30 tu.

Zanzibar hamna kipande cha ardhi Tanganyika. Na hamta kuja kuwa nacho.
Kipo sii ndio hicho cha makurunge
 
Back
Top Bottom