Serikali ya Zanzibar kuchukua na kumiliki eneo Bagamoyo ambalo liko Tanganyika ni kinyume na katiba ya Zanzibar

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
Ndugu zangu majira ya jana 31th May 2023 Ikulu ya Zanzibar kupitia msemaji wake ilitoa taarifa kwa umma kwamba inamiliki shamba la hekta elfu 6 huko Wilaya ya Bagamoyo upande wa Tanzania Bara. Kwamba ardhi hiyo ni mali ya serikali ya Zanzibar kwa ajili ya wazanzibar hivyo ni marufuku mtu yoyote kutoka Tanzania Bara kutumia eneo hilo hata kama anatoka hapohapo Bagamoyo.

Baada ya kuona, kusikiliza na kusoma taarifa hiyo nilipigwa na butwaa. Nilijiuliza kwamba hili jambo linawezekanaje? Kwani kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar Ibara ya 1 inasema; ๐™•๐™–๐™ฃ๐™ฏ๐™ž๐™—๐™–๐™ง ๐™ฃ๐™ž ๐™‰๐™˜๐™๐™ž ๐™–๐™ข๐™—๐™–๐™ฎ๐™ค ๐™š๐™ฃ๐™š๐™ค ๐™ก๐™– ๐™ข๐™ž๐™ฅ๐™–๐™ ๐™– ๐™ฎ๐™–๐™ ๐™š ๐™ฃ๐™ž ๐™š๐™ฃ๐™š๐™ค ๐™ก๐™ค๐™ฉ๐™š ๐™ก๐™– ๐™‘๐™ž๐™จ๐™ž๐™ฌ๐™– ๐™ซ๐™ฎ๐™– ๐™๐™ฃ๐™œ๐™ช๐™Ÿ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™‹๐™š๐™ข๐™—๐™– ๐™ฅ๐™–๐™ข๐™ค๐™Ÿ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™‘๐™ž๐™จ๐™ž๐™ฌ๐™– ๐™ซ๐™ž๐™™๐™ค๐™œ๐™ค ๐™ซ๐™ž๐™ก๐™ž๐™ซ๐™ฎ๐™ค๐™ž๐™ฏ๐™ช๐™ฃ๐™œ๐™ช๐™ ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™—๐™–๐™๐™–๐™ง๐™ž ๐™ฎ๐™–๐™ ๐™š ๐™–๐™ข๐™—๐™–๐™ฎ๐™ค ๐™ ๐™–๐™—๐™ก๐™– ๐™ฎ๐™– ๐™ˆ๐™ช๐™ช๐™ฃ๐™œ๐™–๐™ฃ๐™ค ๐™ฌ๐™– ๐™๐™–๐™ฃ๐™œ๐™–๐™ฃ๐™ฎ๐™ž๐™ ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™•๐™–๐™ฃ๐™ฏ๐™ž๐™—๐™–๐™ง ๐™ž๐™ ๐™ž๐™ž๐™ฉ๐™ฌ๐™– ๐™…๐™–๐™ข๐™๐™ช๐™ง๐™ž ๐™ฎ๐™– ๐™’๐™–๐™ฉ๐™ช ๐™ฌ๐™– ๐™•๐™–๐™ฃ๐™ฏ๐™ž๐™—๐™–๐™ง.

Kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar eneo la Bagamoyo ambalo liko Tanzania Bara si sehemu ya Zanzibar. Hivyo basi sisi watu wa Tanzania Bara au Tanganyika ni vema tukapewa ufafanuzi inakuwaje Zanzibar ikamiliki ardhi ya Bara Tanganyika? Mipaka ya Zanzibar inajulikana na uzuri umeainishwa katika katiba ya Zanzibar yenyewe hivyo ni vema tukaambiwa uhalali wa Zanzibar kumiliki eneo hilo. Kama walinunua tuwekwe wazi na kama walihongwa pia tuwekwe wazi.

Kama hatutawekwa wazi basi huu muungano hatutafika nao mbali maana haiwezekani ardhi ya Tanganyika inatumiwa na watanganyika na Wazanzibar lakini ardhi ya Zanzibar inatumika kwa wazanzibar pekee huku Watanganyika au watu wa Bara wakinyimwa fursa ya kumiliki ardhi Zanzibar.

Ni wakati wa sisi wazalendo wa Tanganyika kwenda mahakamani kuhoji uhalali wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuchukua na kumiliki ardhi ya Tanzania bara kinyume na katiba ya Zanzibar yenyewe. Tunahitaji ushauri wa mawakili kwenye jambo hili na pia tunahitaji ufadhili kama inawezekana kufungua kesi. Hujuma za namna hii dhidi ya Tanganyika hazipaswi kukaliwa kimya maana haiwezekani wananchi wa Bagamoyo Tanganyika au Bara wakanyang'anywa ardhi na kupewa wazanzibar wakati huko Zanzibar hakuna wananchi wanaonyang'anywa ardhi na kupewa watu wa bara. Tukikaa kimya kuna siku Loliondo na Ngorongoro huko wanakoondolewa Maasai kwa mtutu wa Bunduki tutaambiwa ni mali ya Zanzibar.

Mwisho, kero za muungano mwarobaini wake ni rasimu ya Warioba ya serikali tatu. Ni vema tutakapoanza mchakato wa Katiba mpya msingi wetu uwe Rasimu ya Warioba ambayo ni mkusanyiko wa maoni ya wananchi Zanzibar na Tanganyika. Tofauti na hapo hatuwezi kuendelea kuwa na muungano huu ambao umejaa malalamiko kutoka pande zote.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
Screenshot_20230601-111750_1.jpg
Screenshot_20230601-111856_1.jpg
 
Nadhani hili eneo Zanzibar ilipewa kama wawekezaji walitumie kama ranch kufuga ng'ombe na si kwamba ni himaya ya Zanzibar.
kama hali ni hiyo, basi charles hilary hana uwezo kuwa msemaji wa serikali ya hako kawilaya. alivyoongea utafikiri yeye anamiliki tanzania. kulikuwa na shida gani kusema kuwa ranch hiyo ipo chini ya uwekezaji wa zanzibar?
 
Wameanza na Bagamoyo na tukiendelea kukaa kimya mtasikia na Eneo la Ikulu ya Magogoni ni Mali ya Serikali ya Zanzibar.

Isije kuwa eneo Hilo la Hekta 6000 labda walipewa kama masharti ya wao kujiunga na Tanganyika, who knows ๐Ÿ˜Ž
 
Nadhani Zanzibar kapewa eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji!Na kuna ukomo,lingekuwa ardhi ya zanzibar basi wazanzibar wangeuziwa maeneo na kujenga huko!
Nafikiri Zanzibar wanapaswa kunyang'anywa ardhi hiyo na kurejesha umjliki kwa JMT maana toka 77 hawajaliendeleza na kuna kipindi serikali ilikuwa ikitaifisha maeneo iliyotoa kwa wawekezaji na hayakuendelezwa!
 
"ukitaka kula lazima uliwe"in kikwete's voice!

Tumeamua kuungana na zanzibar lazima tukubali kuliwa ndio tule kama Ally karume hapendi kuliwa Bas ni yeye lakini uamuzi wa nani awe Rais wa Zanzibar unaofanyikia chimwaga Dodoma ndio kula kwenyewe!

Tunataka nini tena!!?
 
Nadhani Zanzibar kapewa eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji!Na kuna ukomo,lingekuwa ardhi ya zanzibar basi wazanzibar wangeuziwa maeneo na kujenga huko!
Nafikiri Zanzibar wanapaswa kunyang'anywa ardhi hiyo na kurejesha umjliki kwa JMT maana toka 77 hawajaliendeleza na kuna kipindi serikali ilikuwa ikitaifisha maeneo iliyotoa kwa wawekezaji na hayakuendelezwa!
wananchi nao wanasubiri nini kuvamia? limeni mananasi.
 
Wameanza na Bagamoyo na tukiendelea kukaa kimya mtasikia na Eneo la Ikulu ya Magogoni ni Mali ya Serikali ya Zanzibar.

Isije kuwa eneo Hilo la Hekta 6000 labda walipewa kama masharti ya wao kujiunga na Tanganyika, who knows ๐Ÿ˜Ž
" ...hatari ya kutokushirikishwa kwenye majadiliano mezani ni kukaribishwa mezani kula.."Mwisho wa kunukuu
 
Back
Top Bottom