Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Vikao vya CHADEMA: Tundu Lissu aibuka kidedea kuwania Urais wa Tanzania kwa kupata kura 405 dhidi ya Nyalandu 36 na Dkt. Majige 1

Mkuu Nyalandu sio pandikizi. Isipokuwa sio mgombea sahihi kwa sasa.
Watawala wa kiimla na wababe wanatakiwa kukutana na watu kama Lissu ambaye amesema ukiiba kura hakuna cha kusema 'tunamuachia Mungu'
Chakaza, shida yangu hadi kusema ni pandikizi, ni jinsi mambo ya zamani kumhusu hasa ya vitalu na nyara wakati akiwa Waziri MNRT. Kwa zile tuhuma ambazo magazeti ya kiuchunguzi yaliandika, asingekuwa mtu wao, wangekwisha kula nyama.

Sasa tutarajie makubwa kuibuka juu yake. Labda huko ccm kila mtu hadi Baba yao nafsi ziwasute maana rushwa na janjajanja ndio uti wa mgongo wa chama hicho. Vinginevyo, tutarajie mambo ya ajabu na ya aibu ndani ya chama chao. Umesikiliza clip ya Mary Mwanjelwa?
 
Hizo Ni Movie tuu
movie kivipi mkuu, na uchaguzi ulikuwa wa wazi. Maana kura baada ya kura iligawiwa na kuonekana. Isitoshe wiki kabla ya uchaguzi tulisikia kuwa Nyalandu ni tajiri na kapenyeza Rupia kwa wajumbe wote ili wamchague. Swali langu, sasa kulikoni?

Hata kuna swali moja mjumbe wa kike alimuuliza Lissu kuhusu kivipi ataghamia uchaguzi? Nikahisi kuna mtu katangaza kugawa pesa kwenye uchaguzi toka wajumbe mpaka boda boda.
 
Chakaza, shida yangu hadi kusema ni pandikizi, ni jinsi mambo ya zamani kumhusu hasa ya vitalu na nyara wakati akiwa Waziri MNRT. Kwa zile tuhuma ambazo magazeti ya kiuchunguzi yaliandika, asingekuwa mtu wao, wangekwisha kula nyama.

Sasa tutarajie makubwa kuibuka juu yake. Labda huko ccm kila mtu hadi Baba yao nafsi ziwasute maana rushwa na janjajanja ndio uti wa mgongo wa chama hicho. Vinginevyo, tutarajie mambo ya ajabu na ya aibu ndani ya chama chao. Umesikiliza clip ya Mary Mwanjelwa?

Hiyo clip ya Mwanjelwa sijaisikiliza labda unipe link, nitashukuru. Kuhusu wizi ndani ya wizara yake labda niseme kitu. Wizi na ubadhilifu ndani ya CCM ni mfumo, kila mmoja ndani yao ni mwizi na fisadi kuanzia namba moja kuja chini.

Ukiona anatajwa tuu na hakuna anayechukua hatua ujue ulikuwa wizi wa kimfumo na hats chain nzima kuanzia boss wake walihusika
 
Sitaki kuulizwa maswali mengi, naiona upepo unaenda kuvuma tofauti kabisa.Huenda historia mpya ikaandikwa katika nchi yetu.

Rais Mafufuli ni mwenyekiti wangu wa chama na nunampenda sana lakini kwa hali ya maisha ilivyo wacha nijaribu uamuzi mwingine. Upepo wa Lissu unanifanya nione hali ya mabadiliko huko mbeleni.

Hali ya maisha ni ngumu imepelekea watu wengi kukata tamaa siwezi kua mnafki kisa eti mimi CCM hapana.
 
Wakuu natumaini kuwa mko poa!

Leo nina kasherehe kadogo hapa home kusheherekea nusu ya ushindi wa Bw. Tundu Lissu. Jogoo mkubwa nishamnunua Bugurui na mazaga mengine.

Karibunu sana. Si kwamba sichinjagi majogoo home, la bali huyu wa leo nimemchinja kwa furaha ya ushindi wa Lissu jana.
Hatua ya jana ni kama nusu ya safari ya ushindi.

Tukutane October 28. Onyesha viwanda 8477 ulivyojenga tukupe kura !
 
Back
Top Bottom