Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,016
- 9,885
Akielezea suala linaloendelea kuhusu mkataba wa DP-World na Tanzania ametoa sababu kuwa ni utendaji kazi mdogo wa TICTS ambao umesababisha meli nyingi ziwe zinashushia mizigo Lamu, Mombasa au Afrika kusini hali ambayo imepunguza wateja wa Bandari ya Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema utendaji mbovu wa bandari unasababisha meli zitumie muda mwingi bandarini ambapo gharama ya meli kubaki bandarini huingia mfanya biashara hivyo bidhaa kuwa ghali mtaani. Amesema kwa sasa meli hutumia hadi siku saba kwa mzigo kupakuliwa.
Aidha, amesema awali TPA ilitambua utendaji mbovu na kumpa TICTS mkataba kwa miaka 20 lakini hakukuwa na utendaji mzuri ambapo mkataba huo uliisha 2017 na baadae aliomba kuongezewa miaka mitano ambayo imeisha 2022 na bado hakuweza kuleta vifaa vipya vya kuhudumia bandari.
Waziri Mkuu ameonesha suala la mkataba wa DP-World litarahisisha upakuaji wa mizigo.
Watanzania wametaka maelezo baada ya kuwa na utata katika baadhi ya vipengele vya mkataba huo ambao kwa kiasi kikubwa serikali na spika wa bunge wamekuwa wakivitolea maelezo.
Habari zaidi, soma: