JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Amesema “Eneo linaitwa Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA), marehemu Rais Julius Nyerere alilikabidhi kwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Abood Jumbe, lilikuwa likitumika kuwanenepesha ng’ombe kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar.
“Kulikuwa na Meli inaitwa Jitihada iliyotumika kuwasafirisha ng’ombe, baadaye mradi huo ulififia na hakukuwa na ng’ombe wanaosafirishwa, eneo likabaki tu kwa muda mrefu.
“Watu wengi wameona liko tupu wakanza kuvamia, kuna watu walianza kuuziwa na wengine wakawa wanaambiwa jenga haraka.”
Alipoulizwa kuusu Hati
“Kuhusu nyaraka zikiwemo Hati zinafanyiwa kazi kwa sasa.”
"Tulipoona uvamizi unaendelea ndipo tukatoa taarifa, eneo hilo lina ukubwa wa Hekari 6,000, kabla ilikuwa zaidi ya 17,000, likapunguzwa kwa makubaliano ya Zanzibar na hao waliogaiwa.
“Sehemu ya eneo hilo pia linaingia shamba la miwa la Bakhresa, kwa sasa Serikali inaangalia na muda mfupi ujao tutajua kitakachofanyika pale.”