Salaam, Shalom!!
Tukiwa msibani, tuendelee kupiga stori kidogo!!
Chama Cha DEMOKRASIA na Maendeleo CHADEMA, kilianzishwa May 1992 na Ndugu Mtei aliyewahi kuwa Governor wa Benki kuu ya Tanzania.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, CDM haikusimamisha kabisa mgombea Urais, Nia ilikuwa ni kusoma mchezo wa siasa za Nchi hii, na kuunga mkono chama kilichokuwa na nguvu Kwa wakati huo.
Mwaka 2005, CDM, ilisimamisha mgombea Urais Kwa mara ya kwanza, Mgombea Urais huyo wa wakati huo aliitwa Ndugu Freeman Aikael Mbowe. Baada ya Uchaguzi huo, chama kikaanza kuenea Kwa Kasi, hii ni baada ya Aliyekuwa mgombea Urais wa chama hicho, kuamua kuongeza juhudi ya kulijenga chama.
Mwaka 2010, chama hiki, kiliamua kuja na mgombea Urais mwingine tena, time hii, alikuja ndugu Dr Wilbroad Slaa. Chama kikaendelea kupata uungwaji mkono zaidi.
Mwaka 2015, Dr Slaa alitamani sana kugombea tena akiamini ana nguvu na umaarufu wa kutosha kushinda uchaguzi, lakini kama kawaida ya Chama hiki, kikamramba chenga ya MWILI na kumleta mgombea mpya tena, Time hii, ilimchukua Mzee Lowassa Kutoka timu pinzani Kwa Imani kuwa ingizo Hilo, litaleta tija, na Kweli, tuliiona mambo yalibadilika.
Mwaka 2020, Chama kikatuletea mgombea mpya tena, mgombea Machachari, Ndugu Tundu Antipas Lissu, inasemekana, pasingelikuwa na changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi Ule, chama kingepiga hatua kubwa zaidi.
Kwa trend hii, CDM imeonyesha DEMOKRASIA ya hali ya juu, maana Kila baada ya miaka mitano, imebadili mgombea tofauti na chama Dola, CCM, wao Kila baada ya miaka 10 ndo hubadili mgombea Urais,labda itokee ameitwa mbele za HAKI!!
Kuelekea 2025, CDM itaendeleza Utaratibu huu wa kuja na mgombea mpya, au itaangalia kati ya wagombea Bora waliopita na kutuletea mojawapo?
Kwanini CDM haikuwa ikirudia wagombea Urais kama CCCM
na CUF ya Lipumba?
Karibuni 🙏